Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Wakuu,

Naomba msaada;
1. Je, ufuta unastawi Nachingwea?
2. Na ni aina gani ya mbegu na zinapatikana wapi?

Ahsanteni
Kiongozi hebu nsaidie kunipa elimu juu ya hilo zao. Nimeskia likitajwa tajwa sasa ni vyema tukawa na taarifa kamili ili tujue kuwa kuna opportunity pia kwenye zao la ufuta. Ningependa jua yafuatayo.

1. Soko lake lipoje?
2. Kwenye hekali moja unaweza pata kilo ngapi na kilo moja inauzwaje sokoni??
3. Linachukua miezi mingap hadi kuvunwa
4. Ni maeneo gani yanastawisha zao hili
5. Ni viatilifu vipi vinasumbua zao hili
6. Total cost za kulima zao hili kwa hekali moja
7. Expected profit kwa heka moja.

Ukitueleza haya utakuwa umeshiriki katika kuelimisha umma wa watanzania.

cc - Don Mangi .................................kwa msaada zaidi
 
Wakuu habari zenu,

Mimi nina shamba maeneo ya Mbwenkulu,Lindi nataka kupanda ufuta msimu huu.
Je, ni mbegu gani bora? Nawezaje kuipata? Na ni kwa gharama gani?

Natumai majibu mazuri toka kwenu.

Mungu ibariki JF.
 
Wadau wa jukwaa letu pendwa la "wajasiri wa kutafuta mali" narudi tena kwenu hapa kuomba kutolewa kizani juu ya zao la ufuta. Nimepanga kulima zao ili katika mkoa wa Morogoro katika tarafa ya Kisaki!nimejaribu kudadisi dadisi kwa baadhi ya wenyeji juu ya zao ili, ila bado sijaridhika sana na majibu niliyopata ,na ndio maana nikaona ngoja nikimbilie katika jukwaa letu ili labda nitapata cha ziada!

Kikubwa kwa wale wenzangu wanaopenda kilimo,nilikua napenda kujua yafuatayo juu ya zao la ufuta: Kwanza,je zao ili linaweza toa kilo/gunia ngapi kwa wastani wa heka moja!

Pili: Je gharama za kuanza kuhudumia shamba,kupanda mpaka kuvuna zinaweza kua ni kiasi gani kwa makisio ya juu? Wana Kisaki wamenidodosa kua ni Tsh 250,000/= ila nimeona ni kama gharama ndogo kwa kilimo chenye tija kwa heka moja ya ufuta.

Tatu je ni mbegu gani nzuri ya ufuta kwa maeneo tajwa (Kisaki) itakayo nipa mavuno yenye tija!
 
Huu ufuta hata Mkoa wa Manyara hasa Babati inalimwa sana, na wakulima wakuwa wakifanyiwa Linkage na shirika la Farm Africa ila kwa sasa sijajua wanaendelea vipi make ni long time.

Ila kipindi ni kiwa huko Babati kikazi kilimo cha ufuta kule kilikuwa na Tabia moja, yaani Supply ikiwa kubwa ba Bei ndo inakuw kubwa na supply ikiwa ndogo na bei inakuwa chini.
Why?

Ni kwamba kipindi ambacho wakulima walikuwa wanapata mavuno kidogo wale wanunuzi wakubwa walikuwa wan potezea hivyo kufanya wakulima wakose sehemu ya kuuza, lla kipindi ambacho wakulima walikuwa wana lima kwa wingi na kupata wanunuzi nao walikuwa ni wengi hivyo price ikawa inakuwa juu.
 
Kuna mbegu fupi na ndefu, mbegu fupi ni nzuri mana hata mvua isiponyesha kwa wingi zinastawi vizuri tu, kuhusu wadudu sijawahi kukumbana na tatizo hilonhata sijui mm nalima huko Masasi.
 
Habari za kazi ndugu zangu?

Naomba kuwasilisha mada hii kuhusu kilimo cha zao la ufuta. Nimepitia baadhi ya blog za kilimo nchini, zimeandika mambo mazuri kuhusiana na Fursa ya kilimo cha ufuta, hususani kwa mikoa ya Dodoma, Lindi, Pwani, Ruvuma na Morogoro. Nami nimevutiwa kufanya kitu msimu huu unaoanza.

Naomba kwa mwenye uzoefu/ ufahamu kidogo kuhusu Kilimo cha ufuta tafadhari naomba nisaidiwe kujua maeneo yafuatayo.

1. Muda muafaka wa kulima
2. Changamoto zinazoweza kutazamiwa
3. Upatikanaji wa soko
4. Makadirio ya Juu kwa Ukulima wa Ekari Moja, Pembejeo na mbegu.

Unaweza uka PM, au email me details at. drkinga666@gmail.com

Nitashukuru sana kufahamishwa, Kazi njema!
 
Habari za kazi ndugu zangu?

Naomba kuwasilisha mada hii kuhusu kilimo cha zao la ufuta. Nimepitia baadhi ya blog za kilimo nchini, zimeandika mambo mazuri kuhusiana na Fursa ya kilimo cha ufuta, hususani kwa mikoa ya Dodoma, Lindi, Pwani, Ruvuma na Morogoro. Nami nimevutiwa kufanya kitu msimu huu unaoanza.

Naomba kwa mwenye uzoefu/ ufahamu kidogo kuhusu Kilimo cha ufuta tafadhari naomba nisaidiwe kujua maeneo yafuatayo.

1. Muda muafaka wa kulima
2. Changamoto zinazoweza kutazamiwa
3. Upatikanaji wa soko
4. Makadirio ya Juu kwa Ukulima wa Ekari Moja, Pembejeo na mbegu.

Unaweza uka PM, au email me details at. drkinga666@gmail.com

Nitashukuru sana kufahamishwa, Kazi njema!
Nitakujibu vichache navyojua bila kufuatisha namba zako lakini.

1) Ufuta unaanza kulimwa January, na mwezi May watu wanavuna.

2) Roughly kulima Kwa heka moja kuanzia kuvunja msitu (lindi wanaita kukata useng-) mpaka kuotesha na kuvuna andaa kama kilo 4 au 5.

3) Kuvuna kwa heka kama una bahati waweza kupata labda gunia 7.

4) Mwaka huu tuneuza kilo Tshs 2,500/- kijijini,na ukiweza kuuleta mjini unapiga kama Tshs 4,000/- kwa kilo.

5)..........
 
Tujitahidi kusoma na Topic za wenzetu coz Khs kilimo karibu Mazao yote yameshajadiliwa humu Pamoja na Changamoto zake! ndomana leo ukianzisha mada km hz wachangiaji wanakuwa wachache!
 
Tujitahidi kusoma na Topic za wenzetu coz Khs kilimo karibu Mazao yote yameshajadiliwa humu Pamoja na Changamoto zake! ndomana leo ukianzisha mada km hz wachangiaji wanakuwa wachache!

Mazao mengi bado hatujayachambua na kuyaweka hapa jamvini mfano;

Ulezi sijawahi ona uzi wake, Njegere mbichi za kilolo/Uluguruni sijaona humu, Pilipili mtama za milima ya Matombo bado, Sijaona wazee wakisema cho chote kuhusu Pareto huko Iringa,njombe na mby, Sijaona hoja za mtama mweupe na biashara huko TBL.

Je Viazi vikuu tumevichambua? Kuna Iriki huko Tanga, Kuna watu hawajui Choroko na dengu kwamba ni dili kubwa huko India, Kuna watu wanadhani apples zote zinatoka nje, kumbe zinalimwa hapo Njombe,
Je unayajua marejea na kilimo chake huko Songea enzi zile?

jioni njema.
 
Yaah! nikweli ndugu yangu si mazao yote yalishajadiliwa ila kwa kiasi kikubwa yamejadiliwa Ikiwemo hilo la UFUTA analoliuliza! Mazao ni mengi kwakweli sema tungekuwa na kitu km DATA BASE flan hv yakuweka mada zote!

Mtu akitaka kujua Zao flan pamoja na Changamoto zake anapakua2 anaendelea.
 
