Kilio cha mjane wa Ali Migeyo

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,884
30,228
KILIO CHA MJANE WA ALI MIGEYO
Mohamed Said June 11, 2017 0

Gazeti la Mwananchi la leo Jumapili 11 June, 2017 imechapa makala inayoeleza hali ya umasikini anayoishinayo Janath Migeyo mjane wa Ali Migeyo mmoja wa wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika. Bibi mkubwa huyo anasikitika kwa kusema kuwa ingawa CCM waliahidi kuisaidia familia ya Ali Migeyo ahadi waliyotoa mbele ya kaburi lake siku ya mazishi mwaka 1982, ahadi hiyo haijatekelezwa hadi leo. Lakini ni nani huyu Ali Migeyo? Ali Migeyo kama si kuwa alikuwa kifungoni Jela ya Butimba, Mwanza wakati TANU inaasisiwa Dar es Salaam New Street tarehe 7 Julai 1954, angelihudhuria ule mkutano wa kuasisiwa kwa TANU.

20170611_151807.jpg

Bi. Janath Migeyo mjane wa Ali Migeyo

Hapo chini ndivyo nilivyomueleza Ali Migeyo katika kitabu cha Abdul Sykes:

''Dr. Michael Lugazia akiwa Makao Makuu ya TAA New Street alikuwa anatoka Bukoba, alitaka kuhakikisha kuwa viongozi wa TAA kutoka nyumbani kwao hawapitwi na mkutano ule muhimu wa kuunda TANU. Dr. Lugazia alichukua juhudi za makusudi kupeleka rasimu ya katiba ya TAA kwa tawi la Bukoba. Lakini baada ya kukamatwa kwa Migeyo, TAA ilikuwa imepoteza uhai wake. Hakuna mtu aliyeweza kuwasha tena moto aliouwasha Migeyo. Barua muhimu ya mwaliko iliyoandikiwa TAA Bukoba na Dr. Lugazia ikiambatanisha katiba ya TANU ambayo ilitakiwa kujadiliwa katika mkutano uliokuwa uitishwe Dar es Salaam haikushughulikiwa. Hii ndiyo sababu katika mkutano wa kuasisi TANU mwaka 1954 Bukoba haikuwakilishwa.

Uongozi wa TAA makao makuu uliona kuwa kukamatwa na kushtakiwa kwa Migeyo ilikuwa sawasawa na vitisho dhahiri dhidi yao, ikichukuliwa kuwa wananchi katika mkutano ule walikuwa wamejikusanya kwa amani. Kisa kile kilikuwa salamu za wazi kutoka kwa Gavana Twining kuwa hakuwa tayari kuwaona watu wakihamasishwa dhidi ya serikali. Abdulwahid aliwasiliana na Seaton na kumwomba amtetee Migeyo ambaye alikuwa anashtakiwa Bukoba kwa kosa la jinai. Kamati ya TAA ya Mgogoro wa Ardhi ya Wameru iliyokuwa ikitembelea kanda ya ziwa ilifika Bukoba kujionea hali halisi ya mambo pale Kamachumu. Tarehe 14 Aprili, 1954 Migeyo alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu kwa kufanya mkutano bila ya kibali. Baadaye April 1954, Abdulwahid, Nyerere na Rupia walikwenda Bugandika, nyumbani kwa Migeyo. TANU ilipoundwa tarehe 7 Julai, 1954, Migeyo alikuwa jela ya Butimba, Mwanza akitumikia kifungo. Felix Muganda akitafakari tatizo la Bukoba alimwandikia Nyerere kumfahamisha hali ya mambo ilivyo: ‘’Nimeuita uongozi wote wa Wahaya kuwahamasisha ili wasije wakakata tamaa kutokana na yale yaliyompata Migeyo.’’ Hapo baadaye, uhuru ulipopatikana tutaona jinsi Ali Migeyo alivyoandamwa na serikali ya Nyerere na mwisho kuwekwa kizuizini kwa kile kilichojulikana kama, ‘’kuchanganya dini na siasa.’’

historia
 
Ni miongoni mwa viongozi wanaostahili heshima yakipekee kwa yale walioyafanya dhidi ya Taifa letu.
 
..aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa.

..inasikitisha kuona wakina Mwinyi, Mkapa, na Kikwete, wanajengewa majumba ya mabilioni, wakati nyumba za waasisi wa Tanu zinakaribia kuanguka.

..nilisikitika sana kumuona Mzee Bilali Rehani Waikela akiwa ktk hali ya kusikitisha, toka mahali anapoishi, na hata mavazi yake.
 
Back
Top Bottom