Kilio kwa mh raisi dhidi ya wizara ya kilimo waziri huyu hafai

pedali

New Member
Dec 31, 2013
1
0
WAZIRI WA KILIMO "MZIGO", MWENYEKITI WA BODI TPRI "MZIGO" NAMKURUGENZI TPRI "MZIGO"
Ndugu zanguwana jamii , pengine wengi mtakuwahamlifahamu shirika nyeti nchini la TropicalPesticdes Research Institute – TPRI. Shirika hili ni nyeti sana katikasekta adhimu ya kilimo nchini. Shirika hili lilianzisha toka enzi za watumakini (objective)wenye akili japo wakoloni, mwaka 1945. Baadae shirika hililikawa la Jumuia ya Africa mashariki na baada ya kuvunjika, mtu mwingine makini"Baba wa Taifa" akaamua kuliimarisha, kuliendeleza na kulifanya kuwa shirika laumma kwa sheria ya Bunge Na. 18 ya mwaka 1979. Lengo la kuanzishwa kwa shirikahili ni kufanya utafiti wa Viuatilifu (Pesticides) dhidi ya visumbufu (Pests)katika ukanda wa Kitropiki ambamo nchi yetu imo. Utagundua hapa unyeti washirika hili katika nchi yetu ambapo hata sasa 70% ya watu wake ni wakulima nauchumi unaotegemea kilimo, pamoja na hayo shirika hili kama ilivyo kwa TBS naTFDA ndilo linalosajiri, kuhakiki na kudhibiti matumizi ya viuatilifu ambavyokwa ujumla ni sumu.

Hivi sasakwa vile dunia imekuwa kijiji na kutokana na maingiliano makubwa ya biasharaduniani (utandawazi), mahitaji ya udhibiti wa viutatilifu ili kulinda afya yajamii yanasisitizwa duniani kote. Katika kipindi hiki, nchi/mtu yeyote hatawezafanya biashara ya mazao ya kilimo yeyote hata nyama, maziwa asali n.k. na hasakatika nchi za Ulaya na Amerika iwapo nchi/mtu huyo hatazingatia viwangovilivyokubalika duniani vya masalia ya viuatilifu (Minimum Residue Limits – MRL).Kumbe hapa ndipo umuhimu wa taasisi ya TPRI ambayo ni pekee Tanzania na Afrikamashariki unapoonekana.

Sasa nihivi, shirika hili kama umri wake unavyojiakisi, limetumia rasilimali nyingi zaTaifa na umma wa Watanzania, kwa maana ya mtaji uliowekezwa, miundo mbinu yakipekee, maabara na vifaa ghali, lakini pia Rasilimali watu yenye wasomiwaliobobea katika masuala hayo mtambuka.
Je? Nduguzangu wana jamii na wazalendo wote kwa ujumla mpo tayari kuliona shirika hilinyeti na muhimu katika uchumi wetu wa sasa na urithi wetu toka kwa Baba namuasisi wa taifa hili linakufa? Tena kwa ajili ubadhirifu na maslahi ya watuwachache kwa ushwahiba wa viongozi na ubabe?
Hebutuangalie wanajamii; Mkurugenzi Mkuu aliyeteuliwa hana sifa wala uwezo,Mwenyekiti wa Bodi hana uwezo na Waziri Mh. Chiza anawalinda pamoja na baruanyingi/taarifa nyingi za uozo huo alizoandikiwa.

Nawasilisha,soma uozo huo hapo chini

BARUA YA WAZI KWA WAZIRI MH. CHIZA.
YAH: PROF. MS. PILI KALUNDE SIBUGA NAMKURUGENZI MKUU MRS. EPIFANIA .E. KIMARO HAWAFAI KUWA VIONGOZII TPRI
Kumezukamtindo wa kinyemela wa jinsi ya uendeshaji shirika nyeti la TPRI, mara zote ukituachahoi wana wa TPRI kwa namna mbalimbali lakini hasa pale uteuzi unapofanyika kwakinyemela. Awali Mkurugenzi mkuu wa TPRI aliteuliwa kimya kimya na baadaeakajitokeza yeye mwenyewe mbele za wafanyakazi na kujitangazia utawala wake.Safari hii imefanyika kwa mtindo huohuo kuteua mwenyekiti wa bodi ya TPRI,uteuzi ambao tunautafsiri kutokea katika mazingira yasiyo ya kawaida na pengineya kuja kuimalizia TPRI kwa kadiri tutakavyoainisha katika waraka huu kwako.Kilichotushangaza hapa ni jinsi mwenyekiti huyu kinyume na ilivyo jadi yetuTPRI, kuteuliwa kwa muhula wa tatu wa miaka mitatu! Kawaida Mwenyekiti wa BodiTPRI hudumu kwa vipindi viwili tu vya miaka mitatu kisha hubadilishwa. Haiingiiakilini hata kidogo kuwa ameongezewa muhula wa tatu kwa utendaji uliotukuka .

Historiainaonyesha kuwa Prof. Pili Kalunde Sibuga yupo ndani ya taasisi ya TPRI kwaumri mrefu wa ujana wake, baadhi ya wataafu wanadai wangekuwa wameajiriwa wotebasi leo wote wangekuwa wastaafu. Yawezekana kabisa basi mpaka hapo alipoanza kuwa mwenyekitiwa bodi mwaka 2006 jumla atakuwa na umri usiopungua miaka 20 ndani ya TPRI.Nakumbuka uteuzi wake ulileta matumaini makubwa ndani ya taasisi kwamba sasatumepata Mwenyekiti wa bodi ambae analifahamu fika shirika la TPRI na ambaeatakua msaada mkubwa kwa taasisis yetu. Pamoja na mishangao, matumainiyaliongezeka kwamba pengine wangefanya timu nzuri na Mkurugenzi mkuu ambae naeamekuwapo kwa muda mrefu ndani ya TPRI, kwa kifupi haya yalikuwa matumainiambayo leo nadiriki kuyasema yasiyokutana. Nadiriki sasa kusema pengine kuwepokwao ndani ya TPRI kwa muda mrefu mpaka uteuzi wao, pengine ulizingatia zaidi Jinsia,kuliko uwezo wao kikazi, kwani TPRI ilipo sasa iko hoi bin taaban.

Toka uteuziwake (2006) Prof. Pili Kalunde Sibuga hajawahi kukutana na wafanyakazi walawawakilishi wao kwa madhumuni ya kutaka kuwajulia hali, kujua matatizo, walamafanikio pamoja na kuonekana wazi kwa matakwa hayo toka kwa jumuia ya wanaTPRI. Muhula wake wa kwanza, Prof. Pili Kalunde Sibuga na wajumbe wa bodi yakewalikuja kujitambulisha mbele za wafanyakazi kwa kikao kifupi tu na kishaaliwataka wafanyakazi kuwa na subira kwani angerudi kwa kikao maalumu kuongeanao, jambo ambalo hakulifanya katika kipindi chote ila pale alipokuja kuagakwamba amemaliza muhula wake. Vivyo hivyo kwa lugha na mtindo uleule alirudiaalipoteuliwa kipindi cha Pili, isipokuwa mara hii kwa kujua fika, juu ya wanaTPRI walivyoumia,kulalamikia utendaji wake mbovu na kupata minong'ono yakulalamikiwa juu ya tabia yake hiyo safari hii hakutaka hata kuja kutuaga,akaingia mtini. Tukafunika kombe mwanaharamu apite kama wasemavyo wahenga,akaenda zake. Kweli muonja asali haonjimara moja, maana tungelitegemea Prof. Pili Kalunde Sibuga asingekubali kuruditena TPRI maana alijua alichokifanya. Lakini tayari tunae na mambo yaleyaleyamejirudia, safari hii akipingana hata na kile alichokua akikifanya awamu zotembili, huyu ndio Profesa Pili Kalunde Sibuga, msomi ambae haoni umuhimu wa mtotokumjua baba au mama yake, analo lake!
Tunadirikikusema kuwa kipindi cha pili cha Prof. Pili Kalunde Sibuga, ni kipindi mfu kwaTPRI kuliko kipindi chote kingine TPRI imewahi kukipitia na uteuzi huu wa awamuya tatu tunahisi amekuja kumalizia kuiuwa taasisi yetu muhimu katikamustakabali wa kilimo na uchumi wa taifa.

