Kilio cha wafanyakazi wa Impala Hotel na Naura springs chatua kwa Rais Magufuli na TAKUKURU

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Wafanyakazi zaidi ya 100 wakiwemo 22 waliofukuzwa kazi hivi karibuni bila kulipwa stahiki zao katika hotel za Impala na Naura za jijini Arusha,wamemwomba Rais John Magufuli kusikia kilio chao cha muda mrefu baada ya kukosa msaada kwa uongozi wa mkoa kutokana na mkurugenzi wa hotel ya Naura Springs na Impala,Randy Mrema kudaiwa kuwaweka mfukoni

Wakiongea kwa masikitiko baadhi ya wafanyakazi hao waliodai kufanyakazi kwa zaidi ya miaka kumi,wamesema kuwa uongozi wa hotel hizo uliwaandikia barua ya ukomo wa ajira Ifikapo oktoba 31 mwaka huu kwa kile kilichodaiwa ni kampuni kushindwa kujiendesha .

Kutokana na hatua hiyo walipaswa kuandaa malipo yetu ikiwemo mishahara ya miezi minne tunayoidai ,makato ya NSSF na malipo ya kusitisha ajira kuliko walivyofanya kwa.sasa nankusababisha familia zetu kuteseka kwa njaa"

Wakiongea kwa niaba ya wenzao baadhi ya wafanyakazi waliofukuzwa kazi, Grayson Mwanga na Kisuno Bernard wamedai kwamba uongozi wa hotel hizo umeshindwa kuwalipa stahiki zao na wamekuwa wakiwadharau wafanyakazi pindi wanapoulizia malipo ya mishahara yao.

"Hapa tulipo hatujalipwa mishahara ya miezi minne ,makato ya mfuko wa hifadhi nssf ambayo wamekuwa wakikatwa kila mwezi lakini mwajiri wao hapeleki kwenye mfuko huo jambo ambalo tunataka rais Magufuli aingilie kati" Wamesema Mwanga.

Wamemtuhumu mkurugenzi wa Hotel hizo,Randy Mrema kuwa amewaweka mfukoni viongozi wote wa mkoa wa Arusha ,wakiwemo wa idara ya kazi jambo ambalo wamekosa mtu wa kusikiliza kilio chao na hivyo kumtaka rais Magufuli,TAKUKURU idara ya usalama,waziri mwenye dhamana, kuingilia kati kuchunguza jambo hilo.

"Awali Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqaro alitusaidia sana na kuwezesha kulipwa kwa mishahara ya nyuma lakini naye kwa sasa wamejiweka kando na suala letu hali ambayo tumekosa mtu sahihi wa kutusaidia" Alisema Mwanga

Akiongea sakata hilo afisa wa Idara ya kazi Mkoa wa Arusha, Wilfred Mdumi anayedaiwa kuwekwa mfukoni na mkurugenzi wa hotel za Impala na Naura,Randy Mrema amekanusha kurubuniwa kwa kitita cha fedha na kigogo huyo ili apindishe haki ya walalamikaji,ila amesema kuwa suala hilo analishughulikia kwa umakini mkubwa kwa mujibu wa Sheria za kazi.

" Tumefanya mazungumzo na uongozi wa hotel hiyo na kutoa maelekezo lakini kumekuwepo na suala la utovu wa nidhamu kwa wamiliki wa hotel hizo kukiuka makubaliano ya wazi"Amesema Mdumi

"Ofisi yangu imewashauri wafanyakazi hao pamoja na wale walioachishwa kazi kufungua kesi mahakamani kulalamikia kuachishwa kazi bila kupewa stahiki zao ikiwemo kukatwa makato ya mfuko wa hifadhi wa NSSF bila kupelekwa katika mfuko huo"amesema Mdumi

Vyombo Vya Habari waliomtafuta Mkurugenzi wa hotel hizo RANDY MREMA kupata ufafanuzi wa jambo hilo ,mkurugenzi huyo hakutoa ushirikiano badala yake alitimua mbio na kuingia kwenye gari lake la kifahari na kutokomea kusikojulikana na kuwaacha waandishi waliokuwa wamejazana katika hotel ya Impala wakishangaa.

Hotel za Impala na Naura Springs zimeachwa na marehemu Faustine Mrema aliyefariki mwaka 2017 na kukabidhi Mali hizo zisimamiwe na mtoto wake mkubwa aitwaye Joan Mrema lakini baada ya msiba wa marehemu kumalizika dada wa marehemu pamoja na mama yake na Randy walifanya mapinduzi matakatifu(Kupindua Meza) na kujimilikisha hoteli hizo.

Ends...
IMG-20191102-WA0008.jpeg
 
Wachaga kwa kufanya mapinduzi matakatifu hawajambo. Hata kule kwa Msuya wamefanya mapinduzi kama hayo.
 
Makonda alisema kweli mkamuona mbaya mkamkanya kwenye kilio cha mengi.mwenzenu kaona mbali
 
Sakata la Mgogoro wa Impala Group Hotels lachukua hatua nyingine.

Wiki iliyopita wafanyakazi wamegoma tena.


..Nako Ngurdoto Mountain Lodge kumechacha...Msaidizi na Mkurugenzi wameamua kumdhulumu Meneja Mkuu Mafao yao. ndugu Laizer Matassia aliamua kwenda Polisi kufikisha kilio chako. Mkurugenzi wa Ngurdoto alivyoita akasema hamtambui. Ndugu Laizer Mattasia amekuwa Maneja mkuu kwa miaka yote tangu hotel zilipoanzisha na Marehemu Mrema.

Mbali na hilo, yapo mengine mengi ambayo Mkurugenzi anafanya ya kuwadharau na kuwatukana wafanyakazi.Kuwaondoa wafanyakazi kwenye payroll bila taarifa wala barua ya sababu. Kukata watu mishahara kienyeji.
 
Fanyeni kazi waungwana,ya Impala na Naura waachieni wenyewee wayajenge,siku zote mwenye mali akifa kinachobaki ni vurugu mwanzo mwisho,angalieni tangu Mengi amekufa huko kwenye vitegauchumi vyake mambo bado magumu,juzi kwenye misa ya shukrani mkewe mengi Jack hakutokea,jiulizeni kwa nini?,pigeni kazi pigeni kazi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom