Kilimo kwanza, watanzania kuwa manamba, vibarua na watumwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo kwanza, watanzania kuwa manamba, vibarua na watumwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPadmire, Dec 25, 2011.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Jinsi Kilimo kwanza inavyochukuliwa maana yake ni kuwa Wawekezaji kupewa ardhi kubwa, walime halafu faida yote wapeleke nchini kwao!!!

  Watanzania wapewe fursa walime, wakopeshwe na faida itabaki Tanzania na uchumi wa Tanzania utaimarika. Acheni kutegemea wawekezaji, ni ukoloni mamboleo
  na mwishoni mtaambiwa muwe mashoga


  Hao wawekezaji wanapewa ardhi, watanzania tutakuwa wafanyakazi, vibarua na watumwa kwa mshahara kiduchu - Cheap labor. Hivyo hao wawekezaji watatengeneza faida kubwa.

  Tayari kuna wakorea wamepewa maelfu ya hekari. Pia tumeona au tumesikia KUle Katavi Mh Pinda ameita wawekezaji.
  Pia tumesikia mbarali wananchi walinyang'anywa ardhi pia kule bonde la Kivu Manyara kuna mgogoro.

  Nashangaa hii tanzania haina wachumi au haina vijana waliosomea Kilimo???

  Kwa mfano, Serikali ikipima ardhi yote inayofaa kwa kilimo, halafu ikatangaza na kuwaaalika watanzania, hasa vijana wanaomaliza shule na vyuo. Wale watanzania watagaiwa kuanzia eka 5, 10, 20, 50 Basi. Kwanza serikali itapata kodi ya ardhi ya mwaka, pia itakuwa imetatua tatizo la ajira kwa vijana, Taifa kuwa na akiba ya chakula, export ya mazao hivyo serikali kupata foreign exchange, na shilling kuimarika, kudhibiti mfumuko wa bei na uchumi wa nchi kukua.

  Wako wapi Akina Mustafa Mkulu, JUmanne magembe, NChimbi, Anna Tibaijuka, MAry nagu, na mkubwa wao Pinda????

  Someni hapa.


  Acheni kufikiri jinsi ya kupambana na upinzani ili kubakia madarani.

  Jinsi ya kubakia madarakani ni kutoa huduma kwa wananchi, na kuacha ufisadi tuu.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  tatizo ni kuwa badala ya kufikiria kuwakopesha wakulima wenyeji, viongozi wetu wanafikiria jinsi ya kuzifisadi fedha za kilimo. Zile fedha za EPA ilisemwqa kuwa zipelekwe TIB kwa ajili ta kufungulia agricultural window itakayokopesha wakulima wwenyeji. lakini ukiulizia ni wakulima wenyeji wangapi wamepata hizo fedha sidhani kama kuna atakayekupatia jibu la uhakika na fedha zimeisha.
   
 3. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Kulingana na Taarifa zilizopo kwenye JF na pia kwenye baadhi ya magazeti zile hela za EPA ziliyeyuka kiaina. Inasemekana zilichakachuliwa kwa ajili ya kufanikisha ushindi wa magamba.

  Cha maana hapa ni vijana kujiunga na kupambana. Kuanzisha harakati za kudai ardhi ya kuwekeza. Ukiwa na ardhi mkopo benki ni rahisi. Vijana mpoo? au mnasubiri kuajiriwa na wawekezaji ?
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kikwete ni Agricultural economist. That should tell you something.
   
 5. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Tupomkuu,ila wazee pia hawako salama maana wanaweza kukosa hta nafasi ya kuzikwa!
   
Loading...