Kilio cha maisha magumu: Je, tulikuwa tunategemea vipato haramu?

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
Kuna kilio cha maisha magumu kila kona. Utasikia wakina mama,wafanyakazi, vijana hata wazee wanadai kipindi hiki cha awamu ya tano pesa imekuwa ngumu sana!.

Ninajiuliza;
1:Serikali inatueleza Inazuia ufisadi, kubana matumizi yasio ya lazima, matokeo yake wananchi wanalia eti maisha yamekuwa magumu maana yake nini?

2:Makusanyo ya Kodi ya kuwahudumia wananchi yameongezeka sana lkn kilio kila kona, tatizo nini?

3:Je Maisha bora mtaani kipindi kilichopita yalikuwa matokeo ya wizi,ufisadi,matumizi mabaya ya pesa za umma na ukwepaji kodi?

4: Nasikia hotel zinakoswa wateja na taasisi nyingi zinazorota kutokana na kubana matumizi kwa serikali. Najiuliza hivi hawa jamaa walianzisha hizo taasisi/kumbi/hotel walikiwa na market strategy ya kutegemea wateja wawe serikali tu au?

5: je, unadhani nini kinakosekana ili kikiwepo Mafisadi waendelee kutumbuliwa,wakwepa kodi walipe, Gharama za maisha zishuke, Serikali iwe na pesa za kutosha, n.k na maisha ya wananchi yawe saaafi kwa matajiri na maskini kihalali? nini kinakosekana.

Najaribu kuwaza....
 
Jiongeze ufahamu kidogo tu walau ujue kitu kinaitwa multiplier effect.

Kukupa mwanga kidogo serikali ikitaka kujenga barabara kuna ajira za wajenzi, madereva, kuna compansation kwa watakaovunjiwa, kuna mama lishe, n.k. sasa leo hii havipo who suffers?

Kuondolewa kwa seminar, warsha etc hizo hela zimepelekwa wapi?

Kuondolewa kwa sherehe mbali mbali za serikali walikua wananufaika ni pamoja na mamalishe, hotel/guesthouse, bar, bodaboda, taxi etc

Pia soma vicious cycle of poverty utapata elimu nzuri hutauliza tena hayo maswali
 
nakupata mkuu mimi ni mfuasi wa SOCRATE, naamini katika philosophy ya "True knowledge exists in knowing that you know nothing"
sijakuelewa maana umetoa maelezo yasiyoshikana kwa mtazamo wangu, nimeuliza nini kimekosekana yaani seminar/sherhe/na matumizi ya anasa yasiwepo na mama ntilie,bar,bodaboda waendelee kufanikiwa by creation of alternative sources. Siamini kuwa hapo ndio mwisho wa kufikiri .
 
Mtoa Uzi unapoint.. Nadhani Watanzania wengi tulikua tunategemea vyanzo vya kipato ambavyo sio rasmi na vilikua vikitegemea disposable income za waliokua kwenye taasisi za umma, ambazo kwa kubaniwa matumizi yasiyo na ulazima ktk kipindi hiki imesababisha mzunguko wa fedha kua mdogo, hii inajumuisha kuwabana wafanya biashara ktk kulipa kodi hivyo kupunguza fedha zao za matumizi ya ziada.
 
Asilimia kubwa ya watu walikuwa madalali.Waandishi wa habari hawakuandika tukio bila bahasha ya kaki,Mishahara hewa,Malipo hewa kwa tenda za magumashi.Kwa ufupi mambo yalikuwa hivyo.
Hapa umenena!
 
Hata kipindi cha semina elekezi, warsha, kulipana posho bado watu walilalamika maisha magumu, ndio wakataka mabadiliko...
.

Hata USA taifa tajiri kuliko yote duniani bado watu wanalalamika maisha magumu ndio maana wanamtaka Trump....

NB. Maisha magumu ni bahari hayana mwisho.
 