Kwa nini tunayasema haya, tahmini yautendaji wa Prof. Pili Kalunde Sibuga ndani ya TPRI umekuwa wa kibubu,kimaslahi na mafungate zaidi, na hata pale alipopata mawasiliano toka kamatinyeti za maamuzi na ushauri, kama vile Baraza la wafanya kazi au ajira nanidhamu aliendelea kukaa kimya bila mjibuko. Wakati haya yakitokea upande mmojakwa upande wa Pili wa Mkurugenzi mkuu, wamekuwa na mawasiliano ya karibu, hukuwakifanya vikao vingi vya Bodi na vya Sekretariati ya Bodi bila kujali ufinyuwa bajeti ya taasisi, maslahi ya taasisi na wafanyakazi. Mawasiliano ambayohakika yanaashiria fungate kubwa kati yake na Mkurugenzi ambayo wizara inaonekanakuayaunga mkono. Upo uwezekano mkubwa kwamba Mkurugenzi Mrs. E.E. Kimaro na Prof.Pili Kalunde Sibuga wamecheza pele kuhakikishiana nyadhifa zao chini ya uungwajimkono wa wizara na hasa mpambe wao DAP wa wizara Bw. Shayo akiwapa "support" yakiwizara!

Katikakipindi cha Prof. Pili Kalunde Sibuga, kumekuwapo kuzorota kwa kazikulikokithiri na mauzauza mengi. Maabara zimesimama kwa kukosa vitendea kazi,hata pale ambapo wateja binafsi wamekua wakilipa fedha nyingi ambazozingetumika kununua vitendea kazi vya msingi kufanikisha hilo. Kumbe kumekuwapona mtindo wa Wateja kulipa pesa na kazi kutofanyika kwa wakati au kutokufanyikakabisa. Vituo vya kazi vya nje (Out station) Tunduma, Namanga, Horohoro, silarivimekufa, na matokeo yake Viuatilifu feki vimejaa kila sehemu. Hivyo, viliovingi vinavyosikika sasa toka kwa wakulima kama vile wa Pamba, Kahawa naKorosho na pia kuathirika kwa Afya za watu na mazingira inatokana na viuatilifufeki vinavyopita bila ukaguzi mipakani.

TPRI inavyanzo vingine vingi vya fedha vya ndani lakini chini ya uongozi wa Prof. PiliKalunde Sibuga na Mkurugenzi mkuu Mrs. E.E Kimaro tumeshuhudia upotevu wa pesauliokithiri kwa mfano; Kushuka kwa mapato ya ndani kusikokuwa na maelezo yamsingi kutoka 800m mpaka 350m katika kipindi cha 2012/13; Wizi wa mishara yawafanyakazi wa zaidi ya 300m ambao kama isingekuwa Benki ya NMB wizi huuusingegundulika, wizi ambao umetokea katika kipindi ambapo Mkurugenzi mkuu Mrs.E.E Kimaro akiwa ndio "signatory" pekee wa akaunti za TPRI; kukithiri kwauhodhi wa madaraka wa Mkurugenzi mkuu kulikopelekea kujiuzulu kwa wajumbe wotewa menejimenti yake ya awali; kuvunjwa kwa sera/ kamati/ miongozo na taratibuzote zinazosimamia maamuzi ya taasisi na kisha mambo yote kubakia kwaMkurugenzi na Mwenyekiti wa bodi tu; kuvunjwa kwa kamati ya ajira na nidhamu;wakuu wa idara na vitengo kubaki wakikaimu nafasi hizo kwa muda mrefu sana bilakuthibitishwa hata sasa kinyume cha sheria; kazi za rasilimali watu, Uhasibu namanunuzi kufanywa na Mkurugenzi mkuu isivyopaswa;watu kunyimwa promosheni zao kwa hila na chuki; ofisi za uhasibu zikendeshwa nawatu wasio na sifa; vikao vingi vya bodi kuliko bajeti ya taasisi (Kila kikao35m); fedha za miradi ya wafadhili zikitumika kinyume na miradi wenyewe lichaya kulipa 10% ya fedha za uendeshaji kwa taasisi; kuongezeka kwa kesi ndani yataasisi takriban 20 ambazo ni matokeo ya kutofuata sheria, kanuni na taratibuhivyo kupelekea matumizi makubwa ya taasisi katika kesi; kukua kwa madeni yandani ya wafanyakazi kwa kutokulipwa stahili zao mbalimbali ikiwemo "overtime" ,Posho, likizo n.k.

