little hulk
JF-Expert Member
- Jun 20, 2014
- 1,610
- 556
Acre moja ya ufuta inatoa kilo ngapi za ufuta?
Palizi huwa ngapi?mimi nilinunua eka tano kimanzichana kwa 1mil,nikafyeka kwa laki tano pote,nikalima kwa 250,000 kote ,nimepanda ufuta kila eka 35,000 mbegu nilinunua naliendele(lindi white elfu 10,000 kwa kilo),nimepanda na umeota naandaa palizi la kwanza
mimi nilinunua eka tano kimanzichana kwa 1mil,nikafyeka kwa laki tano pote,nikalima kwa 250,000 kote ,nimepanda ufuta kila eka 35,000 mbegu nilinunua naliendele(lindi white elfu 10,000 kwa kilo),nimepanda na umeota naandaa palizi la kwanza
Nimeanza kuvuna ufuta shambani kwangu, kwa sasa nafanya comparison ya bei na wanunuzi. JF ni jungu kuu naombeni member wenye kujua wanunuzi mbali mbali wanipe contacts zao ile nilinganishe bei nifanye right choice ktk kuuza mzigo.
Thanks wadau wote.
Mrejesho:
- kati ya eka 30 nilizopanda ufuta ulistawi vzuri na kuvunwa eka 17..hii ilisababishwa na uangalizi mbovu wa aliyekuwa ananisimamia shamba.
- kila eka nilivuna wastani wa kilo 350, kipindi hiki ( july 2011-2012) wanunuzi binafsi hawakuruhusiwa lindi kununua ufuta, so niliuza kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani @ 1200/= kwa kilo jumla nilipata kama milion 7 kwa msimu mmoja (gharama za kusafisha msitu wa eka 30, mbegu na malipo ya wafanyakazi zilikuwa ni 3.5 milion), sikuingia gharama ya kusafirisha kwa kuwa walinifata shambani.
- Mwaka 2013 sikulima nilipumzisha shamba kwa kulisafisha eka zangu zote 50 na kutanua kidogo (hili shamba lilikuwa ni msitu wakati nalichukua)
- mwaka huo wa 2013 ulikuwa ni mzuri sana kwa upande wa bei, chomachoma (wanunuzi binafsi) waliruhusiwa na ufuta ulipanda bei hadi kufikia 2500 kwa kilo na unalipwa cash hapo hapo. waliolima walipata pesa nzuri tu.
- mwaka huu vijana wanamalizia kupanda shamba nimelima ekari 35, nilibadili team ya wafanyakazi wa shamba kwa kuwa wengi walinikwamisha kwa kuendekeza starehe badala ya kazi. natumaini wanunuzi binafsi wataruhusiwa.
- watu wengi kutoka mikoa mbali mbali (wachaga kibao) wameanza kuvamia misitu na kuiuza au kulima so kwa sasa kumechangamka sana tofauti na 2011 wakati naanza.
- expectations zangu mwaka huu ni ........35(eka) x 400(kg) x 2500(bei/kg)=35,000,000.
- NB: 400kg kwa eka ni kiwango cha chini cha mavuno, wataalamu wa chuo cha naliendele waliniambia kwa mbegu zao za lindi 2002 na malada natakiwa nipate 1200kg kwa eka. Vijana wapo shamba wanachakarika na mi nipo mjini namtumikia mkoloni (ajira).
Thanks kwa wote:
UKITAKA KUUJUA UTAMU WA NGOMA, UINGIE UCHEZE.
Jaman ufuta ekari 5 gunua 30.hilo si kweli.maana mi nimelima sana ufuta ni kwenye ekari moja sanasana unaweza pata gunia moja na nusu.Mkuu kama ukipata details zaidi itakuwa vizuri ukishea nasi. Maana kwa uzoefu mdogo nilionao watu wanapata gunia kama 10 tu kwa ekari 5, lakini kwa mujibu wa maelezo yako kuna uwezekano mkubwa sana wa kutengeneza angalau gunia hata 30 kwa ekari 5.
Pamoja sana mkuu.
Ni mikoa gani ya Tanzania inafaa kwa kilimo cha kibiashara cha ufuta?
Na je soko kuu la ufuta ni nni?
Pwani, Morogoro pia ni mikoa unaweza lima ufuta. Tatizo ambalo naliona ni wanunuz wa huo ufuta kuwa na bei ya ajabu. Mnunuzi mkubwa naye mjua ni MO ila yeye this tme alikua ananunua kwa1600Tsh kwa kg 1 ya ufuta.Ni mikoa gani ya Tanzania inafaa kwa kilimo cha kibiashara cha ufuta?
Na je soko kuu la ufuta ni nni?
Asanteni na vipi gharama za kulima ekari moja?
Mkuu ufuta unastawi ukanda wote wa pwani na maeneo ya karibu nayo, Wilaya zinazoongoza ni Liwale, Kilwa, Nachingwea, Luangwa, Masasi, Tunduru, Songea pia Ifakara, Tanga kiufupi ni maeneo mengi sana mpaka Mbeya ufuta unalimwa. Kuhusu gharama ni za kawaida kama mchangiaji alivobainisha hapo juu na bei kwa miaka mitatu hii (tangu 2014) umekua ukiuzwa Tshs 1500-2000. Na bei zinatofautiana kutokana na maeneo.Ni mikoa gani ya Tanzania inafaa kwa kilimo cha kibiashara cha ufuta?
Na je soko kuu la ufuta ni nni?
Karibu sana mkuu kwenye ulimwengu wa Great Thinkersjf ni kila kitu nimepata hili wazo la kilimo cha ufuta nika google moja kwa moja ikanileta jf,michango yenu mizuri sana nimepata ,na nimeridhika na michango niliokuwa nahitaji, .
Tuko pamoja humu ahsante sana geniusKaribu sana mkuu kwenye ulimwengu wa Great Thinkers
Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app