Kilio cha Katiba Mpya kiende sambamba na uzoefu wa Bunge Maalum

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Kelele za wanajamii kutaka katiba mpya, kimeanza kusikika kwa nguvu. Maaskofu na waandishi wa habari ni sehemu tu ya wanaopaza sauti wakitaka nchi iwe na msingi mzuri wa katiba mpya.

Mheshimiwa rais akiongea na waandishi wa habari miezi kadhaa iliyopita, alisema kwa sasa anainyoosha nchi kwanza, kabla ya kutoa kipaumbele kwenye shughuli za michakato ya uandaaji wa katiba mpya.

Uzoefu wa bunge la maalum la katiba mpya nyakati za mheshimiwa Jakaya Kikwete, sio mzuri sana kwa watu makini wenye kutambua maana ya muda ni mali (time is money).

Yaliibuka malumbano mengi ndani ya bunge lile, zikasemwa kauli mbaya na zisizofaa kusikika masikioni mwa watoto wadogo. Watu wazima wakabishana pasipo kuwa na chembe ya kujitambua.

Mwisho watu wakasikia maneno kama interahamwe, na wengine wakasusa na kutoka nje. Mambo ambayo kwa mwenye hekima, hayatoi mwanga mzuri wa mustakabali wa nchi kuwa na katiba bora.

Leo hii ukiandaliwa mkutano mwingine wa katiba, kutaibuka sintofahamu kama zile zile za wakati wa mzee Jakaya Kikwete. Kutakuwa na upotezaji wa muda, kwenye malumbano na matusi mengi, yanayotoka kwenye pande zenye mitazamo tofauti ya kisiasa.

Wapendwa tukumbuke kwamba tunaposema tunataka kujenga reli ya standard gauge wenzetu Kenya na Ethiopia tayari wanayo reli ya ubora huo.

Tunapozungumzia mipango ya kuhakikisha kila kijiji kinafikiwa na umeme, wapo majirani zetu ambao wameshayafanya haya tena miaka kadhaa iliyopita.

Kuna suala la kujipanga ili mamlaka kama ile ya anga iweze kufanikisha uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere unakuwa ni njia panda (hub), hatuwezi kufanikisha mpango huo kama bado tunarudi kule kule kwenye mipasho ya bunge maalum la katiba lililopita!.

Watu wanataka waache kumbukizi kwenye medani za kisiasa lakini Afrika inayotuzunguka haina muda wa kutusubiri eti tuweke kwanza suala la katiba vizuri ndipo tuingie kwenye michakato ya kiuchumi.

Uzoefu wa bunge maalum la katiba lililopita wakati wa JK, sio mzuri. Wajumbe wa bunge lile hawakuangalia gharama za wao kuwa mle ndani ya jengo, na wakaona ni haki yao ya msingi kupoteza muda kwenye malumbano na majibishano yasiyo na faida kwa mwananchi wa kawaida.

Je, tunao ushahidi gani wa mabadiliko ya kihulka na kimtazamo miongoni mwa wadau muhimu watakaokuwemo kwenye mchakato wa kupata katiba tuitakayo?.

Siasa za lawama, kejeli, kunyoosheana vidole, hazijawa na msaada wa kuipeleka mbele Tanzania hata kwa hatua moja ya kimaendeleo. Tunajipanga vipi kuwa sehemu ya Afrika yenye maendeleo na wakati huo huo kilio cha wenye kutaka katiba mpya kikafanyiwa kazi?.

Tukumbuke kuwa uwepo wa katiba mpya na yenye kuridhiwa na wengi ni sehemu tu ya mapambano ya kuuinua uchumi wa nchi. Hapo kwenye balance kati ya siasa na uchumi ndipo mahali muhimu sana kwa sasa.
 
Kama majembe walikua kina mpolepole, kina jaji wakiloba ambaye mwanaye kapewa uDCC, nasasa washalambishwa sukari, unafikiri kuna nini tena
 
Hayo malumbano yalianzia kwenye bunge la katiba baada ya kujaza wanasiasa wengi na kumgeuza rais kuwa msimamizi wa mchakato. Lakini tume ya kukusanya maoni ilitekeleza wajibu wake bila hila. Sasa hivi iwapo mchakato ule utarejea na kumruhusu rais kuwa juu ya mchakato ndio tutashuhudia katiba ya ajabu kupita kiasi.
 
Unafikiri katiba mpya ndio muarubaini wa matatizo yetu mkuu?
 
Hayo malumbano yalianzia kwenye bunge la katiba baada ya kujaza wanasiasa wengi na kumgeuza rais kuwa msimamizi wa mchakato. Lakini tume ya kukusanya maoni ilitekeleza wajibu wake bila hila. Sasa hivi iwapo mchakato ule utarejea na kumruhusu rais kuwa juu ya mchakato ndio tutashuhudia katiba ya ajabu kupita kiasi.
Mkuu walikuwepo wawakilishi wa vyama vingi vya kijamii. Sintofahamu ilikolezwa wakati wa mjadala wa serikali mbili au tatu.

Yakaibuka maneno kwamba asilimia kubwa ya wawakilishi wa taasisi ni watu wa system ndio maana maoni ya CCM yanakuwa na ushawishi mkubwa, hali kama hiyo haiwezi kukwepeka hata leo hii kama mchakato wa katiba utaanza tena.
 
Unafikiri katiba mpya ndio muarubaini wa matatizo yetu mkuu?
Mkuu wapo wenye mawazo hayo, na wanakuwa nayo pengine kwa sababu ya kuangalia siasa za Kenya, na baadhi ya udhaifu unaoibuka wakati wa kushughulikia matatizo ya madini.

Wanachoshindwa kutambua ni kwamba ukipata utatuzi wa suala moja kunaibuka matatizo mengine wakati tayari katiba ishapitishwa tena kwa gharama kubwa.
 
Lissu pona haraka uje kuwaambia watupe katiba mpya cose ukipaza sauti yako inawachachafya,
 
Mkuu walikuwepo wawakilishi wa vyama vingi vya kijamii. Sintofahamu ilikolezwa wakati wa mjadala wa serikali mbili au tatu.

Yakaibuka maneno kwamba asilimia kubwa ya wawakilishi wa taasisi ni watu wa system ndio maana maoni ya CCM yanakuwa na ushawishi mkubwa, hali kama hiyo haiwezi kukwepeka hata leo hii kama mchakato wa katiba utaanza tena.

Lile bunge halikuwa na tofauti na bunge hili la JMT la sasa kwani wingi ulibaki kwa wabunge wa ccm. Tofauti ya bunge lile na hili ni maudhui tu ila sio mwenendo. Nadhani uliona tume ya Warioba ilivyofanya kazi, ile watu walivua uvyama wakaweka taifa mbele. Lakini likija sasa kwa muundo ule utaona taifa litawekwa nyuma na uzalendo wa rais ndio itakuwa kichaka cha kupitishia katiba ya mtu. Sasa hivi kuna woga, unafiki na kujipendekeza kwa ajabu.
 
Back
Top Bottom