Hahaaa, Awamu ya nne watu walizoea kupga sana tukubali. Vilio vya sasa vingi ni kutoka kwa wale waliokiwa wakiamkia, kushinda na kulala kwenye viti virefu.
 
.

Hata USA taifa tajiri kuliko yote duniani bado watu wanalalamika maisha magumu ndio maana wanamtaka Trump....

NB. Maisha magumu ni bahari hayana mwisho.[/QUOTE]
Nazungumzia maisha magumu katikati ya nchi inayosadikika kuwa ni tajiri ya rasilimali ikiongozwa na watu wanaodai wanaweza kudecode hizo rasilimali na kuwapa wananchi unafuu wamaisha.

Ugumu wa america ni tofauti na ugumu wa watanzania japo nakubaliana na wewe kuwa ni bahari.
 
Umeandika kwa mtindo wa kutojiamini na unachokisema vile, hupaswi kuhofu umeandika ukweli, watu walizoea vya kunyonga.
nimefanya makusudi ili kila upande utoe maoni bila kuhisi unashutumiwa. Maana kuna watu humu kama tai wanajiandaa kushambulia kwa nguvu kile wasichokipenda hata kama kina faida kwao
 
Jiongeze ufahamu kidogo tu walau ujue kitu kinaitwa multiplier effect.

Kukupa mwanga kidogo serikali ikitaka kujenga barabara kuna ajira za wajenzi, madereva, kuna compansation kwa watakaovunjiwa, kuna mama lishe, n.k. sasa leo hii havipo who suffers?

Kuondolewa kwa seminar, warsha etc hizo hela zimepelekwa wapi?

Kuondolewa kwa sherehe mbali mbali za serikali walikua wananufaika ni pamoja na mamalishe, hotel/guesthouse, bar, bodaboda, taxi etc

Pia soma vicious cycle of poverty utapata elimu nzuri hutauliza tena hayo maswali

Safi sana mkuu umemjibu kisomi sana huyo mkurupukaji,mawazo yake kubana matumiz basi ni kuzuia ufisadi na wizi,apanue ubongo wake kidogo
 
Safi sana mkuu umemjibu kisomi sana huyo mkurupukaji,mawazo yake kubana matumiz basi ni kuzuia ufisadi na wizi,apanue ubongo wake kidogo
acha dhambi ya ushabiki na ufuasi, toa kilicho katika bongo yako.
ametoa selective answer akisahau sehemu B ya creation.
 
Sipendi kubishana mtu ukitaka kujua utajuatu. upate hela kwa mangumashi kihalali uuza madawa usiuze multiplier effects is the answer to his questions.
 
Ni kweli Watanzania walikuwa wamezoea wizi. Kama ugonjwa wowote ule, itabidi muda mrefu upite hadi wazoee kuishi kwa kipato halali. Ilikuwa hivi Rwanda wakati wa Habyarimana, ingawaje hata huko kidogo kulikuwa na nidhamu. Tanzania ilikuwa inaelekea kwenye Jahanum ya kijamii.
Siku zote nilikuwa nashangazwa nilipokuwa naja Tanzania! Utamkuta mtu hohehahe lakini anazungumzia kwa mahesabu ya mamilioni! Hata siye wa nje hatuzipati hizo. Hii ilikuwa kama 'kawaida' ya maisha, na kila mtu alikuwa anaota kuwa anaweza kupata milioni 'wakati wowote' hata bila ya mipango, kazi au usumbufu (kwa vile anawaona walio madarakani).
Katika mambo yote ninayomlaumu JK hakuna kama hili la kuwafanya Watanzania waishi katika ulimwengu wa ndoto ambapo wizi, ufisadi, ufujaji na ukosefu wa uzalendo- vilikuwa vitu vya kawaida na vilivyovumiliwa. Yeye mwenyewe alikuwa naishi katika ndoto ya kudhani ni rais 'muhimu' sana duniani na kwamba amefanya 'mengi' ya maana, na kwamba Tanzania imekwisha endelea!
 
Back
Top Bottom