Na sasa kuharibika kwa mashine ghali (275m) ya kisasakutokana na uzembe wa kutokununua gesi ya 1m tu. Bodi imekataa kuonana nawafanyakazi huku ikitumia fedha lukuki takriban 40m, huku ikishindikana kutoa1m tu ili kuepusha hasara ya takriban 35m ambazo sasa zitahitajika kuitengenezamashine hiyo, kwani sasa itabidi kununua spea na kumleta mtaalamu toka SA kujakuitengeneza. Kinachosikitisha haya yanatokea wakati ambapo wafanyakazi wanajitahidikatika namna mbalimbali kutoa taarifa kwa bodi ya Prof. Pili Kalunde Sibugaambae ameyaweka masikio yake pamba huku wizara ikilipigia upatu fungate hilopasipo ufuatiliaji wowote.

Mh. EngChiza, nidhahiri kwamba Prof. Pili Kalunde sibuga na Mkurugenzi mkuu kwetu sisiTPRI ni kama wajumbe wa kifo (Messengers of death), kwani kwa tathmini hiyohapo juu, hatuoni tutaponea wapi. Imefikia mahali katika kikao cha wafanyakaziwote chini ya chama chao, wameamua kuorodhesha madai yao yoote ili wapatekibali cha kuuza hata nyumba moja wajilipe, kwani kwa mtindo huu chochote nakwa muda wowote kinaweza kutokea (maana kifo au ghafla haina kiume). Kuliachashirika hili life au kuzorota ni usaliti mkubwa kwa taifa japo zaidi ni kwawakulima, lakini hakuna ataekuwa salama, kwani wote tunategemea Bioanuaia,chakula, huduma na matunda ya ekoloji ambavyo vyote vinaathirika vibayapanapokosekana matumizi bora ya viuatilifu. Madhara ya kufa au kuzorota kwataasisi hii ambayo siyo kwako tu, bali nakiri hata mbele za Mamlaka mbalimbaliza juu za nchi hii ni upotofu.

Kutokuwepo kwa mtazamo wa umuhimu wa taasisi hiindiko kunakopelekea kuonekana hapa kuwa mahali pa kuegesha tu na kutozingatiaumakini katika uteuzi wa viongozi wake. Bila taasisi hii Kilimo kwanza, SAGCOT namikakati mingine yote ya kilimo,Uchumi na malengo ya milenia vitazorota kwanidunia imekua kijiji na kila mtu sasa anaogopa madhara ya viuatilfu na taarifazinasambaa kwa haraka na haitachukua muda kabla dunia haijakataa bidhaa zaTanzania kwa uoga wa sumu. Umakini na ustadi wa kulishughulikia hili utaonekanakwa umakini na ustadi wa watendaji ndani ya taasisi hii na wizara yako.Vinginevyo tutaishia kwenye kulaumiana na kazi za zima moto pale wakulima wa Pamba,Kahawa na korosho wanapolalamika tu na kufanya suluhu za kuhairisha tatizobadala ya kutatua tatizo.

Ushauri wetuwa bure, ni Kwamba Mkurugenzi mkuu wako Mrs. E.E. Kimaro ambaye Wizarayakoimejipanga kumlinda kwa udi na uvumba, hafai, hana sifa wala uwezo wakuiongoza taasisis hii nyeti, hata kamati ya bunge POAC (sasa PAC) iliwahikuhoji uteuzi wa mkurugenzi huyu kwani ni ukweli ulio wazi kuwa hakuwa kati yamajina matatu yaliyo penekezwa mbele ya wizara yako, kipindi cha uteuzi wake.
Tunawasilisha

WAFANYAKAZI WA TPRI
 

Daniel Myl

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
536
225
Tangu lini na kwa sheria ipi TPRI ni Agency, TPRI ni kwa mujibu wa PPA act ni kijisehemu cha PHS it has never been an agency
 

Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,648
1,225
1743447_734633933296467_2738211866964166138_n.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom