Kilimo kwanza initiative: Nasaidiwaje na serikali/taasisi za serikali?

bwegebwege

JF-Expert Member
Jul 30, 2010
1,055
1,250
Wakuu;

Poleni kwa majukumu mbalimbali ya kuijenga nchi yetu.

Mimi ni mtanzania niliyeajiriwa, nimekuwa na mikakati ya kujiariri mwenyewe na hususan kujiingiza katika sekta ya kilimo. Tayari nimeandaa mikakati na nimewasiliana na wataalamu kadhaa wa kilimo walio tayari kunisaidia. Tatizo langu ni mtaji!

Sasa nafahamu kwamba sasa kuna hii kitu "Kilimo kwanza Initiative" iliyobuniwa na JK na nadhani Mheshimiwa Pinda amekuwa mstari wa mbele sana kuipromote. Sasa nauliza kama kuna yeyote mwenye taarifa za mpango mzima wa Serikali kusaidia watu wenye nia kama yangu? Je, kuna mikopo maalumu (say kupitia fedha kama zile za EPA etc) na mifuko mingine nisiyoifahamu ambapo mimi (kama mwananchi wa kipato cha kati) naweza kupata msaada ili kuendeleza kilimo? Kwa mfano nikiwa nahitaji kupata trekta na pembejeo nyingine, plus capital (in form of loan) serikali ina facility ya namna hiyo?

Kama kuna mwana JF anayefahamu kwa kina, awe na contacts au taarifa za kupata msaada huo au channels husika naomba anisaidie.

Nakaribisha maoni na PM

Nawasilisha
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,666
2,000
Nenda TIB utapata maelezo mazuri,
Mkuu inaonekana hata shamba huna,pili ningekushauri anzisha kampuni ya mambo ya kilimo na uisajili,kisha anza kutafuta hiyo fedha ya serikali. Unaweza kuanza hata kwa kusambaza pembejeo kwa wakulima ili kupitia huko utajifunza mengi. Nilijaribu kutaka kuziotea hizo hela, nikamwomba rafiki yangu mmoja ambaye tayari yuko vizuri ktk kilimo,akaniambia sajili shughuli zako kwanza,hela ipo.
 
Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,934

mkuu MALLILA ntakutafuta mkuu naona utakuwa msaada mkubwa kwngu. mambo yangu yakiwa fresh mkuu! HESHIMA KWAKO!
 
ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,160
2,000
Mkuu Malila na wengineo

Kwa jibu ulilotoa hapo juu ni kwamba ni vigumu sana kwa mkulima wa kawaida anayetumia jembe la mkono kupata msaada wowote ule sababu msaada mwepesi ni mpaka uwe na kampuni ya kilimo iliyosajiriwa.

Mwaka jana nililima mahindi huko tuliani, yaliyonikuta kule ni siri yangu, i mean hakuna msaada wowote ndugu zangu kwa hawa wakulima wa chini kabisa, mimi ndiyo nilionekana bepari mkuu ingawa ki ukweli na mimi nilikuwa nanganga njaa tu na vi hekta vyangu 50. Je ni wakulima wangapi wa jembe la mkono wanaweza kupata access za mikopo katika mabenki haya ya kilimo? kumbukeni kuna wakulima hata kusikia neno Benki tu wanaogopa. je nini kifanyike basi ili tuwashirikishe na wao katika haya mapinduzi ya kilimo tunayotaka kufanya ?

Hii ni challenge kubwa kwa serikali, ndugu zangu kama kweli serikali ina nia njema ya kuwekeza kwenye KILIMO basi imfikirie zaidi huyu mkulima wa hali ya chini vinginevyo sisi wenye uwezo kidogo ndiyo tutaivamia hii secta na kukopa hayo mamilioni na kwenda kuwekeza huko tukimwacha mkulima wa jembe la mkono hapo hapo alipo.

Bado namfikiria huyu mkulima wa jembe la mkono wakuu hana pa kutokea kabisa, nini kifanyike? tuachane naye sisi tusonge mbele wenyewe?
 
JazzBand

Member
Oct 20, 2010
81
95
Kwenye ofisi za kilimo wilayani kwako kuna kitengo kinaitwa mfuko wa pembejeo wanatoa mikopo kununua matrekta na hata kukarabati mabovu,pia kuwezesha juu ya umwagiliaji yaani vifaa na miundo.
Mkopo ni wa miaka 3 riba %6 na kama alivyokutahadharisha Malilo uwe na shamba baadhi ya wilaya ukichukua fomu watendaji wanakuhamasisha kwa kukupigia simu walau wapate kazi ya kufanya wengi wetu hatujui
 
Kweli kabisa, sitaki kuwakatisha tamaa jamaa zangu,ila ni muhimu kurasimisha kazi zetu.
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,666
2,000
mkuu MALLILA ntakutafuta mkuu naona utakuwa msaada mkubwa kwngu. mambo yangu yakiwa fresh mkuu! HESHIMA KWAKO!

Kuna njia nzuri tunayoweza kuifanya,ili kwa pamoja tufanikiwe, hasa kwa wanaotaka kulima (large scale), nina maana kuanzia eka 100 na kwenda mbele, tuunganishe nguvu ili tupate eneo moja kubwa bure kisha tuligawane kwa kilimo, tukifaulu hapo tutakuwa tuko mahali pazuri pa kuibana serikali yetu itusaidie,sisemi tuunde kikundi hapana. Wengi wanashindwa kupata ardhi kubwa kwa sababu wanaogopa kuanzisha mashamba makubwa porini.

Mwaka huu nilipata fursa ya kutembelea mapori fulani huko Moro, yako barabarani/reli,yana maji na ardhi ina rutuba sana haina mwenyewe. Bado natafuta zaidi ili nikipata pori la ndoto zangu nitajichimbia huko nichape kazi kwa kulima na kufuga.
 
kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,022
1,500
Kwenye ofisi za kilimo wilayani kwako kuna kitengo kinaitwa mfuko wa pembejeo wanatoa mikopo kununua matrekta na hata kukarabati mabovu,pia kuwezesha juu ya umwagiliaji yaani vifaa na miundo.
Mkopo ni wa miaka 3 riba %6 na kama alivyokutahadharisha Malilo uwe na shamba baadhi ya wilaya ukichukua fomu watendaji wanakuhamasisha kwa kukupigia simu walau wapate kazi ya kufanya wengi wetu hatujui
\

JAZZBAND unaweza kutoa mfano wilaya ambayo hilo limefanikiwa?
 
King kingo

JF-Expert Member
Sep 6, 2010
401
195
Kuna njia nzuri tunayoweza kuifanya,ili kwa pamoja tufanikiwe, hasa kwa wanaotaka kulima (large scale), nina maana kuanzia eka 100 na kwenda mbele, tuunganishe nguvu ili tupate eneo moja kubwa bure kisha tuligawane kwa kilimo, tukifaulu hapo tutakuwa tuko mahali pazuri pa kuibana serikali yetu itusaidie,sisemi tuunde kikundi hapana. Wengi wanashindwa kupata ardhi kubwa kwa sababu wanaogopa kuanzisha mashamba makubwa porini.

Mwaka huu nilipata fursa ya kutembelea mapori fulani huko Moro, yako barabarani/reli,yana maji na ardhi ina rutuba sana haina mwenyewe. Bado natafuta zaidi ili nikipata pori la ndoto zangu nitajichimbia huko nichape kazi kwa kulima na kufuga.

Mkuu hayo mapori ya morogoro yako sehemu gani?
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,666
2,000
Mkuu hayo mapori ya morogoro yako sehemu gani?

Ukitoka pale mikumi kwenda kidatu, kuna maeneo mazuri sana, na ukitoka kidatu baada ya kupita Mlimba na kabla ya kufika Ifakara. Ukitoka pale Ifakara round about, unavuka mto kidogo kama unakwenda Mbingu, kabla hujafika gereza la wafungwa kuna mapori kibao. Ukitoka mbingu kwenda Chita nako kuna maeneo ya bure kabisa na kote huko kuna maji ya mito na mvua. Barabara ipo na Reli ya Tazara.

Ukiwa na nia nenda Uchindile,kuna ardhi hadi basi.
 
JazzBand

Member
Oct 20, 2010
81
95
\

JAZZBAND unaweza kutoa mfano wilaya ambayo hilo limefanikiwa?

Hapo morogoro karibu na uwnja wa mpira kunayo mambo hayo ukiwa unaelekea njia ya Dom kupitia usemi wa malilo kuuza pembejeo waone tamasco wakiwa kazini tayari wakiuza matrekta ambayo wakulima wamekopeshwa
 
King kingo

JF-Expert Member
Sep 6, 2010
401
195
Ukitoka pale mikumi kwenda kidatu, kuna maeneo mazuri sana, na ukitoka kidatu baada ya kupita Mlimba na kabla ya kufika Ifakara. Ukitoka pale Ifakara round about, unavuka mto kidogo kama unakwenda Mbingu, kabla hujafika gereza la wafungwa kuna mapori kibao. Ukitoka mbingu kwenda Chita nako kuna maeneo ya bure kabisa na kote huko kuna maji ya mito na mvua. Barabara ipo na Reli ya Tazara.

Ukiwa na nia nenda Uchindile,kuna ardhi hadi basi.

Mkuu heshima mbele asante sana kwa maelezo yako ubarikiwe... Uchindile ndio wapi tena maana wengine bado tumeng'ang'ania DSM????
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,666
2,000
Mkuu heshima mbele asante sana kwa maelezo yako ubarikiwe... Uchindile ndio wapi tena maana wengine bado tumeng'ang'ania DSM????

Ukitoka Chita,unasogea mbele kidogo kama unakwenda mgororo, na kabla ya kufika mgororo utafika kwanza Uchindile, kuna ardhi kubwa sana,mvua inanyesha hadi basi,ardhi inarutuba ya kutosha, usafiri wa train/Tazara ndio wa kuaminika ila malori yapo. manpower ipo.

Kuna mwekezaji mmoja tu aliyeingia pale, ni GRL, anafanya vitu vikubwa sana pale.
 
newmzalendo

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
1,377
2,000
mkuu malila,
wazo la kuchukua ardhi kwa umoja ni la msingi,nihesabu mimi ktk hilo kundi.unaposema ardhi ni ya bure,inamaana ni ya kijiji au ipo kati ya kijiji na kijiji hivyo in a no Mans land,tufafanulie kidogo.
 
Haswaaaaa umepatia.
Ardhi kama hii huhitaji watu makini, kwa sababu utakuta wenyeji wanaogopa nguruwe,nyani nk. Ni ardhi ambayo ipo miaka nenda rudi haitumiki na inafaa kwa shughuli za uzalishaji.

Kwangu mimi kuchukua ardhi kwa umoja si wazo ni vitendo, nimefanya sehemu tatu na zote nime/tumefanikiwa, nilioanza nao sehemu ya kwanza nusu waliishia njiani,tuliobaki tumesababisha wengine kujiunga nasi, tukafungua sehemu ya pili kwa mafanikio sana, lakini sehemu zote hizo hazijatosha kiu yetu ya kuwekeza ktk kilimo. Uzuri ardhi tumeiendeleza yote.

Ninachotaka kusema hapa,ni kwamba tukiamua tutafanikiwa sote kwa pigo moja,bora ushirikiano mkuuu.
 
newmzalendo

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
1,377
2,000
Malila! on your next land acquisition kwa kilimo kikubwa nitakuwa nipo ktk kundi,sasa ngoja nianza mpango wa kusaka Tractor MF kwa ajili ya kuendesha shamba,nimeweka lengo la kulinunua ndani ya miaka miwili (realistic time frame).
tafadhali usisahu
 
poa.
 
tajirisana

Member
Sep 29, 2010
83
95
malila, nashukuru sana kwa hizo taarifa hata mimi nimeshatuma mtu huko morogoro akanitafutie maeneo zaidi, ninaanza na hekta 3 nataka kuongeza naoma nipatie namba yako ili tuwasiliane nijumlishe kwenye hilo kundi maramoja twende moro
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom