Kilio cha Mlalahoi: Kupanda kwa bei ya umeme wanasiasa mko wapi?

Nimeshangazwa sana na ukimwa wa wanasiasa kuhusu kupanda kwa bei ya umeme. Ifike mahali wanasiasa wawajibike kwa wananchi dhidi ya ugumu wa maisha kila kukicha. Kupanda kwa eni ya umeme kutasababisha ugumu wa maisha na mfumko wa bei hivyo kuimarisha umaskini kwa wanachi. Au ni maandalizi ya uchaguzi mwaka 2015 ili kuwahonga kirahisi watu chumvi, kanga na sukari kwa sababu ya ugumu wa maisha?

Wako busy wakifurushana katika vyama vyao.Si unajua tena,Wao kwanza sisi baadaye!
 
Ask not what your Country can do for you ask what you can do for your Country. - John F. Kennedy

mkuu, wananchi kwa sehemu kubwa wanatimiza wajibu wao...tunalipa kodi, rasilimali za nchi zinauzwa, "misaada", mikopo ambayo walipaji wakubwa ni sie....tunataka hao tuliowapa kazi ya usimamizi watimize wajibu wao.
 
nitaanzisha chama changu ambacho kitakuwa hakina ukanda ukabila umimi nitatumia muda mwingi kushugulikia matitizo ya walipa kodi kutatua matatizo yao na si kutumia pesa luzuku kwa kuandaa hekaya feki kama cdm na kijiripua
 
Rubbish!!!! any reason why you made a decision to switch your ID to this one!? Mara KE mara ME shida yote hii ya nini? Khaaaa!!!!

Ask not what your Country can do for you ask what you can do for your Country. - John F. Kennedy
 
Tangu lini aliyeshiba akamjua mwenye njaa!? Kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe, bila Watanzania kuja juu na kuukataa huu mfumo dhalimu wa MACCM hali ya maisha kwa Watanzania walio wengi itazidi kudidimia. Wamethubutu, wameweza na sasa wanasonga mbele.

Gothic rafiki yangu umefilisika kimawazo tanesco na ccm wapi kwa wapi kama hutaki umeme washa kibatari, alafu uone sim utachajia wapi
 
nitaanzisha chama
changu ambacho kitakuwa hakina ukanda ukabila umimi nitatumia muda
mwingi kushugulikia matitizo ya walipa kodi kutatua matatizo yao na si
kutumia pesa luzuku kwa kuandaa hekaya feki kama cdm na
kijiripua

sidhani kama kitafikia hata umaarufu kama wa SAU.
 
Watanzania nasi tumekuwa mno wapole, huvi kwa umoja wetu tukikubaliana wstumiaji wa umeme tukubali kutotumia hiyo nishati kwa wiki moja tu watapata wapi income hao tanesco??? Viwanda wazime umeme wstumie generators na sisi hohehahe tutumie vinatari tuone
Mkuu nimekuwa nawaza kama ww, kwa kuwa wanasiasa wanakula na kusaza hwana wanachopoteza, kazi ni kwa mtz mwenye kipato cha kubabaisha, serikali inajisifu kuwa imewaunganisha umeme wananchi weng zaid mwaka huu lkn wanamtwisha mzigo wa malipo ambapo huyu mwananchi ataishia kutumia umeme kama anachoma sindano coz anawezashindwa kulipa mwisho wa mwenz. Tukiamua wote kwa pamoja kutumia huo umeme wao na kulipa bei mpya watamwuzia nani?
 
kama umewasikiliza vizuri, tanesco inadaiwa bil 400. Hilo ni deni la serikali na taasisi zake mfano vyombo vya ulinzi na kila mwaka wana bajeti ya matumizi ya kawaida. Ni mfumo usiokuwa wa uwajibikaji wizara haziulizwi kama zimelipa madeni. wanajua nini kinachoendelea
 
hahahahaha lol!!!! Weye ndio bado kweli!!!! CCM haihusiki na madudu ya TANESCO!!!!! Weye wa wapi wewe? Ndio umezuka tu jamvini na kujifanya unajua mambo kumbe huna ujuwalo!!! Tulizana kwanza ujifunze kwa kina hapa jamvini badala ya kukurupuka na kuandika madudu.

Gothic rafiki yangu umefilisika kimawazo tanesco na ccm wapi kwa wapi kama hutaki umeme washa kibatari, alafu uone sim utachajia wapi
 
Kasome 'Confessions of an Economic Hitman',ndo utajua hawa "wanasiyasa" wetu wako wapi kwenye hili.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Stabilaiza

Ni kweli mada yako ina mashiko, ila napata shaka EWURA ipo kwa masilahi ya nani?serikali, watumiaji huduma za umeme, maji, nishati na mafuta?

Kimsingi inatia shaka kama ipo kwa masilahi ya wananchi au kama ni kupata posho na mishahara minono kwa kazi ndogo sana za ubabaishaji kama kusingizia wadau wamekutana na EWURA , hivyo kuridhia kupanda bei.Tatizo la kupanda bei ya umeme ni makosa ya wizara kwa kuridhia capacity charges, kuridhia kuendelea kuendesha mtambo wa IPTL, kuridhia kuwa na mikataba ya mitambo ya kutumia mafuta yapata miaka minne sasa, huku bei zao za umeme ni kubwa mno kiasi tanesco haikuwa na uwezo wa kununua umeme huo.

Nakumbuka akina JOHN MNYIKA walipinga kiasi kikubwa bungeni hiyo mitambo kuwa italeta mzigo wa watumiaji ikasemekana ni kwa muda tu.na serikali wakati huo kukopa pesa kwenye vyombo vya fedha kwa riba kubwa kulipia mafuta. Hiyo yote ndo imeleta hii kadhia.Kimsingi hao walioridhia walipashwa kufikishwa mahakamani kulinginza taifa kwenye utata huu na gharama kubwa za umeme ambao umeongeza bei ya umeme. Tatizo nchi yetu watanzania si watu wakuhoji ubabaishaji.

Simbachawene alipohojiwa akasema mtu atakaye shindwa kulipa bei ya kupanda umeme akawashe kibatari , ikuwa kuwa kila namna umeme lazima upande hata kama wadau mtahusishwa kama daganya toto kuridhia, lakini iwe funika kombe serikali ipandishe bei.

Kimsingi kupanda bei ya umeme, ni kupandisha ugumu wa maisha , hivyo tukaze kamba tu, maana mfumko wa bei inakuja sasa hivi.
 
Last edited by a moderator:
Kasome 'Confessions of an Economic Hitman',ndo utajua hawa "wanasiyasa" wetu wako wapi kwenye hili.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Thanks Man umenisaidia sana kujua kinachoendelea juu ya sakata la BEI YA UMEME hapa Nchini kupitia simulizi la 'the CONFESSIONS OF AN ECONOMIC HITMAN' by PERKINS.
 
kupelwa Katika hali halisi,sababu zinazotolewa na wanasiasa wetu kuhusu upandishwaji wa bei ya umeme hazina halali hata chembe.

Ndiyo maana kuna dhana inayosema ukiwa mwanasiasa,ni lazima uwe mwongo.

Nakumbuka JK alipoingia madarakani,kama mkuu wa nchi mwaka 2005,nakumbuka kabisa kuwa miongoni ya comments zake za mwanzo kabisa alitamka kuwa bei ya umeme ya wakati huo ilikuwa kubwa mno,kwa hiyo akawahakikishia waTz kuwa katika awamu ya utawala wake atafanya kila awezalo kuhakikisha umeme huo haupandi tena na ikiwrzakana ushushwe bei.

Alipoingia waziri Muhongo kuongoza wizara ya Nishati,naye aliwahakikishia waTz kuwa ukombozi wa kupanda kwa gharama za umeme ni kupatikana kwa gesi kusini nwa nchi yetu na akawahikishia waTz kuwa bomba la gesi litakapofika Dar na gesi hiyo kutumika kwenye mitambo ya kuzalisha umeme,bei hiyo ya umeme itashukasana

Sasa tunaabiwa kuwa bomba hilo kwa sasa limekaribia sana kufika Dar,lakini tofauti ya ahadi za wanasiasa wetu,hali inayojitokeza ni vice versa,badala ya bei hiyo kushuka badala yake imepanda na siyo tu kuwa imepanda bali imepaa,kwa kupanda kwa asilimia 40!!

Kwa maana hiyo ni vigumu sana kuziamini kauli za wanasiasa,kwa kuwa wengi wao,kauli zao ni za usanii wa hali ya juu!!
 
Last edited by a moderator:
Nimesikia umeme hauta panda kwa kiwango kimoja kwa wote

1. Walio kuwa wanatumia unit 0-50 bei itapanda chini ya 40%
2. Walio kuwa wanatumia unit kati ya 50-75 bei zao zitapungua zitafanana na namba moja hapo juu, kwa kuwa watumiaji wa chini wamepandishwa hadi wanao tumia unit 75 kutoka 50.
3. Walio kuwa wanatumia zaidi ya 75 kwa matumizi ya nyumbani bei itapanda zaidi ya 40%
4. Wenye viwanga bei itapanda zaidi ya 40% kama sijakosea.

Ila namba tatu ndio watakuwa wanalipa bei ya juu kuliko makundi yote.


Anaye jua zaidi anaweza kutusaidia zaidi ...
 
Guys if you wanna know what's on in our Country & why USA and China are both vying for having projects contracts with our Country then read the book called THE CONFESSIONS OF AN ECONOMIC HITMAN once you carefully read this book you will be able to understand why Americans are pushing for the energy projects in Tanzania and why some of the Ministers like Prof Muhongo stand by the foreign investors in the energy sector investment could he be one of those economic hitmen on the USA side?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom