Kilimo Kimedorora, Ufukara wa Wananchi Umeongezeka, Kuna Harufu ya Ufisadi Kwenye Mbolea

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
620
1,543
Kilimo Kimedorora, Ufukara wa Wananchi Umeongezeka, Kuna Harufu ya Ufisadi Kwenye Mbolea

[Sehemu ya 4 na ya Mwisho ya Hotuba ya ndugu Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto (MB) kuhusu Mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kwa mwaka 2017/18]

Mheshimiwa Spika,

Ibara ya 31 ya hotuba ya Waziri Mkuu inazungumzia sekta ya kilimo na kueleza kuhusu mavuno ya msimu wa 2015/16 na uhaba wa chakula kwenye baadhi ya maeneo nchini. Hata hivyo Serikali haijazungumzia Kabisa mdororo kwenye sekta ya Kilimo.

Taarifa ya ya robo mwaka ya Benki Kuu nchini, BOT quarterly economic bulletin ya Disemba 2016 inaonyesha kuwa sekta ya Kilimo ilikua kwa kasi ya 0.6% tu kutoka ukuaji wa 2.5%. Asilimia 75 ya Watanzania wote wamejiajiri katika sekta ya Kilimo, hivyo mdororo huu ya sekta ya Kilimo kutoka ukuaji wa 2.5% mpaka ukuaji wa 0.6% ni ishara mbaya mno kwa ustawi wa zaidi ya robo tatu ya Watanzania.

Kwa Vijijini 78% ya Watanzania wanajihusisha na Kilimo. Hii maana yake ni kwamba wananchi wengi vijijini hawafanyi uzalishaji, jambo hili ni hatari sana, ni dalili kuwa ufukara wa watu wetu unazidi. Ni kwa sababu hii, pamoja na uchumi wetu kukua kitakwimu, 7% kwa mwaka, lakini bado wananchi wetu walio wengi wanaishi kwenye dimbwi la ufukara. Maana ukuaji huo wa Uchumi hauhusishi kilimo, hauhusishi zaidi ya robo 3 ya Watanzania.

Ukuaji huu mdogo wa Kilimo unapaswa kuishtua Serikali kwani ni hatari sana, ni hatari mno. Maana unajenga uchumi unaowaacha karibu zaidi ya robo 3 ya Watanzania kwenye ufukara, ni uchumi unaopanua matabaka ya mafukara na matajiri.

Tatizo hasa ni nini? Tatizo kubwa ni sera za Serikali haswa kwenye pembejeo.

Kwanza ilikuwa makosa kwa Serikali kutenga bajeti ndogo ya Ruzuku ya Mbolea kwa wakulima wanyonge wa Taifa hili, karibu 75% ya Watanzania wote. Bajeti ya kwanza ya Serikali ya awamu ya tano ilishusha fedha za ruzuku ya mbolea kutoka Shilingi bilioni 10 kwa mwaka wa Fedha wa 2016/17 kutoka shilingi bilioni 78 za mwaka wa Fedha wa 2015/16. Serikali inayojinasibisha na wanyonge haiwezi kupunguza bajeti ya ruzuku ya mbolea kwa wanyonge.

Hili lilikuwa kosa kubwa kabisa la msingi, Tanzania ni moja ya nchi zinazotumia mbolea kidogo kwenye uzalishaji, uwiano wa mbolea kwa hekari tunazidiwa hata na malawi. Kwa hekari moja Mkulima wa China anatumia mbolea mara 10 ya kiasi anachotumia mkulima wa Tanzania. Kwa hali hiyo ni lazima tija ya Kilimo chetu iwe ndogo, ni lazima uzalishaji uwe hafifu, ni lazima mdororo utokee kwenye sekta ya Kilimo.

Waziri Mkuu anasema kuwa Serikali imesambaza mbolea tani 30,000 Kwa kutumia Kampuni ya mbolea Tanzania. Hili ni jambo jema, hata kama mbolea hiyo ilichelewa kuwafikia wananchi, hata kama kiasi hicho ni kidogo mno.

Lakini Waziri Mkuu anatambua kuwa bei ya kila mfuko wa mbolea imeongezwa kifisadi Kwa shilingi 15,000? Wakati mawakala wa mbolea wa wadogo wananunua mfuko mmoja (mbolea aina ya DAP) Kwa shilingi 55,000 Dar Es Salaam, Serikali ambayo
Imenunua mbolea ya shilingi 10 bilioni imelipa kila mfuko shilingi 65,000 na mpaka mbolea ifike Kigoma, Rukwa, Katavi nk bei inakuwa shilingi 75,000.

Ukiondoa gharama za usafiri, kila mfuko wa mbolea maafisa wa serikali wameongeza cha juu shilingi 15,000. Naomba Waziri Mkuu aagize ukaguzi maalumu kwenye ununuzi wa mbolea aliyotolea Taarifa kwenye hotuba yake. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali akague mfumo mzima wa manunuzi ya mbolea na Taarifa iletwe Bungeni.

Kwangu na Chama changu tunaofuata Ujamaa wa Kidemokrasia, Kilimo ndio sekta ya msingi, ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa, ni sekta nyeti ambayo hatutaacha kuisemea. Hivyo pamoja na hilo la uchunguzi wa suala la mbolea naitaka pia serikali ifanye yafuatayo:

a. Serikali irekebishe hali hii katika bajeti ijayo ili kuhakikisha kuwa inatenga pesa za kutosha kwa ajili ya kununua mbolea.

b. Serikali itenge pesa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza utegemezi wa kilimo cha mvua ambazo zinazidi kutokutabirika

c. Serikali ijenge maghala ya kutosha na Bunge liongeze bajeti ya hifadhi ya Chakula ya Taifa.

Mheshimiwa Spika,

Namtakia kila la kheri Mheshimiwa Waziri Mkuu katika majukumu yake ya kikatiba.

Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge - Kigoma Mjini (ACT Wazalendo)
Bungeni Dodoma
Aprili 11, 2017
 
Safi Sana zito kilimo ndiyo kila kitu ata hao waliyopo huko juu matumbo yamejaa mpaka yanataka kufutuka ni kazi ya mkulima ila Kwa nini sekta ya kilimo inadharaulika kiasi hiki?
 
d. serikali ijenge kiwanda cha mbolea. phosphate deposits zipo za kutosha. hata ifanyeje haiwezi kutosheleza mahitaji kwa ruzuku. dawa ni kujenga kiwanda wananchi wanunue kwa bei rahisi.
 
Hapa Serikali ilishachemka mno na ufukara kwa awamu hii ya hapa kazi tu ndo kiwango kikubwa cha ufukara kitakuwa kwa kiwango cha juu zaidi sasa 'HAPA KAZI TU' hiyo kazi sijui inafanyika wapi maana unapojinasibisha kuwa hapa kazi tu inatakiwa hiyo kazi ionekane lakini kwa hapa Tanzania msemo huu ni tofauti kabisa na wenda ni kazi ya kuongeza ufukara kwa Watanzania.
 
Kilimo Kimedorora, Ufukara wa Wananchi Umeongezeka, Kuna Harufu ya Ufisadi Kwenye Mbolea

[Sehemu ya 4 na ya Mwisho ya Hotuba ya ndugu Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto (MB) kuhusu Mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kwa mwaka 2017/18]

Mheshimiwa Spika,

Ibara ya 31 ya hotuba ya Waziri Mkuu inazungumzia sekta ya kilimo na kueleza kuhusu mavuno ya msimu wa 2015/16 na uhaba wa chakula kwenye baadhi ya maeneo nchini. Hata hivyo Serikali haijazungumzia Kabisa mdororo kwenye sekta ya Kilimo.

Taarifa ya ya robo mwaka ya Benki Kuu nchini, BOT quarterly economic bulletin ya Disemba 2016 inaonyesha kuwa sekta ya Kilimo ilikua kwa kasi ya 0.6% tu kutoka ukuaji wa 2.5%. Asilimia 75 ya Watanzania wote wamejiajiri katika sekta ya Kilimo, hivyo mdororo huu ya sekta ya Kilimo kutoka ukuaji wa 2.5% mpaka ukuaji wa 0.6% ni ishara mbaya mno kwa ustawi wa zaidi ya robo tatu ya Watanzania.

Kwa Vijijini 78% ya Watanzania wanajihusisha na Kilimo. Hii maana yake ni kwamba wananchi wengi vijijini hawafanyi uzalishaji, jambo hili ni hatari sana, ni dalili kuwa ufukara wa watu wetu unazidi. Ni kwa sababu hii, pamoja na uchumi wetu kukua kitakwimu, 7% kwa mwaka, lakini bado wananchi wetu walio wengi wanaishi kwenye dimbwi la ufukara. Maana ukuaji huo wa Uchumi hauhusishi kilimo, hauhusishi zaidi ya robo 3 ya Watanzania.

Ukuaji huu mdogo wa Kilimo unapaswa kuishtua Serikali kwani ni hatari sana, ni hatari mno. Maana unajenga uchumi unaowaacha karibu zaidi ya robo 3 ya Watanzania kwenye ufukara, ni uchumi unaopanua matabaka ya mafukara na matajiri.

Tatizo hasa ni nini? Tatizo kubwa ni sera za Serikali haswa kwenye pembejeo.

Kwanza ilikuwa makosa kwa Serikali kutenga bajeti ndogo ya Ruzuku ya Mbolea kwa wakulima wanyonge wa Taifa hili, karibu 75% ya Watanzania wote. Bajeti ya kwanza ya Serikali ya awamu ya tano ilishusha fedha za ruzuku ya mbolea kutoka Shilingi bilioni 10 kwa mwaka wa Fedha wa 2016/17 kutoka shilingi bilioni 78 za mwaka wa Fedha wa 2015/16. Serikali inayojinasibisha na wanyonge haiwezi kupunguza bajeti ya ruzuku ya mbolea kwa wanyonge.

Hili lilikuwa kosa kubwa kabisa la msingi, Tanzania ni moja ya nchi zinazotumia mbolea kidogo kwenye uzalishaji, uwiano wa mbolea kwa hekari tunazidiwa hata na malawi. Kwa hekari moja Mkulima wa China anatumia mbolea mara 10 ya kiasi anachotumia mkulima wa Tanzania. Kwa hali hiyo ni lazima tija ya Kilimo chetu iwe ndogo, ni lazima uzalishaji uwe hafifu, ni lazima mdororo utokee kwenye sekta ya Kilimo.

Waziri Mkuu anasema kuwa Serikali imesambaza mbolea tani 30,000 Kwa kutumia Kampuni ya mbolea Tanzania. Hili ni jambo jema, hata kama mbolea hiyo ilichelewa kuwafikia wananchi, hata kama kiasi hicho ni kidogo mno.

Lakini Waziri Mkuu anatambua kuwa bei ya kila mfuko wa mbolea imeongezwa kifisadi Kwa shilingi 15,000? Wakati mawakala wa mbolea wa wadogo wananunua mfuko mmoja (mbolea aina ya DAP) Kwa shilingi 55,000 Dar Es Salaam, Serikali ambayo
Imenunua mbolea ya shilingi 10 bilioni imelipa kila mfuko shilingi 65,000 na mpaka mbolea ifike Kigoma, Rukwa, Katavi nk bei inakuwa shilingi 75,000.

Ukiondoa gharama za usafiri, kila mfuko wa mbolea maafisa wa serikali wameongeza cha juu shilingi 15,000. Naomba Waziri Mkuu aagize ukaguzi maalumu kwenye ununuzi wa mbolea aliyotolea Taarifa kwenye hotuba yake. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali akague mfumo mzima wa manunuzi ya mbolea na Taarifa iletwe Bungeni.

Kwangu na Chama changu tunaofuata Ujamaa wa Kidemokrasia, Kilimo ndio sekta ya msingi, ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa, ni sekta nyeti ambayo hatutaacha kuisemea. Hivyo pamoja na hilo la uchunguzi wa suala la mbolea naitaka pia serikali ifanye yafuatayo:

a. Serikali irekebishe hali hii katika bajeti ijayo ili kuhakikisha kuwa inatenga pesa za kutosha kwa ajili ya kununua mbolea.

b. Serikali itenge pesa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza utegemezi wa kilimo cha mvua ambazo zinazidi kutokutabirika

c. Serikali ijenge maghala ya kutosha na Bunge liongeze bajeti ya hifadhi ya Chakula ya Taifa.

Mheshimiwa Spika,

Namtakia kila la kheri Mheshimiwa Waziri Mkuu katika majukumu yake ya kikatiba.

Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge - Kigoma Mjini (ACT Wazalendo)
Bungeni Dodoma
Aprili 11, 2017
Kilimo cha peasant hakitufikishi popote,tuwe na wakulima wakubwa kabisa Wa kibiashara hapo kilimo kitatutoa.mfano mashamba ya OLAM mbinga)Sii MTU analima hatua 10 nje ya nyumba yake anajiita mkulima.Halafu anashusha bei Kwa kuwa ana shida, yule aliyelima Kwa kukopa benki anapata hasara
 
hii topic ina replies tano?! USHILAWADU oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

fb_img_1489897850821-jpg.483578
 
  • Sekta ya kilimo inawaingizia watanzania wengi sana kipato, hivyo ni vyema sekta hii ikapewa uzito unao stahili.
  • 80% ya watanzania ni wakulima therefore kuendeleza kilimo ni kuwaendeleza watanzania wa kipato cha chini.
  • Sekta ya mifugo pia inabid itazamwe kwa jicho la pili kwa sababu watanzania wanafuga kwa mazoea na wanapata faida kiduchu sana hivyo ni jukumu la serikali kuongeza wataalamu wa mifugo....mfano nchi ya botswana ina mifugo michache sana ila inafanya vizur sana kwa kuexport nyama na maziwa afrika.
 
Back
Top Bottom