Kilimo gani kinalipa kwa mvua za Vuli?

Doltyne

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
440
170
Habari za leo wana jamvi,
Mamlaka ya Hali ya Hewa imetoa tamko/ kama sio tangazo la kuwepo kwa mvua nyingi sana kwa kipindi hichi cha Vuli kinachokuja, nadhani ni Oct - Dec flani hivi... Sasa Nina Shamba Dogo tu lenye Heka Tatu, lipo katika eneo lenye muinuko kidogo ila sio mkali kabisa, Sijawahi kulima hapo, aliyekuwa analima sana ni Mama Mzazi, Pana Ardhi nzuri tu, kwa kumbukumbu zangu ameshalima Mananasi, Mahindi, Mihogo nk... Sasa mimi nataka kufuata nyayo zake, nauliza kwa mwenye utaalam na eneo au mvua hizi... Kilimo gani kitafaa kwa mvua hizi za muda mchache? Shamba lipo Dar Es Salaam, Kati kati ya Mbezi ya kimara na Bunju, eneo linaitwa Kibesa, Ni mbele kidogo ya Mpiji Mahohe...

Haya Ndugu, tuitikie wito wa Kilimo kwanza huu... NB: Nina Plan ya hapo baadae kufuga Sato kwa biashara... mwenye info zaidi anaweza kunijuza pia...

Natanguliza shukrani zangu za dhati kabisa kwa wote.

Maa Salaam.
 
kwa Ardhi hiyo ya kimara mbezi Bunju kilimo cha vuri wala hakikufai yani haita kulipa kama una uwezo chimba Kisima ili umwagilie tuu hata huo Ufugaji Wa Samaki unao utaka kama hauna kisima hautaweza kwani maji yote yatakauka baada ya mda
 
Muhogo ni miongoni mwa mazao yenye kustahimili ukame naamini kwa mvua za vuli itakua ni mahala pake vinginevyo uendelee kuatafuta ushauri lakini sishauri upande mahindi maharage na jamii nzima ya mazao yafananayo na hayo.
 
Habari za leo wana jamvi,
Mamlaka ya Hali ya Hewa imetoa tamko/ kama sio tangazo la kuwepo kwa mvua nyingi sana kwa kipindi hichi cha Vuli kinachokuja, nadhani ni Oct - Dec flani hivi... Sasa Nina Shamba Dogo tu lenye Heka Tatu, lipo katika eneo lenye muinuko kidogo ila sio mkali kabisa, Sijawahi kulima hapo, aliyekuwa analima sana ni Mama Mzazi, Pana Ardhi nzuri tu, kwa kumbukumbu zangu ameshalima Mananasi, Mahindi, Mihogo nk... Sasa mimi nataka kufuata nyayo zake, nauliza kwa mwenye utaalam na eneo au mvua hizi... Kilimo gani kitafaa kwa mvua hizi za muda mchache? Shamba lipo Dar Es Salaam, Kati kati ya Mbezi ya kimara na Bunju, eneo linaitwa Kibesa, Ni mbele kidogo ya Mpiji Mahohe...

Haya Ndugu, tuitikie wito wa Kilimo kwanza huu... NB: Nina Plan ya hapo baadae kufuga Sato kwa biashara... mwenye info zaidi anaweza kunijuza pia...

Natanguliza shukrani zangu za dhati kabisa kwa wote.

Maa Salaam.
Nakushauri lima mihogo, ikishashika tu ardhini una uhakika wa kuvuna mwakani na kuuza sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom