Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Thanx mkuu...kwani debe moja huwa lina kilo ngapi? Mi soko langu ni la hao hao waasia...na hiyo bei ni mikoa ya kusini kama Mtwara au kati Singida nk?

Kuhusu ujazo naona mkuu keshakujibu hapo juu na bei ya 30k ni mikoa ya Morogoro na Dodoma. Sina uzoefu kwa mikoa mingine ila wadau wanakuja hapa bila shaka kila utakalouliza litajibiwa hapahapa kiufasaha kabisa!

Ningependa kuitumia fursa hii kwa wale wadau ambao mna pesa ila hamna mashamba basi tuwasiliane haraka msimu ndio huu nitakukodisha shamba langu kwa bei bwerere kabisa!

Nitupieni maombi yenu kwa PM chapchap!
 
Kuhusu ujazo naona mkuu keshakujibu hapo juu na bei ya 30k ni mikoa ya Morogoro na Dodoma. Sina uzoefu kwa mikoa mingine ila wadau wanakuja hapa bila shaka kila utakalouliza litajibiwa hapahapa kiufasaha kabisa!

Ningependa kuitumia fursa hii kwa wale wadau ambao mna pesa ila hamna mashamba basi tuwasiliane haraka msimu ndio huu nitakukodisha shamba langu kwa bei bwerere kabisa!

Nitupieni maombi yenu kwa PM chapchap!

Zao la ufuta hasa linalimwa kwa wingi mikoa ya kusini yaani Lindi na Mtwara na mikoa iliyotajwa ya Dodoma na Morogoro. Kituo kikuu cha utafiti wa mazao hayo yako kule Naliendele nje kidogo ya Mtwara.

Mkoa wa Lindi ndo hasa uongoza kwa uzalishaji mkubwa. Kama ilivyosemwa miezi ya June hadi Septemba wakati ule miti inapukutisha majani ufuta unapatikana sana. Kuna ushindani mkubwa kwani kampuni kama OLAM, METL na nyingine hununua na bei kwa kilo si chini ya 2000-3000/-
 
Kama yako serious ni pm nikute akili jinsi ya kununua mwaka jana tuliwanunulia wa China 500th.
 
Msaada wa hayo masoko jamani.Mi nategemea kulima ekari 500 msimu ufwatao kama nitakua na uhakika na soko hata 1000 nitalima
 
Wana JF,

Kwa wale unaolima ufuta au mnaonunua kwa wakulima wadogo,projection inaonyesha kutakuwa na soko zuri la ufuta mwaka huu. Nimekuwa approached na mfanya biashara mwenye partnership na mchina anaehitaji tani 200,000 mwaka huu wakati wa kuvuna.

Ufuta unahitajika ni lindi 2002. Tupo kwenye maongezi ya awali na nampelekea sample this weekend. Kwa wenye interest stay in touch. Usiulize bei at this stage kwa maana ni mapema mno ila itakuwa nzuri
 
Habari yako Street Smart,

Na mimi nafikiria kuanza kilimo mkoani Lindi hasa Kilwa. Kama unaweza kunisaidia kwa ushauri jinsi ya kupata mashamba na kilimo chenyewe nitashukuru sana.

Unaweza kunitumia kunitafuta kwenye email: imuganyi@conncoll .edu ili tuongee zaidi.

Asante sana.
 
UFUTA

Ni zao linalostahimili baridi na hulimwa maeneo yasiyozidi mita 1500 juu ya usawa wa bahari.Mvua ni Kati ya milimita 400-500 ambazo hutosha kabisa kutoa mavuno Mengi.

AINA ZA MBEGU

Ziada 94,inakomaa Kwa siku 120-130 na inastahimili magonjwa.Ina uwezo wa kutoa mavuno zaidi ya kilo 1000 Kwa heka.
Nal 92,inakomaa Kwa siku 90-110 na inastahimili magonjwa hasa mabaka ya majani.Ina uwezo wa kutoa mavuno kiasi cha kilo 1200-1500 Kwa heka.

MAGONJWA NA NAMNA YA KUYAZUIA


Magonjwa makubwa ya UFUTA ni mabaka na ukungu kwenye majani.Magonjwa haya yasipozuiwa yatapukutisha majani na hivyo kusababisha Mazao kupungua.

KIZUIA

  • Panda UFUTA mapema
  • Tumia mboga zinazostahimili magonjwa Kama-Nal 92
  • Ng'o mimea iliyoathirika
  • Tumia kilimo cha mzunguko
 
Asante Mkuu, unaweza kutoa mwanga kidogo kuhusu masoko ya zao hili? Wasiwasi wangu lisije likawa na changamoto kama za Masoko ya Mpunga na Mahindi, ambapo Majambazi fulani huko "Sirikalini" yanapiga mkwala kuuza mazao hayo ndani na nje ya nchi wakati yenyewe yanaingiza kutoka nje na kuuza kwa bei za ajabuajabu!

Asante!
 
Kuna mtu alinambia kuwa huu ni msimu wa Ufuta huko Mbeya, kwa mwenye taarifa zaidi kuhusu mchakato wa biashara hii huko Mbeya au Dodoma au popote linakopatikana atupatie tafadhali.

Natanguliza shukrani wadau
 
Mi nina tuekari twangu kama 30 hivi Kisarawe nataka nilime ufuta, nitaanza na ekari 5, nisaidieni bei sokoni zinasimamaje now kabla sijatupia mtaji humo.
 
Hakika Mungu ashukuriwe maana naZidi kupata habari muhimu sana juu ya kilimo cha ifuta,mungu aniangazie na atuangazie wote wenye nia ya dhat ya kuingia katika kilimo hiki cha ufuta.

Mwaka huu mwezi wa nane natarajia kuanza kilimo hiki, mwenyezi naomba unipiganie ili malengo na ndoto zangu zitimie. Tuzidi kupeana ujuzi jamani.
 
Ufuta hauhitaji mvua nyingi. Sasa kwa kipindi hiki inaonekana mvua zinaendelea kunyesha tu kiasi ambacho maua yatakuwa yanaharibika na kushindwa kutengeneza matunda vizuri ya ufuta. Hebu tusaidiane hapo nini kinachotakiwa kufanyika
 
Kwa sasa hali ya soko ikoje #masagati and does the business pay good I need your assistance kwa yeyote mwenye uzoefu I wanna invest into the business.

Thanks in Advance.
 
Hakuna shida Mkuu, mimi nimeanza kutayarisha Shamba Mwaka huu nalima UFUTA Eka 10,nitakuwa naleta mrejesho hapa kadri kz itakavyokuwa inaendelea Ila kutembelea kwenye maonyesho ni Muhimu zaidi.

Mku mm pia nimelima ekari 3 tu kwa kuanza ss naelekea kuhitimisha project. Hivi sasa soko zuri linapatika wapi au kunataratibu zipi kwenye kuuza?
 
Wadau niko zangu Dodoma vijijini huku nanunua nunua ufuta na kwenda kuuzia pale Dom mjini na ss hv bei ni 2600 mpk 2650 kwa kilo

Ila ningependa kujua Soko la Dar bei ikoje kwa anaejua ili niangalie km naweza naweza kupeleka mzigo huko

Natanguliza shukrani
 
Back
Top Bottom