Kilio cha wanafunzi hawa kwa umma

The Black

Senior Member
Aug 8, 2013
193
111
KILIO CHETU

*Ujumbe huu uufikie umma.*

Mnamo tar 19/02/2016 Serikali kupitia Tume ya vyuo vikuu (TCU) ili vifungia vyuo vikuu vishiriki vya Mt Joseph tawi la Songea na Arusha wanafunzi hao walihamishiwa katika vyuo vikuu tofauti ikiwemo Chuo kikuu cha Dodoma.

Ni baada ya kuchukua hatua stahiki kufuatilia matatizo yetu yanayotukumba katika ngazi mbalimbali za kiuongozi ili kutatua changamoto zetu lakini mpaka sasa hatuelewi ni nani atakaye tusaidia tunapenda kuujulisha umma kuwa serikali imetutelekeza tunataka umma ulitambue hilo. Sisi ni waalimu wa masomo ya sayansi na hisabati, tusiopungua 203. Ni idadi ambayo ni kubwa Sana na yenye athari katika jamii.

''Tunaukumbusha umma kuwa ni baadhi ya wanafunzi tuliohamishiwa katika Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) hasa tuliokuwa mwaka wa Tatu(3) tukarudishwa mwaka mmoja wa masomo''

Leo hii hatutambuliki Kama tumerudia mwaka..! Na imepelekea hadi sasa tunafanya mafunzo kwa vitendo(field) bila kupewa hela wakati ni haki yetu kupata maana bado ipo ndani ya bajeti yetu ya masomo. " Je serikali ulikuwa mpango wako kutuhamisha kwa nia ya kututesa na kutupotezea ndoto yetu ya kimasomo?"
Hatuamini macho yetu kwa hili linaloendelea.
wenzetu tuliokuwa tunatumia mtaala ule ule serikali inawatambua na wamefanikiwa kumaliza wakati sisi tumekataliwa na kufutiwa matokeo yetu yote na kulazimika kurudia au kusoma miaka miwili ndani ya mmoja tena kwa muda mfupi tena bila pesa zozote ikiwemo ya field tuliyonayo sasa huku wazazi wetu ambao ni wakulima tena wadogo wakiubeba mzigo huu mkubwa, hatujui hatma yetu nini sisi tulioitwa watoto wa kambo. Wazaz wanalazimika kuuza mashamba ili watoto wao wajimudu katka vituo vyao vya masomo ya mafunzo.

Pia imepelekea tukawa na maswali mengi maana hadi sasa hatujui nini hatma yetu kwa sisi wanufaika wa mkopo Kama mkopo wetu upo kwa mwaka wa masomo ujao. kwani hii inadhihilisha kuwa endapo serikali haitawajibika kwa hili jambo kuna hatari ya kutoendelea na masomo kwa mwaka ujao hii ni kutokana na kukosa hela ya kujikimu pamoja na malipo mengine ambayo ni pamoja na ada (fee).

Tumefuatilia Sana Bodi ya mkopo (loan board), Tume ya vyuo vikuu (TCU) na wizara ya Elimu (wizarani) lakini majibu tunayopewa ni kwamba hawatambui kuwa tumerudishwa mwaka hivyo wafuatilie. Mpaka leo hii tumeonekana ni wahanga ambao hatuna pakupatiwa ufafanuzi na ufumbuzi wa tatizo letu,

kwani umma utambue kuwa tangu mwezi wa tisa (9) tarehe12, 2016 tupo vituoni bila hata hela ya kuendeshea haya mafunzo kwa vitendo tunazidi kupaza sauti zetu ili Serikali ilitambue hilo

Tupo katika mazingira magumu tena sana! ombi letu lisikike hata katika vyombo vya habari ili liweze patiwa ufumbuzi haraka na mapema ili kunusuru maendeleo yetu kitaaluma.

TUNAIPENDA SANA TANZANIA YETU
 
Inauma sana kwa hiki kinachofanyika ukizingatia weng wao ni watoto wa wakulima,, wanapoteza dreams zao,, wamepoteza pesa nyng,, af leo serikal inakaa mbal nao, kwel?? Huuu Siyo ubinadam
 
Kwani boom simlipata kama kawaida au?
Kiukweli mwaka wa3 hamuendi field.?
Sasa kama UDOM imewarudsha nyuma waambieni wao ndo wawape pesa field.?
KUMBUKA*
BAJETI YAKO ILISHAPANGWA MIAKA YOTE UKIWA CHUONI.
Either ukiumwa ukahrsha mwaka iyo ni official chuo kitapeleka taarifa loanboard thn utaongezewa mwaka wako wa kupewa mkopo..
OK!!!!?
JE UDOM walipeleka t aariffa kua nyny mnarudia field..?
 
Kwani boom simlipata kama kawaida au?
Kiukweli mwaka wa3 hamuendi field.?
Sasa kama UDOM imewarudsha nyuma waambieni wao ndo wawape pesa field.?
KUMBUKA*
BAJETI YAKO ILISHAPANGWA MIAKA YOTE UKIWA CHUONI.
Either ukiumwa ukahrsha mwaka iyo ni official chuo kitapeleka taarifa loanboard thn utaongezewa mwaka wako wa kupewa mkopo..
OK!!!!?
JE UDOM walipeleka t aariffa kua nyny mnarudia field..?
Sio kwamba tuliishafanya field ila nikwamba tukiwa st.joseph tulikua tunafanya field mwaka wa pili na watatu,hivyo basi sisi tulikua hatujafanya field moja ambayo ilibidi tuimalizie tukiwa UDOM,shida iliyopo ni kuwa hatujawekewa hela ya field kutoka loans board mpaka sasa ikiwa ni wiki ya tano tangu tuanze field
 
Back
Top Bottom