Kilimo kwanza ibadili muelekeo ndio itanufaisha wakulima

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,375
2,000
Kwa muda sasa serikali imekuwa ikiendesha mpango wa kilimo kwanza ikilenga kuinua kilimo nchini. katika kutekeleza hili serikali imekuwa na mpango wa kugawa pembejeo za kilimo kwa wakulima.

Binafsi nafikiri kwa hali ilivyo kwa sasa katika nchi yetu kwa maana ya kwamba kwa kilimo chetu tunaweza kujitosheleza kwa chakula pembejeo si si kipaumbele cha kwanza bali soko la mazao ndio kipaumbele cha kwanza.

Inasikitisha kuona wapo watanzania wanaozalisha matunda yanaozea mashambani, inasikitisha pale tunapokuwa tunasafiri katika mikoa tofauti unakuta mtu anauza ndoo ya nyanya shilingi 700, mazao ya chakula wakulima wakizalisha kidogo bei zinapanda wakizalisha sana bei zinashuka hivyo kuongeza kwake mavuno kunakuwa hakuna maana bali kipato chao kinabaki palepale.

Kwa wakulima hawa tujiulize wanataka nini ili kuongeza ukubwa wa mashamba yao au kuongeza tija, pengine tuwahoji wakulima wenyewe watueleze kama atalima msimu mmoja akapewa ruzuku bila soko na kutafutiwa soko la uhakika bila ruzuku kipi angependa kitangulie.

Mimi napendekeza serikali kwanza kulifanya mamlaka inayosimamia gala la taifa kuwa inanunua mazao ya aina zote kutoka kwa wakulima hasa ya chakula, pili kufungua mipaka yote kwa watu wanaopeleka chakula nje ya nchi wanunue kutoka magala ya taifa na chakula kiondolewe ushuru ili kiuzwe nchi za jirani bure, ile fedha anayopata mkulima kutokana na kuuza chakula nje ni faida tosha kwa serikali yetu.

Kwa matunda zipo taasisi kama tirdo ambazo zinafanya utafiti wa technolojia washilikiane na SIDO kuunda vikundi au kutafuta wajasiliamali wa kuwakopesha au kuwafundisha ili waanzishe viwanda vidogo vidogo vya kusindika matunda na mboga mboga katika maeneo yenye kuzalisha vitu hivi kwa wingi huku serikali ikipandisha kodi kwa bidhaa za aina hiyo zinazotoka nje ili kulinda soko la viwanda hivi vidogo na sio shirika kama SIDO linalosimamiwa na serikali kusimamia miradi ya kipuuzi kama bidhaa za mianzi, vikapu na mambo mengine ambayo tija yake ni ndogo sana katika uchumi wa jamii zetu.

Tatizo kuwa la wajasiriamali wa Tanzania ni packaging ambapo ukienda SIDO kwa sasa chupa moja ya ml 350 yenye ubora kama wa chupa za maji na juisi ni shilingi 400 sasa mjasiliamali anayeweza kukamua machungwa atauza shilingi ngapi kama chupa tupu bila lebel wala juisi ni 400. Serikali iwekeze katika SIDO kuweka viwanda vya bei nafuu vya kuwasaidia wajasiliamali katika packaging za plastiki, maboksi na mengine.

Wananchi maeneo mbalimbali wana utaaramu wa kutengeneza gongo, hawa tunawakamata na tunaagiza gongo kutoka nje sasa kwa nini tusitafute kiwanda cha kununua gongo kutoka kwa watu na kuisafisha na kuiweka katika chupa ili tujiuzie na tupeleke na sisi nje na hili ni soko mojawapo la mazao ya kilimo.

Wapo viongozi wasiofaa kuwa viongozi wanaodhani wakiwazuia wakulima kuuza nje, wakapiga marufuku ya bidhaa zinazotokana na mazao ya kilimo kama gongo mazao yakawa mengi bei zikashuka ndio wanakuwa wameongoza vizuri kwani mfumuko mwa bei umebaki chini kumbe hao ndio wanatakiwa kufungwa mawe ya kusagia shingoni na kutoswa baharini kutokana na kuwapatia wakulima umasikini huku wakisimama kwenye majukwaa na kulalamika kuwa kilimo chetu kimendelea kuwa cha jembe la mkono.

Mabadiliko ndani ya sekita ya kilimo yataletwa na wakulima wenyewe pale wanapowekewa mfumo mzuri wa soko mambo mengine ya pembejeo wao wenyewe wanaweza kuyamudu pale wanapokuwa wanalima kibishara zaidi.
 

Qualifier

JF-Expert Member
Dec 14, 2012
1,253
1,225
Hongera sana ndugu yangu kwa mawazo ya kimapinduzi, mimi binafsi sijawahi kuona kitu ambacho serikali hii inafanya kwa manufaa ya wananchi wa hali ya chini, sera ya kilimo kwanza imekuwa mara zote inawanufaisha wafanya biashara pamoja na viongozi wa chama na serikali wanao simamia mpango huo. Semina na makongamano ndio yanayo chukua sehemu kubwa ya kasima ya mpango huu, Utakuta katika kijiji wakulima wanapewa mfuko moja wa mbolea kwa bei ya ruzuku kama mkulima anahitaji mifuko kumi basi tisa atanunua kwa bei ya kuruka.

Halafu mara zote mbolea na mbegu za ruzuku vinafika wakati msimu umesha pita. Sasa kama serikali inakusudia kumsaidia mkulima kwa nini isitoe punguzo la kudumu katika pembejeo zote? Pembejeo sio mbelea ya minjingu tu hata dawa za wadudu, magugu, ukungu nk ni pembejeo. Halafu tusiote ndoto kuwa serikali hii isiyo tujali wakulima wadogo kuwa itainuka kwenda kututafutia masoko, ninashauri tuunde vyama vyetu vitakavyo tetea maslahi ya wakulima wadogo.

Ikifika mahala tunatakakupeleka mazao yetu nje na serikali inafunga mipaka, tuungane pamoja kusema HAPANA bila kuogopa msitu wa mabwepande. ninakumbuka mwakajana nwatu tuliwekeza katika kilimo, ninao mfano halisi wa wilaya ya Kilombero watu tuliwekeza katika kilimo cha mpunga kwa kiasi kikubwa sana na mungu alijalia hali ya hewa ikawa nzuri mpunga ulistawi na mavuno yalikuwa mazuri sana ,muda wa mavuno watu tulikuwa tunachekelea kwa furaha huku kila mkulima aliye fanikiwa akijisemea nafsini mwake "umaskini bye bye" cha ajabu wakati watu wanarudisha mazao nyumbani serikali ikafunga mipaka mcele usiuzwe nje na badala yake ikato vibali kwa wafanya biashar wakubwa kuagiza mchele toka nje jambo ambalo lilua soko la mchele na mpunga unatuozea kwenye maghala ya mashine za kukobolea mpunga.

Hii ni serikali inayo lenga kumkomboa mkulima mdogo kweli? mkulia atakombolewa kwa maneno ya kwenye majukwaa wakati wa kampeini za uchaguzi? kwanini serikali mara zote inalenga kumdidimiza mkulima? Mfano mwingine ni pale mkulima anapo gundua kuwa kuna soko zuri la mahindi mabichi sehemu fulani anatafuta mtaji na analima mahindi eka kadhaa ili ayauze yakiwa mabichi kusudi atimize lengo lake iwe nila kujenga nyumba ua kusomesha alimradi ndo lengo lake la kulima mahindi auze mabichi. Cha kushangaza atakapo vuna na kuyapeleka sokoni yanakamatwa kwa madai eti serikali ime piga marufuku kuuza mahindi mabichi, hii nibusara kweli?
 
  • Thanks
Reactions: ego

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,375
2,000
NAWASHAURI WAKULIMA WAUNDE CHAMA CHAO KISICHOKUWA NA MKONO WA SERIKALI AU CHAMA CHA SIASA CHOCHOTE NDANI YAKE KIANZE KUTETEA WAKULIMA KAMA VINAVYOFANYA VYAMA VYA WAFANYAKAZI MATHALANI WALIMU. HAIWEZEKANI NIMELIMA MAHINDI YANGU MTOTO ANATAKA KWENDA SHULE NATAKA KUUZA MAHINDI KUMPELEKA MTOTO SHULE MKUU WA WILAYA ANAPIGA MARUFUKU NISIUZE ETI KUZUIA NJAA. KAMA SERIKALI INAHISI NJAA INAKUJA BASI INUNUE YENYEWE ITUNZE LAKINI KAMA HAWANUNUI WANATUZUIA KUUZA BASI NI SWALA LA KWENDA MAHAKAMANI NA KUDAI FIDIA. INASHANGAZA BIDHAA ZA VIWANDANI KAMA SIGARA ZINAZOPELEKWA NJE ETI SERIKALI INASAMEHE KODI KWA KIGEZO CHA KULETA FEDHA ZA KIGENI KWA MAZAO YA KILIMO LAZIMA YALIPE KODI. NI WAKATI SASA SERIKALI KUUNDA TAASISI YA UCHUMI SAMBAMBA NA TRA INAYOANGALIA MASUALA YA UCHUMI NA KUFANYA MAAMUZI NA SI KILA KIONGOZI MARA WAZIRI, MARA MKUU WA MKOA, MARA MKUU WA WILAYA KILA MMOJA ANATOA AMRI ZAKE BILA KUJUA KUWA BILA YA KUWA NA MPANGO WA PAMOJA WA KUJUA TUNAENDA KUFANYA NINI NA HILI LITAKUWA NA MATOKEO GANI KUANZIA NGAZI YA TAIFA MPAKA KIJIJI. mfano unatoa ruzuku ya mbolea bila shaka mavuno katika kilimo yataongezeka na mazao yakiongezeka ni kama hewa yataanza kutembea kuelekea sehemu yenye upungufu bila kujali ni ndani ya mipaka yako au nje, sasa unakuta mkuu wa wilaya au mkoa bila kujua kinachofanya cha kuwapa mbolea kitasababisha nini mara wanaanza kuona vyakula vinaanza kusafirishwa kuelekea maeneo mengine basi wao wanakurupuka kuweka marufuku na matokeo yake wizara imeweka msukumo kupitia pembejeo ili kuongeza uzalishaji na mkuu wa mkoa au wilaya anazuia maendeleo haya kwa kuzuia soko la mazao yaliyoongezeka mwisho wa siku kilimo kinabaki pale pale na hawa viongozi wote wanasiamama kwenye majukwaa pamoja wakidhani wako pamoja kumbe mmoja anasapoti kilimo mwingine anadidimiza na tafsiri yake ni kuwa wote hawajui wanachokifanya wangekuwa wanajua wangetambuana kuwa huyu anachokifanya kinamaanisha nini
 

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,371
2,000
Mkuu una point, but huu uandishi huu?

Maana hamna aya, koma, herufi ndogo na kubwa humohumo!!
 

CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
6,990
2,000
Kuna jamaa Mmoja Wa Ghana aliwahi kusema Ukitaka kuwa masikini basi fanya hivi, Laumu kila kitu isipo kuwa wewe mwenyewe, Laumu mfumo mzima, Laumu Serikali, Laumu Mabenki kwa kukataa kukupa mkopo uanzishe biashara.

Hapa tutalaumu sana usiki na mchana but wewe mwenyewe chukua hatua huwezi kulaumu huku umekaa kweny keybord haiwezekani hata siku moja, Tuanapenda sana kulauma ila ukweli ni kwamba hata Serikali ifanye nini hakuna tutakacho weza.

Mfano: Migodi ya kule Kanda ya ziwa wanachukua mboga kutoka kenya za kuwalishiwa wafanya kazi wao. Si kwamba wana chuki na watanzania, no ni kwamba hakuna mwenye kuonyesha kuzalisha mboga za kiwango za kuwauzia, mtu unakuta ana mboga matuta matatu analaumu kwamba hapati soko,

Shoprite si kwamba walikuwa wanafanya makusudi kuagzia hadi Mchicha kutoka South, ni kwamba hakuna msambazaji wa uhakika Bongo wote usanii tupu unapewa contract unaanza kwenda kukusanya kwa wauzaji wengine ndo upelelek hilo haliwezekani.

Kuna soko kubwa sana la Matunda nje, But huwezi chuma matunda kwenye gunia upeleke Ulaya au Asia jamaa wanajali afya ni lazima wapime na waone kama yana kidhi ubora,

Ukienda kule Tanga kuna kipindi unakuta wanachuma machungwa mabichi na kuyababua na moto ili yaonekane yameiva kumbe hakuna,

Ni Lazima sisi wenyewe tuamke, tuwe wabunifu,tutafute masoko, tutafute partners wakufanya nao bioashara,
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom