Kilinge kilipata shambulio... nikaunganisha na likizo

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,552
Nawasalimu katika Kristo Yesu aliye hai.

Na kwa wale ambao si wa imani hii nawasalimu katika imani zao... Lililo kubwa ni upendo kujali na tafakuri

Nilipotea barazani kwetu hapa, kuna coincidence ilitokea
Mipango ilikuwa nichukue likizo baada ya kipindi cha kampeni na uchaguzi kwisha, maana kwa hakika kwa upande wetu tulikuwa busy na tulijitoa kwa hali na mali kuhakikisha tunakuwa na mtazamo mpya...!!!!

Usiku wa kuamkia October 29 kilinge kikapata shambulio kubwa la kimwili hardware yote ikateketea kwisha kabisa lakini software ikasalimika kwa asilimia 100

Kipindi cha kampeni nikapata marafiki nyoka wanafiki wengi sana waliodhani wanamfahamu Jr kuliko wanavyojifahamu wenyewe.

Waliojifanya wana mapenzi mema nami kuliko familia zao na michepuko yao, waliojifanya ni washauri wema sana kuliko wale wanaowatumikia kule walikotumwa.

Wachumia tumbo hawa...MUNGU AWAREHEMU SANA..Kuna siku kutapambuzuka hata usiku uwe mrefu kiasi gani....!!!

Nimerejea JF tena ...nilikuwa likizo ...Familia yetu ya JF nje ya JF tulikuwa na mawasiliano ya karibu na tukapashana yanayotokea duniani kila sekunde

Haters na wanafique wako popote TUNAWAHITAJI KAMA KIOO CHETU...Lakini kwa bahati mbaya sana..wanaishi dunia ya miji bila majumba ...barabara bila magari....misitu bila watu...

Wanajaribu sana kutuonesha wafu wakati makaburi tunajua yalipo na wanatuonesha vitabu wakati kurasa tunazifunua sisi....!!!

Mwenda tozi na omo.....!?

NIMEREJEA...!!!
 
Lile chawi la machawi, wanga la wanga limerudi..🤣😅

Wewe umekuja kuharibu tu.
 
Karibu tena mkuu Mshana Jr pole kwa yote, na nakutakia yote mema.

Hivi hio familia ya Jf nje ya Jf ni kwa ajili ya Kila mwana Jf ama ni maalum tu?
 
Back
Top Bottom