bwegebwege
JF-Expert Member
- Jul 30, 2010
- 1,071
- 185
Wakuu;
Poleni kwa majukumu mbalimbali ya kuijenga nchi yetu.
Mimi ni mtanzania niliyeajiriwa, nimekuwa na mikakati ya kujiariri mwenyewe na hususan kujiingiza katika sekta ya kilimo. Tayari nimeandaa mikakati na nimewasiliana na wataalamu kadhaa wa kilimo walio tayari kunisaidia. Tatizo langu ni mtaji!
Sasa nafahamu kwamba sasa kuna hii kitu "Kilimo kwanza Initiative" iliyobuniwa na JK na nadhani Mheshimiwa Pinda amekuwa mstari wa mbele sana kuipromote. Sasa nauliza kama kuna yeyote mwenye taarifa za mpango mzima wa Serikali kusaidia watu wenye nia kama yangu? Je, kuna mikopo maalumu (say kupitia fedha kama zile za EPA etc) na mifuko mingine nisiyoifahamu ambapo mimi (kama mwananchi wa kipato cha kati) naweza kupata msaada ili kuendeleza kilimo? Kwa mfano nikiwa nahitaji kupata trekta na pembejeo nyingine, plus capital (in form of loan) serikali ina facility ya namna hiyo?
Kama kuna mwana JF anayefahamu kwa kina, awe na contacts au taarifa za kupata msaada huo au channels husika naomba anisaidie.
Nakaribisha maoni na PM
Nawasilisha