Kilio cha wengi ni katiba ya Warioba

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
9,491
2,000
Tangu ilipotelewa rasimu ya mabadiliko ya katiba iliyoongozwa na jaji warioba na kufikia kuundwa bunge la kuijadili,rasimu hiyo ilionekana kama ndio suluhisho la wengi na kilio kimepatiwa ufumbuzi lakini ghafla bila kuamini mjadala ule ulivurugwa na watu wasio itakia mema nchi hii wakiwemo waliokuwa wabunge wa maarufu ambao hivi sasa wapo upinzani walisimama kidete kuvuruga mchakato ule kwa kudhani 2015 ni lazima wangepitishwa na chama chao na kugombea urais na kuendelea kutumia katiba ile hatarishi

Baada ya uchaguzi wengi wamerudi na kuidai ile rasimu irudi tena ifanyiwe kazi kwa mategemeo itasaidia hata yule aliyekuwa kinara wa kuikandamiza sasa ameanza kuitamani na kuililia kinafiki kwa kuwa tu nae hivi sasa amekuwa kundi la wenye miguu minne na mikia,

Kilio hiki kimekuwa kikubwa lakini naastajabishwa na hawa jamaa walikuwa ni vinara wa kupinga ufisadi hivi sasa halipo baada ya kununua corruption machine na kuihifadhi ndani ,
sasa wamegeuka kupinga kila kitu hata yale waliokuwa wakiyapigia kelele kama uzalendo,
sasa hapa kwenye hii katiba watu hawa kweli bado wanaaminika si wanaweza kuikana na kuipinga kwa sababu kila walichokipigania ndani ya miaka miwili hii wamekipinga na kukubali kulala selo

Tumshauri rais auendeleze ule mchakato lakini nina hakika pia utapingwa kwa nguvu zote,maana jamaa walifanya kosa kubwa sana la kukumbatia dampo mbele ya nyumba hata likijaribiwa kusafishwa haliachi kubaki na alama chache za uchafu

Ni hakika hiyo katiba inayoliliwa pia itapingwa raisi wape nafasi tuone unafiki wao!
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,473
2,000
tunaitaka katiba ya warioba kama ilivyo bila kutiwa mikono kama mzee sitta(alale anapostahili) alivyofanya umafia..
tunaitaka katiba ya wananchi/ya warioba sababu itatusaidia kuwakamata waliofanya ufisadi ukiwemo ufisadi wa nyumba za serikali.
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
5,933
2,000
Wametafuna fedha chungu nzima Kwenye bunge la Katiba na mwishowe hakuna cha maana kilichofanyika , bora ile hela Yale mabilioni yangetumika kupatia wananchi huduma Za Maji , kujenga vituo vya polisi Kwa kila mtaa, kununua madawa, kuimarisha huduma Za elimu n.k! Yani wote ambao walioanzisha hila ktk kuiharibu ile ktk ya Warioba Mungu atawalipa Kwa wakati wake!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom