Kilimo kwanza sera sahihi ya ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo kwanza sera sahihi ya ccm

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CCMTHINKER, Nov 23, 2010.

 1. C

  CCMTHINKER New Member

  #1
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kilimo kwanza ilikuwa ni sera namba moja ya wachumi wa kikoloni. Walipofika walianza na kilimo kwanza kabla ya elimu .Wakaleta mazao kama mahindi,maharage,mpunga,chai,kahawa,pamba,karafuu nk mazao ambayo hayakuwepo Tanzania.watanzania .Mazao hayo yalipoletwa na wachumi wa kikoloni yalikomboa watanzania walio wengi nchi nzima kichakula na kiuchumi toka miaka hiyo hadi leo hii .Hebu tuwapigie makofi wachumi wa kikoloni kwa kuwa na mipango thabiti endelevu ya kiuchumi ya kusaidia watu wa chini kwa miaka mingi tofauti na wachumi koko wa leo ambao kazi yao ni kukusanya takwimu zisizo na kichwa wala miguu zisizomsaidia mtanzania kutoka kwenye ulofa zaidi ya kuzirundika kwenye maktaba na kongamano za kujadili tafiti maruhuni ambazo wanajua undani wa tafiti hizo ni hao walioziandika wenyewe na wachumi koko wenzao.CCM inajua kilimo kwanza ndio jibu la miaka mingi ya kuondoa umaskini kwani hata wasomi wakistaafu wengi waweza ishi kwa kilimo na ufugaji.
  CCM iliunda sera hii ya kilimo kwanza kwani inajua kuwa Mikopo mingi ya mabenki ya dunia inalipiwa na pesa za kigeni zitokanazo na mauzo ya mazao ya wakulima kama wa chai,kahawa,pamba korosho n.k ambayo ndio uti mkuu wa mgongo wa pesa za kigeni.Hazilipwi kutoka kwa wapiga porojo ZA KISIASA WALIOKO MIJINI NA WASOMI BLABLA wenye majina makubwa lakini wazalishao maneno matupu yasiyobadili hali duni ya mtanzania na watanzania walio wengi.Wala mikopo hiyo hailipwi na na wapiga filimbi wa hamelini waishio mijini wakifanya biashara za maandazi,kuzurura na vilaptop mabegani na umachinga wa kuuza bidhaa za nje vikiwemo vinywaji vya nje na kucheza disco kama pale billicanas Dar es salaam.Baada ya kujua kuwa wakulima ndio wachangiaji wakubwa wa fedha za kigeni na kupitia wao mikopo ya mabarabara nk hulipwa kutokana na jasho lao ikaonelea Kilimo kwanza kipewe kipaumbele.
  CCM baada ya kuona kuwa ili ifanye vizuri ihangaike na walio wengi ambao wako vijijini kwa sera ya kilimo kwanza.Na ndio siri ya CCM kushinda vijijini.Ni sera sahihi sana ya kukomboa walio wengi ambao ni asilimia themanini ya watanzania.Tofauti na sera za vyama vingine ambavyo ukiondoa suala la ufisadi kwenye agenda zao hata huwezi jua sera zao ni nini .wanabaki weupe hawana cha kuwaambia watanzania walio wengi watawatoaje kwenye umaskini.Hawana sera elekezi.Kukosoa tu si sera lazima uwe na kitu concrete cha namna gani utamtoa mtanzania kutoka kwenye umaskini.
  Hongera Rais na Waziri Mkuu kwa sera ya kilimo kwanza inayoweza kukombo walio wengi kiuchumi ambao ni asilimia themanini ya watanzania.Hao asilimia Ishirini wa Mijini wasiwanyime usingizi wamewekewa barabara za lami,umeme,nk na bado wanawanyima kura waacheni na blabla zao. hangakeni zaidi na wa vijijini sasa hivi kama ni rasllimali kwekezwa mijini imetosha boresheni maisha vijijini kupitia sera ya kilimo kwanza.nguvu kubwa za raslimali zielekezwe huko watu wa vijijini sasa iwe zamu ya watu wa vijijini wa mjini inatosha.
  ccmjuu@gmail.com
   
 2. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  crap from crapville .... through crap o molder
   
 3. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Unapojipa kazi ya kupiga propaganda, jiandae.

  ...Hamna nchi iliyoendelea kwa kudharau wasomi na wakaazi wa mijini.
   
 4. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  CCMTHINKER jipange kwanza Kilimo kwanza si sera.
   
 5. C

  Chagula Member

  #5
  Nov 24, 2010
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali ya Mwinyi ilipotangaza OPEN MARKERT, watanzania walidhani basi huu ndio wakati wa kula vya umma na kuiba serikalini. matokeo yake, kilimo cha pamba huko mikoani kikafa, wachaga wakafyeka mikahawa yote na wakaanza kulima majani ya kulisha ng'ombe wa maziwa, viongozi wa serikali waliokaa Oysterbay wakaanza kufuga n'gombe wa maziwa na kuku. Sasa hepu tujiulize, nchi ina wakulima asilimia 80, na wafanyakazi na wazururaji asilimia 20. kama wafanyakazi wanaanza kulima na kufuga, sasa mkulima wa huko Busweru atalima nini? Coop za pamba zilikufa, migodi ya madini sasa ni ya viongozi wa CCM siyo ya taifa, korosho, katani, kahawa, karanga, ngano na hata mahindi, hayana mpangilio wa kuwainua wakulima, badala yake viongozi wananunua ardhi kwa ajili ya familia zao. Je haya ndiyo maendeleo kweli? Nchi imekufwa, imeuawa na uongozi mbovu wa CCM ya sasa. benki haina hela zote walichukua wakamegeana na kufanyia biashatra zao na wake zao. Hela za kulipa nchi za kigeni (EPA), hazipo na kama zipo zitalipia nini wakati wananchi wameacha kilimo cha uchumi, siku hizi kilimo kikuu ni cha mchicha, pilipili na kabichi ili wale. Hakuna nchi yeyote duniani ambayo inapanga bajeti yake ya taifa kwa kutegemea pesa za misaada eti kutoka kwa WAFADHILI. Tanganyika na Zanzibar ni nchi huru TANZANIA, kwa nini isijitegemee kama Botswana, tunakaa na viongozi walaji tu eti wafadhili watatupa misaada na waarabu watakuja wawekeshe? tangu lini mtu atoke Libanoni aje Shinyanga na kuchukua Almasi yetu na sisi tunakaa tu na kuendelea na umaskini wetu? tabgu lini mtu aje toka Ghana na kuchimba dhahabu yetu na sisi tunapata asilimia 2tu na kutegemea tutaendelea badala ya kuwapa utalaamu wa kuchimba madini vijana wetu wenyewe? ni lini Tanzania itajitegemea, sasa karibu miaka 50 tangu tupate UHURU na bado tumo kwenye orodha ya TOP TEN MASKINI DINIANI. CCM aibu hii. namuomba JF aliangalie sana hili suala la uchumi wa taifa na aacha kuchagua viongozi wahuni na wezi.
   
 6. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hivi unadhani watanzania wote ni mazumukoko.Tunajua sera hiyo uchwara ina maana gani.Baada ya kuingizwa mkenge na watawala wa dunia,kwa siri wameigiziwa kwa mara nyingine tena upuuzi kama MKUKUTA,MKURABITA nk.mambo ambayo hayatekelezeki kabisa,nia ikiwa ni kuwafikirisha watanzania kwamba serikali yao inawajali,kumbe hamna lolote.Anyhow,siku zenu zinahesabika. QUOTE=CCMTHINKER;1297937]Kilimo kwanza ilikuwa ni sera namba moja ya wachumi wa kikoloni. Walipofika walianza na kilimo kwanza kabla ya elimu .Wakaleta mazao kama mahindi,maharage,mpunga,chai,kahawa,pamba,karafuu nk mazao ambayo hayakuwepo Tanzania.watanzania .Mazao hayo yalipoletwa na wachumi wa kikoloni yalikomboa watanzania walio wengi nchi nzima kichakula na kiuchumi toka miaka hiyo hadi leo hii .Hebu tuwapigie makofi wachumi wa kikoloni kwa kuwa na mipango thabiti endelevu ya kiuchumi ya kusaidia watu wa chini kwa miaka mingi tofauti na wachumi koko wa leo ambao kazi yao ni kukusanya takwimu zisizo na kichwa wala miguu zisizomsaidia mtanzania kutoka kwenye ulofa zaidi ya kuzirundika kwenye maktaba na kongamano za kujadili tafiti maruhuni ambazo wanajua undani wa tafiti hizo ni hao walioziandika wenyewe na wachumi koko wenzao.CCM inajua kilimo kwanza ndio jibu la miaka mingi ya kuondoa umaskini kwani hata wasomi wakistaafu wengi waweza ishi kwa kilimo na ufugaji.
  CCM iliunda sera hii ya kilimo kwanza kwani inajua kuwa Mikopo mingi ya mabenki ya dunia inalipiwa na pesa za kigeni zitokanazo na mauzo ya mazao ya wakulima kama wa chai,kahawa,pamba korosho n.k ambayo ndio uti mkuu wa mgongo wa pesa za kigeni.Hazilipwi kutoka kwa wapiga porojo ZA KISIASA WALIOKO MIJINI NA WASOMI BLABLA wenye majina makubwa lakini wazalishao maneno matupu yasiyobadili hali duni ya mtanzania na watanzania walio wengi.Wala mikopo hiyo hailipwi na na wapiga filimbi wa hamelini waishio mijini wakifanya biashara za maandazi,kuzurura na vilaptop mabegani na umachinga wa kuuza bidhaa za nje vikiwemo vinywaji vya nje na kucheza disco kama pale billicanas Dar es salaam.Baada ya kujua kuwa wakulima ndio wachangiaji wakubwa wa fedha za kigeni na kupitia wao mikopo ya mabarabara nk hulipwa kutokana na jasho lao ikaonelea Kilimo kwanza kipewe kipaumbele.
  CCM baada ya kuona kuwa ili ifanye vizuri ihangaike na walio wengi ambao wako vijijini kwa sera ya kilimo kwanza.Na ndio siri ya CCM kushinda vijijini.Ni sera sahihi sana ya kukomboa walio wengi ambao ni asilimia themanini ya watanzania.Tofauti na sera za vyama vingine ambavyo ukiondoa suala la ufisadi kwenye agenda zao hata huwezi jua sera zao ni nini .wanabaki weupe hawana cha kuwaambia watanzania walio wengi watawatoaje kwenye umaskini.Hawana sera elekezi.Kukosoa tu si sera lazima uwe na kitu concrete cha namna gani utamtoa mtanzania kutoka kwenye umaskini.
  Hongera Rais na Waziri Mkuu kwa sera ya kilimo kwanza inayoweza kukombo walio wengi kiuchumi ambao ni asilimia themanini ya watanzania.Hao asilimia Ishirini wa Mijini wasiwanyime usingizi wamewekewa barabara za lami,umeme,nk na bado wanawanyima kura waacheni na blabla zao. hangakeni zaidi na wa vijijini sasa hivi kama ni rasllimali kwekezwa mijini imetosha boresheni maisha vijijini kupitia sera ya kilimo kwanza.nguvu kubwa za raslimali zielekezwe huko watu wa vijijini sasa iwe zamu ya watu wa vijijini wa mjini inatosha.
  ccmjuu@gmail.com[/QUOTE]
   
Loading...