Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Mimi nawashauri vijana wasijidanganye kwenda shambani ni bora wabaki mjini wakiwa wanabeti kuliko kufuata hizi porojo za huku mitandaoni. Hivi kilimo kingekuwa kinalipa leo tungewaona wakulima wakiwa wamechoka kiwango kile? Mbona hata hao mabwana shamba wenyewe hawawekezi kwenye kilimo? Kuliko kwenda kulima ni bora uajiriwe kazi ya ulinzi huko kwa wahindi. Ukitaka kuwa masikini nchi hii danganywa ukalime.
Moja ya fikra pumba nilizowahi kushuhudia hii.
 
Mie huwa naona fahari sana mtu akiongea ukweli lakini sio kuja kuongea ujinga ujinga eti "msikimbilie ajira fanyeni kilimo" nadhani labda huwa mnaongelea kilimo cha bangi hicho ndio kinalipa fasta.

Semeni ukweli tu kilimo hata nchi zilizoendelea kinafanywa na matajiri na wala sio watu wa kawaida, unapoongelea kilimo ukasema unalima eka 3 hiyo ni bustani sio kilimo. Mimi ninalima na ninajua kilimo lakini husijekusema kijana unakomalia ajira kwa nini, wengine mara oooh hauna pesa unamilikije iphone x au samsung s8 sidhani kama hiyo inahusiana....

Unapoongelea kilimo kuna vitu hivi la, ima uviweke kichwani na vitahitaji fedha

1. Ardhi
2. Mbilea
3. Maji
4. Usimamizi
5. Mafanyakazi
6. Matunzo
7. Mbegu
8. Madawa
9. Uvunaji
10.uhifadhi wa mazao
11.ushindani wa bei sokoni
12.kuoza au kuharibika

Hiyo ni kwa kilimo cha kizamani, hapo ukisema ulime kisasa kuna kuweka drip irrigation system kwa eka 1 tu unatumia zaidi ya 1,450,000/= haya fanya unalima ekari 5 utatumia bei gani...!!!!

Mie nadhani ni vema tusikichukulie poa kilimo, na tusifananishe kilimo na bustani....atanzania wakulima ni wachache ndio maana masikini wengi wanapatikana huko.

Masoko yenyewe miyeyusho unalima nyanya unakuta bei ni 2000 kwa kile kindoo cha lita 5 si mtu utakufa na mawazo....

Unapokuja kusema uongo eti umewekeza 500,000 baada ya miezi minne ukavuna mahindi ya 3,000,000/= huu ni uwongo mweupeeee pee......ukiambiwa leta cost zote sidhani kama utaweza zaidi ya kujiuma uma.
Mbona inawezekana brother? Acha kudhani haiwezekani kisa haijakutokea wewe.Ekari moja ya mahindi inaweza kutoa hata gunia 30 na zaidi za kg 100 zikilimwa kitaalamu sasa akikuta bei ya kilo moja sokoni ni Tsh 1000 hiyo si ni milion tatu kamili?

Afu gharama ya kulima watu wamekariri ohh hela ya kukodi ardhi wakidhani kila mtu analima kwa kukodi kumbe kuna watu wanalima mashamba ya wazazi wao au ya watu waliowapatia tu walime mfano mzuri ni mimi mwenyewe nalima zaidi ya ekari 7 na hakuna hata moja niliyoikodi sasa ondoa gharama ya kukodi weka hivi

Kulima ekari 1 Tsh 80,000
Mbegu 60,000
Kupanda 50,000
Kupalilia 100,000
Mbolea DAP 60,000+Urea 54000+CAN 43,000
Mifuko 15,000
Kuvuna avune mwenyewe
Kusafirisha atumie mkokoteni au punda

Jumla Tsh 462,000#

Hata hapo nimepiga cost za juu kwenye mbolea maana kuna mashamba mengine hata mbolea ya dukani hayahitaji kutokana na rutuba yake murua kabisa

Kuna watu wananunua mbegu tu na mifuko tu , kulima wanalima wenyewe kupalilia wanapalilia wenyewe ,kuvuna wenyewe na wanavuna good tu wakipata bei poa wanapiga pesa nzuri tu.

Lakini pia unaposema kilimo hakilipi eti kinalipa kwa matajiri kwani hao matajiri walizaliwa matajiri? Kupata kunazidiana ndiyo maana kuna wakulima wana mtaji wa kilimo bilion 2 wengine laki 2 na kila mtu anapata faida kwa viwango vyake , nikiweka laki 2 nikapata laki 5 au 6 faida hapo laki 4 sasa utasemaje hakuna faida? Kikubwa kumaintain juhudi na kutafuta namna ya kutatua changamoto zinazokukabili kama mkulima utafanikiwa tu.

Hata mimi niliota kulima ekari 1 ila nikafanikiwa leo hii ukiniambia nilime ekari moja naona unanitania leo nipo ekari 7 japo sijafika ekari 10 but mwaka huu namwomba Mungu nifike 10 na zaidi malengo ni siku moja nilime ekari 100 hata na zaidi na nitafanikiwa nisipokata tamaa
 
Kila ekari mbili nimepata gunia 37, nikauza gunia 35×@90,000/=.
Gharama za kulima
Mbolea mifuko 2 @61,000/=
Mahindi kg 20=100000/=
Palizi =140000 ya kwanza na pili
Kupukuchua gunia moja ni shilingi 1500×37=52500
Gharama ya kupanda nilitumia 20000 na nguvu kazi ya nyumbani.
Upo mkoa gani..? kwa hekar mbili hizo gunia ni possible, mi mwenyewe nafanya kilimo cha mahindi ila bei zinatuangusha masalani kwa sasa gunia linauzwa 40k
 
Mbona inawezekana brother? Acha kudhani haiwezekani kisa haijakutokea wewe.Ekari moja ya mahindi inaweza kutoa hata gunia 30 na zaidi za kg 100 zikilimwa kitaalamu sasa akikuta bei ya kilo moja sokoni ni Tsh 1000 hiyo si ni milion tatu kamili?

Afu gharama ya kulima watu wamekariri ohh hela ya kukodi ardhi wakidhani kila mtu analima kwa kukodi kumbe kuna watu wanalima mashamba ya wazazi wao au ya watu waliowapatia tu walime mfano mzuri ni mimi mwenyewe nalima zaidi ya ekari 7 na hakuna hata moja niliyoikodi sasa ondoa gharama ya kukodi weka hivi

Kulima ekari 1 Tsh 80,000
Mbegu 60,000
Kupanda 50,000
Kupalilia 100,000
Mbolea DAP 60,000+Urea 54000+CAN 43,000
Mifuko 15,000
Kuvuna avune mwenyewe
Kusafirisha atumie mkokoteni au punda

Jumla Tsh 462,000#

Hata hapo nimepiga cost za juu kwenye mbolea maana kuna mashamba mengine hata mbolea ya dukani hayahitaji kutokana na rutuba yake murua kabisa

Kuna watu wananunua mbegu tu na mifuko tu , kulima wanalima wenyewe kupalilia wanapalilia wenyewe ,kuvuna wenyewe na wanavuna good tu wakipata bei poa wanapiga pesa nzuri tu.

Lakini pia unaposema kilimo hakilipi eti kinalipa kwa matajiri kwani hao matajiri walizaliwa matajiri? Kupata kunazidiana ndiyo maana kuna wakulima wana mtaji wa kilimo bilion 2 wengine laki 2 na kila mtu anapata faida kwa viwango vyake , nikiweka laki 2 nikapata laki 5 au 6 faida hapo laki 4 sasa utasemaje hakuna faida? Kikubwa kumaintain juhudi na kutafuta namna ya kutatua changamoto zinazokukabili kama mkulima utafanikiwa tu.

Hata mimi niliota kulima ekari 1 ila nikafanikiwa leo hii ukiniambia nilime ekari moja naona unanitania leo nipo ekari 7 japo sijafika ekari 10 but mwaka huu namwomba Mungu nifike 10 na zaidi malengo ni siku moja nilime ekari 100 hata na zaidi na nitafanikiwa nisipokata tamaa
Nakuunga mkono mimi nalima takribani ekari 20 ila huku niliko rutuba ipo vizur Dap haihitajiki na tunavuna wastani wa gunia 10-25 kwa hekari,huku mvua sio changamoto hata kidogo shida kubwa ni network ya masoko ndo inatutesa sana,huwezi jana tu nimetoka kuuza gunia 25/1000k kwa ajili ya dogo shule utaona jinsi bei zinavotufelisha.
 
Mimi nawashauri vijana wasijidanganye kwenda shambani ni bora wabaki mjini wakiwa wanabeti kuliko kufuata hizi porojo za huku mitandaoni. Hivi kilimo kingekuwa kinalipa leo tungewaona wakulima wakiwa wamechoka kiwango kile? Mbona hata hao mabwana shamba wenyewe hawawekezi kwenye kilimo? Kuliko kwenda kulima ni bora uajiriwe kazi ya ulinzi huko kwa wahindi. Ukitaka kuwa masikini nchi hii danganywa ukalime.
unawaponza watu mzee baba
 
Kuna watu wapo busy kuhangaika kutafuta ajira serikalini na mashirika binafsi, wengi hufikiri kuwa wanaweza kutoka kwa kuajiriwa, vijana wengi wanaogopa kujihusisha na kilimo aidha wanafikiri kuwa kilimo hakilipi na wajanja waliopo huko hawawambii wenzao kuwa kilimo kinalipa.

Nitoe ushuhuda kidogo mwezi wa 9 mwaka jana nimelima ekari mbili gharama haikuzidi laki 5 lakini nimeuza mahindi hayo zaidi ya milioni 3. Na bado mengine nikaacha kwa ajili ya chakula, hebu fikiria sasa ni biashara gani ya laki tano ambayo unaweza ifanya kwa mtaji wa laki tano ukapata mil 3 kwa muda wa miezi 4 kwa kifupi haipo.

Mishahara mingi ya waajiriwa wenye shahada ni 450,000/=(kwa wale wenye mikopo) na 560,000/= kama huna mkopo, sasa tufanye hesabu fupi tuchukulie uhalisia kwamba vijana wengi wamesoma kwa mkopo, 450,000 ukilipia nyumba, umeme, maji na matumizi mengineyo unajikuta haifiki tarehe kumi tano unaanza kukopa tena, lakini ukichukua 450,000×12 =5,400,000/= kwa mwaka mzima, hii pesa kwa mkulima ni msimu mmoja tena huyo ni mkulima mdogo kabisa na kwa mwaka kuna misimu miwili.

Ushauri wangu kwa vijana tujaribu kuwekeza kwenye faida yake ni kubwa lakini pia kilimo ni mradi endelevu, idadi ya watu inazidi kuongezeka hivyo mahitaji ya chakula ni mengi kuliko idadi ya watu.
Mkuu popote ulipo kunywa kahawa na kashata ntalipa. Au kwa kuwa upo Tarime kula nyama kwa kichuri bill ni yangu.

Umeleta hoja ya maana sana kwetu sisi vijana tunaohangaika kutwa kucha kutafuta kazi za laki 4 kwa mwezi. Ukizoea hizo project za kilimo ndogo ndogo zinakupa mahitaji karibu yote muhimu.
Binafsi nadeal na mahindi na mpunga. So nasupport hoja yako from real experience na currently nalipa hadi ada ya chuo kwa kilimo.
Ila kama hutojali naomba unisaidie namna ya kupata hiyo mbegu ya DK niijaribu coz me nmekua nikiitumia seedco.
 
Unalima wapi mkuu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom