Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Mimi nilinunua eka tano kimanzichana kwa 1mil,nikafyeka kwa laki tano pote,nikalima kwa 250,000 kote, nimepanda ufuta kila eka 35,000 mbegu nilinunua naliendele (Lindi white elfu 10,000 kwa kilo), nimepanda na umeota naandaa palizi la kwanza.
 
mimi nilinunua eka tano kimanzichana kwa 1mil,nikafyeka kwa laki tano pote,nikalima kwa 250,000 kote ,nimepanda ufuta kila eka 35,000 mbegu nilinunua naliendele(lindi white elfu 10,000 kwa kilo),nimepanda na umeota naandaa palizi la kwanza
Palizi huwa ngapi?
 
mimi nilinunua eka tano kimanzichana kwa 1mil,nikafyeka kwa laki tano pote,nikalima kwa 250,000 kote ,nimepanda ufuta kila eka 35,000 mbegu nilinunua naliendele(lindi white elfu 10,000 kwa kilo),nimepanda na umeota naandaa palizi la kwanza

Naweza kupata eneo la kilimo huko kwa bei nafuu?
 
Nimeanza kuvuna ufuta shambani kwangu, kwa sasa nafanya comparison ya bei na wanunuzi. JF ni jungu kuu naombeni member wenye kujua wanunuzi mbali mbali wanipe contacts zao ile nilinganishe bei nifanye right choice ktk kuuza mzigo.
Thanks wadau wote.

Mrejesho:
  • kati ya eka 30 nilizopanda ufuta ulistawi vzuri na kuvunwa eka 17..hii ilisababishwa na uangalizi mbovu wa aliyekuwa ananisimamia shamba.
  • kila eka nilivuna wastani wa kilo 350, kipindi hiki ( july 2011-2012) wanunuzi binafsi hawakuruhusiwa lindi kununua ufuta, so niliuza kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani @ 1200/= kwa kilo jumla nilipata kama milion 7 kwa msimu mmoja (gharama za kusafisha msitu wa eka 30, mbegu na malipo ya wafanyakazi zilikuwa ni 3.5 milion), sikuingia gharama ya kusafirisha kwa kuwa walinifata shambani.
  • Mwaka 2013 sikulima nilipumzisha shamba kwa kulisafisha eka zangu zote 50 na kutanua kidogo (hili shamba lilikuwa ni msitu wakati nalichukua)
  • mwaka huo wa 2013 ulikuwa ni mzuri sana kwa upande wa bei, chomachoma (wanunuzi binafsi) waliruhusiwa na ufuta ulipanda bei hadi kufikia 2500 kwa kilo na unalipwa cash hapo hapo. waliolima walipata pesa nzuri tu.
  • mwaka huu vijana wanamalizia kupanda shamba nimelima ekari 35, nilibadili team ya wafanyakazi wa shamba kwa kuwa wengi walinikwamisha kwa kuendekeza starehe badala ya kazi. natumaini wanunuzi binafsi wataruhusiwa.
  • watu wengi kutoka mikoa mbali mbali (wachaga kibao) wameanza kuvamia misitu na kuiuza au kulima so kwa sasa kumechangamka sana tofauti na 2011 wakati naanza.
  • expectations zangu mwaka huu ni ........35(eka) x 400(kg) x 2500(bei/kg)=35,000,000.
  • NB: 400kg kwa eka ni kiwango cha chini cha mavuno, wataalamu wa chuo cha naliendele waliniambia kwa mbegu zao za lindi 2002 na malada natakiwa nipate 1200kg kwa eka. Vijana wapo shamba wanachakarika na mi nipo mjini namtumikia mkoloni (ajira).

Thanks kwa wote:

UKITAKA KUUJUA UTAMU WA NGOMA, UINGIE UCHEZE.

Salaam,

Bado wafanya hii biashara ya ufuta. nataka kuanza kama chomachoma- mnunuzi binafsi. ningependa kuomba ushauri.

asante.
 
