Kilimo kipi kitafaa mtaji kwa mtaji wa Tsh. Milioni 7.5?

ECPENDABLE

Member
Feb 5, 2017
40
7
Wataaalam na wanazengoo kilimo kipi kinalipa mtajii milon 7.5 isiwe tuu perishable fruit na maanisha vyakula vya kuoza hapana sitaweza kulima nataka mazao yenye life span kubwa nakaribisha ushauri.
 
Hiyo hela kabla hujaanza kulima kanunue mazao msimu huu wa kuvuna mfano mpunga Kg 650 uje uuze bei ikichangamka mfano kg 900 au 1000

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wataaalam na wanazengoo kilimo kipi kinalipa mtajii milon 7.5 isiwe tuu perishable fruit na maanisha vyakula vya kuoza hapana sitaweza kulima nataka mazao yenye life span kubwa nakaribisha ushaurii.
Nunua mazao weka store uza bei ikipanda.
 
Iko hivi ndugu. Tatizo kubwa zaidi la shughuli za uzalishaji si mtaji bali mipango (kuanzia malengo mpaka mikakati). Kama kweli uko serious na suala la kuwekeza kwenye kilimo basi tengeneza malengo yako kisha uyawekee mipango na mikakati sahihi. Usianzie kwenye mtaji ulionao bali anzia kwenye lengo ulilonalo.

Mfano. Lengo ni kuwa muuzaji mkubwa wa mchele. Angalia wapi uanzie. Je, utaanzia shambani? Au utaanza kununua mpunga, ku-uprocess na kisha ku-upackage?

Angalizo: Epuka kupoteza muda wako kusikiliza watu wenye mitazamo hasi. Wale watu ambao kwao kila kitu hakiwezekani. Mfano, kuna comment hapo juu imeandikwa "kilimo = umasikini". Hakuna sekta "masikini" Tanzania. Ni vile unavyojiweka. Mawazo mgando siku zote yapeleke kapuni bali yakumbatie yale yanayokuhamasisha.

Pia tumia vema mitandao ya kijamii hususan twitter. Kule kawafuate wale waliofanikiwa kwenye kilimo. Wale negative headed kama kawa wapotezee.
 
Mkulima mie!
healthy_crops_CBpTgbBnp54.jpg
 
Kwa bongo hapa:

KILIMO=UMASKINI
Nchi hii ina safari ndefu sana. Wengi wana mindsets za kimasikini za kudhani mafanikio yako kwenye zile sekta ambazo unafanya kazi umechomekea. Ndiyo ni mitazamo ya kimasikini na ndiyo sababu wazungu hutoka kwao ulaya. Wanakifika wanatafuta maeneo ya porini huko na kuanza kuzalisha bidhaa ambazo sisi tunaziona za kimasikini na kisha kufanikiwa ndani ya miaka michache tu.

Nakumbuka mzungu aliyekuja kuanzisha kilimo cha parachichi za kisasa Rungwe miaka ya 2007. Tulimwona taahira lakini leo hii hiyo ndiyo habari ya mjini. Sasa hivi ndiyo waliomcheka ndiyo wanapanda penuni mwao na kwwnda kukiuzia kiwanda chake kama outgrowers! Sasa hapo umasikini uko wapi? Shambani au kichwani?
 
Wataaalam na wanazengoo kilimo kipi kinalipa mtajii milon 7.5 isiwe tuu perishable fruit na maanisha vyakula vya kuoza hapana sitaweza kulima nataka mazao yenye life span kubwa nakaribisha ushauri.
Mwanazengo ameiliza pesa yake alime nn ,mshaulini cha kulima sio kumtoa nje ya mada,
Hakuna fusaa isiokuwa na hasara au changamoto,anunue mazao gani mpeunga au mahindi.
Mpunga kama sio mzoefu unauziwa mmbovu hata huo msimu ukifika huwezi kuuza kwa faida
Mahindi unatakiwa utafute dawa nzuuuli ndio uyahifadhi tofauti na hapo hupati kitu
Kwa kuwa unataka kulima mm nakushauli ulime mazao ya miezi 3,kama tikiti,vitunguu maji,viazi mvilingo,nyanya aina zote,karoti,hivyo vilimo vinalipa unatakiwa usimie mwenyewe,lkn pia tumia bwana Shamba kwa ushauli WA zao unalotaka kulima
 
Nchi hii ina safari ndefu sana. Wengi wana mindsets za kimasikini za kudhani mafanikio yako kwenye zile sekta ambazo unafanya kazi umechomekea. Ndiyo ni mitazamo ya kimasikini na ndiyo sababu wazungu hutoka kwao ulaya. Wanakifika wanatafuta maeneo ya porini huko na kuanza kuzalisha bidhaa ambazo sisi tunaziona za kimasikini na kisha kufanikiwa ndani ya miaka michache tu.

Nakumbuka mzungu aliyekuja kuanzisha kilimo cha parachichi za kisasa Rungwe miaka ya 2007. Tulimwona taahira lakini leo hii hiyo ndiyo habari ya mjini. Sasa hivi ndiyo waliomcheka ndiyo wanapanda penuni mwao na kwwnda kukiuzia kiwanda chake kama outgrowers! Sasa hapo umasikini uko wapi? Shambani au kichwani?

Wewe una capital(pesa,tech,manpower etc) kama ya huyo mzungu?Au ndo wale wa kwenda kuuzia Maparachichi yao Soko la Matola?hahah

Kilimo ni TAALUMA na sio kwa ajili ya watu waliofeli kwny maisha/wanaotafuta kujiweka bize kama ilivyo huku bongo.

Kwa Bongo Kilimo=Umaskini.

Imeisha hio.
 
Wataaalam na wanazengoo kilimo kipi kinalipa mtajii milon 7.5 isiwe tuu perishable fruit na maanisha vyakula vya kuoza hapana sitaweza kulima nataka mazao yenye life span kubwa nakaribisha ushauri.
Umeeleweka Ila ili upate ushauri sahihi, kuna maswali ya kujibu.

1. Unataka ulime wapi? Hii itasaidia kuamua ulime nini.

2. Shamba unalo tayari au hiyo hela utaanza kukodi shamba au kununua?

3. Tayari eneo la kulima ni shamba safi au nilakusafisha na kung'oa visiki?

4. Unategemea kulima kwa kutegemea mvua au umwagiliaji?

5. Una oulet ya kuuza mazao au unategemea kuuza kupitia madalali.

6. Unaweza kusimamia mwenyewe au unategemea kumlipa mtu mwingine akakusimamie? Hii ni muhimu ili upange uta control vipi hicho kilimo.

Ukisha jibu maswali hayo ni rahisi kupata ushauri sahihi haswa kwenye kuhesabu matumizi na mapato ili uweze kukadiria faida utakayoipata.

Kitakacho fuata ni kuchagua mbegu sahihi kutegemea eneo unalo lenga kulima na haina ya kilimo.
 
Iko hivi ndugu. Tatizo kubwa zaidi la shughuli za uzalishaji si mtaji bali mipango (kuanzia malengo mpaka mikakati). Kama kweli uko serious na suala la kuwekeza kwenye kilimo basi tengeneza malengo yako kisha uyawekee mipango na mikakati sahihi. Usianzie kwenye mtaji ulionao bali anzia kwenye lengo ulilonalo.

Mfano. Lengo ni kuwa muuzaji mkubwa wa mchele. Angalia wapi uanzie. Je, utaanzia shambani? Au utaanza kununua mpunga, ku-uprocess na kisha ku-upackage?

Angalizo: Epuka kupoteza muda wako kusikiliza watu wenye mitazamo hasi. Wale watu ambao kwao kila kitu hakiwezekani. Mfano, kuna comment hapo juu imeandikwa "kilimo = umasikini". Hakuna sekta "masikini" Tanzania. Ni vile unavyojiweka. Mawazo mgando siku zote yapeleke kapuni bali yakumbatie yale yanayokuhamasisha.

Pia tumia vema mitandao ya kijamii hususan twitter. Kule kawafuate wale waliofanikiwa kwenye kilimo. Wale negative headed kama kawa wapotezee.
nimekupata vyema saana mkuuu
 
Nadhani kikubwa n kumpa moyo hsa kuhusu mahali pa kulima, kama ni klimo cha umwagiliaji kwa maji mfereji au mto? Soko la hayo mazao maana kuna mazao ya muda kama ilivyokuwa dengu/ mbaazi. Pia suala la usimamizi maana kilimo kinahitaji mtu atenge muda wa kuliangalia shamba kwa ukaribu sio kumtuma mtu mwingine angalie wakati mkulima yuko mbali na shamba, hapo ataliwa.
 
Umeeleweka Ila ili upate ushauri sahihi, kuna maswali ya kujibu.

1. Unataka ulime wapi? Hii itasaidia kuamua ulime nini.

2. Shamba unalo tayari au hiyo hela utaanza kukodi shamba au kununua?

3. Tayari eneo la kulima ni shamba safi au nilakusafisha na kung'oa visiki?

4. Unategemea kulima kwa kutegemea mvua au umwagiliaji?

5. Una oulet ya kuuza mazao au unategemea kuuza kupitia madalali.

6. Unaweza kusimamia mwenyewe au unategemea kumlipa mtu mwingine akakusimamie? Hii ni muhimu ili upange uta control vipi hicho kilimo.

Ukisha jibu maswali hayo ni rahisi kupata ushauri sahihi haswa kwenye kuhesabu matumizi na mapato ili uweze kukadiria faida utakayoipata.

Kitakacho fuata ni kuchagua mbegu sahihi kutegemea eneo unalo lenga kulima na haina ya kilimo.
Mleta maada hii post muhimu sana kwako.
 
Je unahitaji kulima mahindi na hauna muda wa kusimamia? Au unataka upate mavuno mengi zaidi? Njoo ofisini kwetu.

Ofisi ya YAD yenye wataalamu wabobezi wa kilimo sasa inakuletea mpango wa kusimamia shughuli zote za shambani. Mkulima utatukabidhi shughuli zako pale shambani kwako sisi tutafanya kila kitu kwa utaalamu zaidi na kukukabidhi mazao yako yakiwa yamekomaa. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakuhakikishia kwa ekari moja kuvuna mahindi zaidi ya gunia 30. Usihangaike sasa, sisi tupo kwa ajili yako, Kwa Wale ambao hawana mashamba tutakuwezesha kupata mashamba ya kukodi kwa elfu 40 tu na mashamba ya kununua kwa elfu 60 tu hata ukihitaji ekari 100 za kununua utazipata kwa bei hiyo hiyo.

Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu.
Jengo la NSSF SONGEA
Ghorofa ya 3 chumba no. 317
Simu. 0621133117
 
THE HORTICULTURISTS

Jiunge kwenye kundi letu la whatsap tujadili mada mbali mbali kuhusu kilimo.
Kutana na wataalamu upatiwe majibu ya maswali yako kuhusu kilimo.
 
Back
Top Bottom