Kilimo kwanza: changa la macho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo kwanza: changa la macho

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Fisadi.Jones, Oct 6, 2009.

 1. F

  Fisadi.Jones Senior Member

  #1
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimeambiwa kinachotokea huko vijijini kwetu, nikasikitika sana. Inawezekana kabisa tulilogwa.

  Mkulima anaambiwa atoe 70,000 ili apewe pembejeo za 600,000. Lakini hali yao ni mbaya mwaka huu kwa kuwa mvua hazikunyesha. Na huu si mda ambao wakulima kwa kawaida wanakuwa safi mfukoni. Na pia huu si mda wa kutayarisha mashamba pia.

  Basi mkulima anaomba kwamba hiyo 70,000. Anaambiwa basi saini haya makaratasi tukupe 10,000. Mkulima anasaini, anapewa 10,000 akalinde njaa angalau kuliko akose kila kitu, watu wanaondoka na pembejeo za 600,000. Inasikitisha kwamba kuna ambao wanapewa mpaka 5,000.

  Kuna mtandao umejengwa kati ya watendaji wa vijiji na mawakala wa pembejeo kupora wakulima hizi pembejeo. Na kwa kuwa mkulima inabidi aje na barua ya mtendaji, basi ukijifanya mjuaji mtendaji anakuwekea ribiti.

  Matokeo yake pembejeo wakulima hawpati. Na hata wale wenye 70,000 inakuwa ngumu kuzipata kwa sababu priority wanaamua watendaji na mawakala ambao wana ajenda yao tofauti.

  Na wakulima wakishatapeliwa hivyo, pembejeo hizo (mbolea, etc) zinapelekwa kuuzwa Kenya.

  Sasahivi watendaji na mawakala walio kwenye mtandao huo huko neema tupu. Magari ya kifahari ndio yanaingia kwa kwenda mbele. Watu wanakuwa matajiri from no where.

  Jitayarisheni na EPA nyingine. Ila hii ni ngumu maana watuhumiwa watakuwa wengi mno.
   
 2. R

  Rayk New Member

  #2
  Oct 6, 2009
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii inchi tunaimaliza wenyewe, kama watu hawana hata huruma kwa wakulima wadogo wadogo ambao ndio wamejaa nchini, tutaweza kuupunguza huo umaskini hata kidogo kwa namna hii
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  sio changa la macho......mpaka sasa kila mkulima anapata mbolea bila usumbufu wowote.....wakulima kila msimu wanapewa ushauri wa kutosha kuhusu kilimo na ufugaji........serikali imejenga uwezo wa ndani zaidi ndio maana korea walitaka tuwauzie sehemu ya jamhuri yetu ili wawekeze kwenye kilimo lakini tukakataa.............kwa kifupi tuna mawazo mengi endelevu ya kujitegemea kiuchumi.............
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Tumuombe Mungu atusaidie maana hali inatisha
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  hili ni changa la ukweli kabisa na lililo kubali na likakubalika.....maisha bora kwa kila mtanzania..........
   
 6. F

  Fisadi.Jones Senior Member

  #6
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ona jinsi tulivyojaaliwa siasa ... tumekuwa na mawazo mengi endelevu tokea uhuru, na bado kuna wenzetu wanapelekewa msaada wa chakula leo hii. Nia njema haimpeleki mtu mbinguni.

  Kwa hiyo unasema hakuna wakulima wanaopewa 5,000 na kuachia pembejeo za 600,000 kwa sababu wamekosa 70,000?

  Unasema kwamba hakuna mbolea ambazo walikuwa wapewe hao wakulima na sasa zinapelekwa Kenya kuuzwa?

  Labda maana yako ya "kila mkulima" inamaanisha kitu kingine. Tupange nikupeleke nikakuonyeshe mkulima mmoja aliyepewa 10,000 na kuachia haki yake ya pembejeo kwa sababu hana 70,000 halafu unielezee unamaanisha nini unaposema "kila mkulima anapata mbolea bila usumbufu wowote".
   
 7. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mimi nina wasiwasi kuwa hii KILIMO KWANZA inaweza kuwa kama yale MABILIONI YA KIKWETE tu. Kwani mimi nimetembea wilaya kama kumi na mbili na zaidi ya vijiji 50 ndani ya wilaya hizo hakuna hata mwananchi mmoja aliyepata hizo pesa za Mhe. Kikwete
  Mie naona kama vile ni mbinu mbinu za kutupeleka vyema hapo 2010 then tutaanza kulia na kusaga meno sisi WABANGAIZAJI
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Wamekwisha amua iwe hivyo kuwa ardhi ya Tanzania iuzwe kwa kaulimbiu ya kilimo Kwanza, kwa hiyo hata mgesema mpaka povu liktoke mdomoni haitasaidia.Cha msingi kuelewa ni kuwa tunarudisha ukoloni bila ya sisi wenyewe kujua au kwa kujua in exchange ya vitu vidogo tu ambavyo hatuna faida navyo. Ardhi sio kitu cha kuchezea jamani. Ardhi ndio chanzo cha migogogro duniani. Utampaje mgeni ardhi kwa miaka 99 huu ni utani oneni majirani zetu Kenya oneni Zimbabwe wanavyohangaika. Sie umri wetu hatuifeel effect yetu tuwafikirie wajukuu zetu vitukuu vyetu vitaenda wapi vitalima wapi jamani.Tusikimbilie short term benefits tuangalie vile vile long time effects ya sera hiyo, tukumbuke kuna global warming duniani, eneo la kaskazini la leo sio la miaka ile sasa linakaribia kuwa semi arid, eneo lote ni semi arid. Translation yake ni kuwa ardhi inayonadiwa na inayopendwa ni ile arrable ambay ni southern Highlands na part of Rufiji basini.Tukiitoa hiyo kwa sandakalawe kwa wawekezaji wale wa Kaskazini na Central ambako ni semi arid watalima wapi kumbukeni kuwa at the same time populaion inaongezeka idadi ya watu haipungui bali inaongezeka kila siku, tukae chonjo jamani tuwe serious na tuipende nchi yetu kwa ukweli kwa faida ya vizazi vijavyo.
   
Loading...