Kilio dhidi ya Spika Ndugai ni kikubwa kuliko kwa DC Sabaya. Je, siku za Ndugai nazo zinahesabika?

Ndo ujue JF Ina mabata wengi.Anasubiri SSH amtumbue Ndugai.
Ndugai anaweza kutumbuliwa kupitia njia tofauti na zile za kuwatumbua wateuliwa. Ndugai akionekana ana kosa, anaweza kutumbuliwa kupitia vikao vya chama chake, kwa kuwatumia wabunge, japo kwa sasa, hilo inaonekana ni vigumu kutokea.
 
Hujui mihimili inafanya vipi kazi, Spika haingiliwi, bado huelewi, hivi nyie watu akili zenu shule mlisoma wapi? Unamlinganisha level ya Spika na DC? Kweli? Ndio maana Chadema imejaa mazezeta wengi sana, Hivi unamjua Spika vizuri na ni mhimili gani?
Umefoka sana lakini nina hakika akiki yako itakuwa ni kisoda. Spika anaweza kuondolewa japo siyo kwa namna ile ambayo wateule wa Rais huondolewa.

Siyo kweli kuwa hawezi kuondolewa.
 
Ndugai anaweza kutumbuliwa kupitia njia tofauti na zile za kuwatumbua wateuliwa. Ndugai akionekana ana kosa, anaweza kutumbuliwa kupitia vikao vya chama chake, kwa kuwatumia wabunge, japo kwa sasa, hilo inaonekana ni vigumu kutokea.
Sasa kwa taarifa yako chama kinampasuko mkubwa mno, zipo Timu zaidi ya tatu bambazo zote hazipo upande wa mama, usifikiri zile 100%alizo pata kupitishwa uenyekiti niza kweli, Speaker ana timu yake kubwa tu, kina Nape wana ka timu zao, lakini pia Polepole na Bashiri pia Wana timu yao,kwa Rais kumtoa Speaker ningumu sana kuliko unavyo dhani we,
Pia turudi upande mwingine,usifikiri anavyo fanya Rais kuna hata Mbunge mmoja wa ccm anaye Furahia zaidi ya wale waliyo fanyiwa vibaya na Rais aliye pita,Kumbuka hata kina Sabaya niwajumbe wa kamati za CCM,ndipo hapo ninapo enda mbele zaidi 2025 Kama Rais atahitaji kugombea inambidi arudi upinzani ili achukue Fomu maana ndani ya Ccm pekeyake tayari ana upinzani wa kutosha,
Naendapo CCM ita mpitisha mama halafu upinzani wawe na na mtu mwenye Sera nzuri Kama Doctor Slaaa basi ujue upinzani watapita kwa kishindo kikubwa mnno.
 
Hujui mihimili inafanya vipi kazi, Spika haingiliwi, bado huelewi, hivi nyie watu akili zenu shule mlisoma wapi? Unamlinganisha level ya Spika na DC? Kweli? Ndio maana Chadema imejaa mazezeta wengi sana, Hivi unamjua Spika vizuri na ni mhimili gani?
Umepata kichaka unakunyaaa!!
Mbona wabunge wa CCM wanamuomba Rais atunge sheria? CCM kuna maandazi zaidi ya vyama vingine. Ndio maana mwendazake akifanikiwa kuwarubuni wakahamia kwa inzi wa kijani anawapa na position hapohapo sababu sisiemu haina watu weledi.
 
SSH hana akili wala guts za kumsogelea Ndugai, na akijaribu anaweza idodosha serikali yake mwenyewe, hamna mtu yoyote mwenye akili timamu anamuamini SSH, wanaheshimu tu katiba yao amelize muda wake wenye akili timamu wachukue nchi.
 
Kwani spika hadi atenguliwe inapigwa kura au anatumbuliwa tuu kwa amri ya Rais.
Sory mimi sio mwanasiasa wala sheria sikupitia ndio maana nauliza
 
Hujui mihimili inafanya vipi kazi, Spika haingiliwi, bado huelewi, hivi nyie watu akili zenu shule mlisoma wapi? Unamlinganisha level ya Spika na DC? Kweli? Ndio maana Chadema imejaa mazezeta wengi sana, Hivi unamjua Spika vizuri na ni mhimili gani?
Unajua Spika anatoka chama gani cha siasa?
Unamjua Boss wa hicho chama?
Unajua huwezi kuwa spika bila kuwa mbunge pia huwezi kuwa mbunge bila kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa?
Endelea kuwatukana CHADEMA
 
Back
Top Bottom