Kilimo gani kina asilimia kubwa ya kufanikiwa?

Bella Ciao

JF-Expert Member
May 28, 2019
1,804
4,444
Wakuu habari,

Ningependa kujiingiza kwenye kilimo, lakini bado sijajua ni mazao gani nataka kulima. Nilifikiria kulima mpunga lakini moyo wangu unasita.

Kilimo gani kinaweza kunitoa kimaisha kwa sasa? Ningepata na mchanganuo ingekuwa vizuri zaidi.

Ukiachana na kilimo, pia niliwahi kufikiria kufuga samaki.

Asanteni.
 
Kilimo cha parachichi
Unapanda miche baada ya miaka mitatu unaanza kuvuna
Kilo moja ya parachichi 1200 mpaka1600 inategemea na ubora wake
Wateja ni Wazungu na Wakenya yanasafirishwa nnje
Wanalima Njombe na Mbeya
Mkuu hiyo miaka mitatu sitaweza kuhimili changamoto, atleast maximum miezi 6 Zao linalolimwa zaidi ya muda huo sitaweza
 
Halina changamoto ukilima unarudi zako mjini kuendelea na shughuli zako nyingine kule unatafuta kijana wa jirani awe anachungulia chungulia.
Lima tangawizi
Lima pilipili mwendokasi
Lima viazi mviringo
Hapo kwenye tangawizi inalimwa maeneo gani? Gharama zake je? Vipi kuhusu soko?
 
Soko la pilipili?

Soko la pilipili wala huangaiki hapa hapa bongo unamaliza
Hapo kwenye tangawizi, inalimwa maeneo gani? Gharama zake je? Vipi kuhusu soko?
Soko lake sio zuri sana kilimo ni bahati kuna kipindi kilo moja huwa inakua 4000 na kuna kipidi inashuka mpaka 1000
Wanalima Tanga, Mbeya, Arusha, Morogoro yaani sehemu zenye udongo tifutifu.
Gharama za kulima hapo lazima ukodi shamba kama huna
Lazima ununue mbegu
Gharama za kupanda
Gharama za palizi
Gharama za za dawa
Kilimo sio lelemama funga mkanda ingia shambani ufanye kilimo biashara.
 
Mahindi na mpunga braza. Ila tu ufate tartibu za kilimo na uchaguzu wa mikoa ili ujihakikishie kupata mazao ya uhakika na ubanifu wa pesa.

Usiwaze kuhusu bei. Kilimo hasra yake ni kukosa tu mazao ila yakipatikana tu basi faida ipo kwenye mauzo
 
Kilimo ni Probability otherwise ufnye kilimo cha umwagiliaji,,ila kama unafanya kilimo cha kutegemea mvua za MUNGU, unabet so kubaliana na matokeo yoyote.
 
Hakuna kilimo chenye mafanikio Tanzania, unalima ili maisha yaende na hasara.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom