kilio cha wakulima wa korosho nchini Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kilio cha wakulima wa korosho nchini Tanzania.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by janejean, Feb 22, 2012.

 1. j

  janejean Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya kuweka utaratibu wa stakabadhi gharani kwa lengo la kuboresha hali za wakulima hao. Msimu huu umekuwa tofauti sababu hadi kesho wamekaa na stakabadhi zao na hela hawajapata wakati korosho walishakabidhi tangu mwaka uliop wanashindwa hata kupeleka watoto shuleni. Sasa kweli kilimo kwanza ndio hiki!
   
 2. U

  Uwilingiyimana Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo ndugu umenena. Tatizo la nchi hii ni kwamba tumeruhusu siasa zitawale kila kitu. Wananchi wanahangaika vibaya mno. Wamelima kwa shida, na sasa, baada ya kuvuna kwa wingi, wanaishi kwa dhiki na kudhalilika kwelikweli...kidumu chama cha mapinduzi!
   
 3. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Shida ni utaratibu uliopo...

  Mwanzoni, wafanyabiashara wa korosho(hasa Wahindi),walikuwa wananunua wenyewe korosho za mkulima.. Hivyo mfanyabiashara alikuwa anapanga bei anayoitaka mwenyewe,kulingana na kiasi cha tani anazohitaji,na bei walizopanga wafanyabiashara wenzake,na wingi ama upatikanaji wa korosho zenyewe..

  Msimu wa korosho huchukua miezi mitatu hadi minne..Hivyo kupelekea bei kubadilika mara kwa mara.. Wakati mwingine(mara nyingi)mfumo huo huwa na faida kwa mkulima,na mara nyingine huwa faida isipatikane.

  Serikali ikasema itazinunua korosho toka kwa mkulima,kisha yenyewe itazipiga mnada ambapo zitanunuliwa na wafanyabiashara(Wahindi),ambao hao huuza nchi za ughaibuni.. Ilimshawishi mkulima na kwa shingo upande akakubali..

  Mwaka wa uchaguzi (2010),mfumo wa stakabadhi ulifurahisha wakulima wa zao hilo kwani walilipwa advance ya bei iliyotangazwa na serikali,kisha wakalipwa balance ya walichokuwa wanadai,halafu wakapewa "bonus" ..

  2011,imewatumbukia nyongo wakulima.. Wafanyabiashara wanagoma kununua korosho kwenye mnada wa serikali.. Hiyo inapelekea kucheleweshwa kwa malipo wanayodai wakulima wa zao hilo..

  Kisingizio chao(si cha kuaminika),ni kwamba soko la korosho kidunia limeshuka,kutokana na wingi wa korosho zilizozalishwa India.... na Brazil??
  Hivyo wao wakinunua watamuuzia nani?
  Hiyo ni basic concept ya mifumo hii..
   
 4. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,046
  Likes Received: 6,492
  Trophy Points: 280
  Tena hao wakulima wa korosho wengi wao ndiyo waliowapigia kura.
   
Loading...