Kilio wafanyakazi Vodacom Huduma kwa wateja. ISON BPO ni Fyonzaji, Erolink Ltd cha mtoto

Naam
Wakuu, leo hii majira ya saa nane mchana, nilipita mlimani city ilipo HQ ya Vodacom Tanzania.

Safari yangu hii ilikua ni kwa ajili ya kuonana na marafiki zangu niliosoma nao chuo wanaofanya kazi pale na ndipi nilipoona ukweli wa ule usemi kuwa, "utaona umuhimu wa kitu pale tu utakapokipoteza".

Wengi tunajua kuwa erolink ilikua ni kampuni inayorun operations ktk call center ya Vodacom kwa ufyonzaji mkubwa. Well, mwezi wa tano mwaka huu, walishindwa bid ya kuendelea kuoperate call center ya Vodacom na kampuni ya ISON BPO (ambayo ilikuwa tigo call center) ikawin hiyo bid.

Wafanyakazi wa call center walitegemea mabadiliko chanya kutoka kwa ISON BPO but mambo yamekuwa hoi zaid ya yalivyokua kwa erolink. ISON wamecopy kila kitu kutoka kwa erolink na kuondoa baadhi mambo muhimu kama night allowance (ambayo ipo kisheria) kwa shift za usiku. Erolink walikuwa wakilipa night allowance but ison wameondoa.. Nimeona copy ya mkataba wao.

ISON wanawafanyisha kazi wafanyakazi wale kwa masaa 9 kwa siku but masaa yanayolipwa ni 8 tu. Yaani lisaa limoja hawalipi kwa madai kwamba, lisaa hilo mfanyakazi anakua amekwenda lunch na tea. Kwa utaratibu wao, lunch ni dk 40 na tea ni dk 20. Hizo hawalipi japo umezitumia ukiwa ndani ya masaa ya kazi. (hili sijui limekaaje kisheria - wataalamu wa sheria tusaidiane). Erolink walikua wakilipa muda wa tea na lunch.

Kwa mujibu wa ISON, unapewa break ya dk 40 za lunch na 20 za tea. Hupewi muda wa washroom. Wapo strict sana. Mfanyakazi anakaa kwenye system masaa hadi manne au matano kabanwa mkojo anaogopa kutoka kisa hana dk za washroom. Huu ni Unyanyasaji mkubwa.

Tena nilichokishangaa zaidi, ni pale ambapo, ule muda wa dk 40 na 20 za break, inabidi wafanyakazi waje wakaulipie kwa kufanya kazi siku ya sita kwa masaa matano. Kulipia yale masaa waliyoenda break ktk siku tano za kazi.. This is bulshit. Yaani wafanyakazi nimekuta wakilalamika na kusema bora erolink.

Makampuni kama haya ya kidalali yanayokuja nchini na kuwanunua wafanyakazi wa kitanzania kwa bei rahisi na kuwauza bei ghali, yanahitaji kupewa mwongozo chanya usiowatesa watanzania.

Yaani vodacom inatoa 800,000+ kwa kila call center agent but, hizi kampuni Fyonzaji, zinakata nusu ya mshahara huo na kuwalipa basic salary ya 400,000. Makato yakipita hapo, mshahara unakua 310000 hivi. Hapo bado kampuni husika inalipwa pesa za kurun operations. Serikali inabidi irekebishe ile sheria ya kazi ya 2004 inayosema minimum salary kwa wafanyakazi wa makampuni ya simu iwe 400,000 gharama za maisha zimepanda. Huo mshahara ni mdogo kwa life la sasa.

Anyways, nimewahasa vijana waendelee kupiga kazi huku wakicheki mishe zingine. Maana kazi ya call center ni ngumu mno.. Ila hiyo waliyoipata wasiiache kwanza hadi wapate kazi zingine. Mtaani pagumu.
Hii ishu iliendeleaje.. nimekutana na muhanga wa hiyo spanco anawaponda sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom