Kilimo chetu vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo chetu vipi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by chikira, Sep 1, 2008.

 1. c

  chikira Member

  #1
  Sep 1, 2008
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikiangalia kwa mshangao mambo mengi yanayoendelea Tanzania.Kwa mshangao, kwa vile tunafanya mambo yetu utafikiri wote kesho tutakufa,yaani kwa kimombo 'we will all be dead tomorrow'.Hivi kweli kuna 'logic' gani ya kutekeleza utatiti wa kilimo kabisa,huku tukidai kuwa kilimo ni uti wa mgongo.Kuna mtaalam mmoja alisema maneno haya,'a country without research is dead,'yaani kwa kiswahili nchi bila utafiti imekufa!Sasa tunaelekea wapi kama sio shimoni.'There is alot of rhetoric about ASDP',lakini zote hizi ni mbinu za kisiasa za kuwadanganya watanzania.Hakuna hela zinazokwenda moja kwa moja kumhudumia mkulima mdogo.Wanasiasa hawa ni watu wa ajabu sana.Wanasema watapeleka mbinu bora za kilimo kwa wakulima.Sasa,hizo mbinu bora zitatoka wapi bila utafiti?Ni kitendawili.Nadhani wanategemea World Bank, IMF na wafadili wengine kutusaidia.Lakini kwa mtu mwenye akili timamu moja kwa moja angeona hili,kwamba hawa wanaoitwa wafadhili,kamwe nia yao si kutusaidia,lakini wana ajenda zao za siri,ambazo hatima yake sio nzuri hata kidogo kwetu.Serikali kwa ujumla wake, ichukue hatua ya makusudi kabisa, kugharamia utafiti wake.Nchi yetu ni tajiri sana,kwa hiyo uwezo huo upo.Ikiwa Ethiopia na Botswana wameweza hakuna sababu kwa nini sisi tushindwe.Nchi hizo zote ni maskini kuliko Tanzania.
   
Loading...