Mkuu kama ukipata details zaidi itakuwa vizuri ukishea nasi. Maana kwa uzoefu mdogo nilionao watu wanapata gunia kama 10 tu kwa ekari 5, lakini kwa mujibu wa maelezo yako kuna uwezekano mkubwa sana wa kutengeneza angalau gunia hata 30 kwa ekari 5.

Pamoja sana mkuu.
Jaman ufuta ekari 5 gunua 30.hilo si kweli.maana mi nimelima sana ufuta ni kwenye ekari moja sanasana unaweza pata gunia moja na nusu.
 
Wadau naomba anayefahamu soko la ufuta hapa Dar es salaam anisaidie nataka kufanya biashara ya kulangua mikoani na kuja kuuza hapa Dar es salaam.
 
Ni mikoa gani ya Tanzania inafaa kwa kilimo cha kibiashara cha ufuta? Na je soko kuu la ufuta ni nni?
 
Ni mikoa gani ya Tanzania inafaa kwa kilimo cha kibiashara cha ufuta?
Na je soko kuu la ufuta ni nni?
Pwani, Morogoro pia ni mikoa unaweza lima ufuta. Tatizo ambalo naliona ni wanunuz wa huo ufuta kuwa na bei ya ajabu. Mnunuzi mkubwa naye mjua ni MO ila yeye this tme alikua ananunua kwa1600Tsh kwa kg 1 ya ufuta.
 
Asanteni na vipi gharama za kulima ekari moja?

Kilimo cha ufuta hakina gharama kama una eneo tayari. unaweza sema kulima ekari moja ni 50,000/= kutegemea na mahala, mbegu 10,000/= hivi kutegemea na mahala, dawa ya kupulizia 16,000/= ambayo unaweza kupulizia mara 2 kwa vipindi tofauti kwani ufuta huwa unashambuliwa sana na wadudu, unaweza kukodi mpuliziaji 10,000/= palizi 25,000/=.... lakini mkuu hesabu hiyo kwa wakulima wa huku Rufiji sijui sehemu nyingine.

Rufiji ufuta unastawi lakini kutegemea na eneo ila kwa kilwa huwa wanavuna ufuta mwingi sana kulinganisha na huku
 
Ni mikoa gani ya Tanzania inafaa kwa kilimo cha kibiashara cha ufuta?
Na je soko kuu la ufuta ni nni?
Mkuu ufuta unastawi ukanda wote wa pwani na maeneo ya karibu nayo, Wilaya zinazoongoza ni Liwale, Kilwa, Nachingwea, Luangwa, Masasi, Tunduru, Songea pia Ifakara, Tanga kiufupi ni maeneo mengi sana mpaka Mbeya ufuta unalimwa. Kuhusu gharama ni za kawaida kama mchangiaji alivobainisha hapo juu na bei kwa miaka mitatu hii (tangu 2014) umekua ukiuzwa Tshs 1500-2000. Na bei zinatofautiana kutokana na maeneo.

Mfano maeneo ya Kilwa mpaka Tunduru wanunuzi wananunua kupitia vyama vya ushirika hivyo kuna ushuru kadha wa kadha lazima walipe ndio maana bei yao huwa chini tofauti na mikoa wanayouza magulioni ambako gharama za mnunuzi zinakua ndogo mpaka bei huonekana kubwa. Asante.
 
Ufuta una gharama sana, kupalilia hatua kumi kwa kumi buku 1,kupanda kwa kutwa moja buku5,kwa mpandaji na mchimbaji mashimo buku7,hapo hujanunua dawa za kupulizia magugu na za kupulizia wadudu, kukata kutwa buku 5 kiufupi ukitaka kulipa ufuta jipange.
 
JF ni kila kitu nimepata hili wazo la kilimo cha ufuta nika google moja kwa moja ikanileta JF. Michango yenu mizuri sana nimepata, na nimeridhika na michango niliokuwa nahitaji.
 
Back
Top Bottom