KILIO TANZANIA NI KILIO CHA KUJITAFUTIA

Wandagara

Member
Aug 4, 2016
70
39
Usiambiwe tu ukapenda nakuitikia ndio hapohapo. Fikili kwanza kwanini umeambiwa na ndipo utoe jibu la kukubali au kutolidhiana na jambo hilo. Rais wangu wewe ni mchapakazi sana na huruka hii ya uchapakazi na uadilifu ulionao umefanya hata walionyuma yako kuwa wa ndio tu. Ndo maana leo napata huzuni linapokuja swala la MIKOPO kwa wanavyuo wa mwaka 2016/17 napatwa na ukakasi maana majibu niyasikiayo nikama kunifanya mimi niende nchi jilani na kuwa mkimbizi. Eti leo wanasema watapewa mikopo kulingana na ufaulu wao mpaka wamechaguliwa hapa kuwa na hoja kama izi na wamechaguliwa kwanini kama hawana sifa za kusomeshewaa? Huu ni mkopo si kwamba wanasomeshwa bure inamaana bodi ya mikopo ina viongozi mbulu mbulu sana mpaka nao wanashidwa kusima kama watanzania duni wanaojua nchi na wakazi wa nchi yao kimaisha na kiuchumi? Mheshimiwa Rais ivi karibuni ulitoa tamko hutapenda kuona watanzania wakiteseka wa kipato cha nchini lakini watu dhaifu na duni ni wanachuo wa elimu ya juu mbali na kusema wanaharibu pesa za mkopp kwa kunywa pombe naomba niulize ni utafiki wa aina gani ulifanywa na kujua wanatumia vibaya pesa izo lakini si ni mkopo? Mh. Rais Magufuri mie sikuingilii katika majukumu yako ila nasema Kila mtu atahukumiwa kulingana na matendo yake. Wewe unapenda ukweli ndo ulivyojipambanua lakini kumbuka maneno yako maana waenga wanasema maneno yanaumba. Mungu anakuona kama utasahau maneno yako uliyoyasimamia kwa siku 63 kabla yakukalia kigoda hicho chenye kuitaji hofu ya Mungu.

Note: wizara ya elimu msikulupuke tu mana kama waliomba mikopo ni 70000 na kila mmoja alilipia 50000 hii inamana mna kianzio cha Sh. 3,500,000,000 huu ni mfano tu mjue hata sisi tulio nje tunamtizamo chanya kwa ajili ya taifa letu.

Vijana wenzangu tuwe na mtizamo mpana maana tunaoumia ni sisis tusikulupuke maana kimya nalo ni jibu linaloumiza kuliko kelele zinazoqapatia uwezo wakusema.

Mungu mubaliki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JP Magufuri.

Magesa J Mugeta
 
Kwa hesabu yako hiyo (ada ya 50000 kuomba mkopo) ni dhahiri kwamba zikitumiwa kama zawadi na Bahati Nasibu ya Taifa, zitapatikana fedha za kutosha za mkopo kwa wanafunzi mwakani, wakiunganisha na bahati nasibu zinazochezeshwa na mitandao ya simu kila kukicha.

ELIMU KWANZA
 
Back
Top Bottom