Habari zenu wadau,

Leo nimeona nije na mada ili kama kuna watu wenye information zinazoweza kusaidia basi na wachangie ili tuweze kupata faida. Kwa kifupi ni kuwa ninashawishika kujishughulisha na kilimo ili kuongeza kipato na nimeamua kujishughulisha na kilimo cha ufuta.

Ufuta kama zao lingine lolote lina mahitaji yake muhimu. Ninaomba kama kuna yeyote anayeweza kutoa maelezo kuhusu zao hili kwenye vipengele vifuatavyo basi anisaidie.
  1. Je ni aina gani ya mbegu zinazopatikana na kustawi Tanzania, na katika hizo ipi ni bora zaidi.
  2. Kwa ekari moja, kama ukifuata ushauri wa kitaalamu unaweza kupata kiasi gani cha ufuta katika mavuno assuming normal conditions?
  3. Je ufuta unahitaji dawa za kuua wadudu, na kama ni ndivyo inahitajika kufanya zoezi hilo mara ngapi ili kupata mavuno mengi na bora? Pia gharama za kupiga dawa kwa ekari inaweza kufikia kiasi gani?
  4. Je zao hili ustawi katika mazingira gani? Hapa nina maana hali ya hewa, udongo n.k.
  5. Ni mbinu gani za kilimo naweza kutumia kuongeza wingi na ubora wa zao hili.
Wakuu wenye hizi habari tunaomba mfunguke kwa faida ya wengi.

Kwa ekari moja unawe\za kupata kilo 300-500, kilo moja inauzwa 2000/=-2500/=
Gharama zote za kulima, madawa na kuvuna inaweza kufikia laki moja kwa ekari moja.
 
Ufuta!

Nizao pekee lililonistaabisha kwa namna ya mabadiliko ya bei yake kwa kipindi cha miaka 3 iliyopita, bei imekua kwa 150%
msimu unaoisha gunia limepimwa kwa wastani wa 230k kwa mkulima.
Utafiti unastahili, linaweza kuwa mkombozi.

upatikanaji wa wingi wa ufita inategemea na huduma zako kwenye shamba,I mean matunzo.
 
Nimeuza kwa 3,200/=

Mkuu hiyo bei umeuzia wapi?? Msimu wa June 2013 tuliuza kwa 2000/= hadi 2500/= pale Kwedikwazu Handeni Tanga, waliopeleka dar waliuza hadi 3500/= kwa wahindi.

Nadhani ifike mahali wakulima ndo tuamue bei ya kuuzia kwa hawa wahindi tusijekuwa kama wakulima wa pamba wanaolima na kupangiwa bei!
 
Asanteni kwa taarifa wadau, kwa upande wetu sisi tumejiorganise tuko watu watatu.tunatarajia kulima kwenye bonge la ziwa Rukwa large scale.pia naushauri tunaweza unganisha nguvu tukawa tunaexport kwa pamoja nje wadau..
 
Kama huna data usiseme, Ufuta Lindi mwaka huu mwezi wa sita bei ya mwisho wameuza sh2650 hiyo bei ya 1600 ni ya mwaka jana tena ni 1750.

Ni hivi ni kilimo rahisi sana ila kina muda maalumu yaani ukifika muda wa kupanda ni lazima upande, baada ya wiki mbili au tatu ni lazima upalilie, kinachobaki hapo ni kukata matawi ya miti shambani yasichipie kwani yanaweka kivuli na ufuta unashindwa kunawili.

Ukishakomaa ni lazima ukatwe ndani y wiki mi au tatu kutegemea aina ya mbegu kwani kinyume na hapo utamwagikia shambani .
Kabuku ndio wapi uko mkuu..uko Lindi msimu uliopita wameuza 1600 kwa kilo..it means gunia moja hadi laki na nusu, hekari moja ni wastani wa gunia 6 times 150000 = 900000..ukiwa na hekari tano ni =mil 4.5.

Kumbuka gharama za uzalishaji hazivuki laki5
 
Asanteni kwa taarifa wadau, kwa upande wetu sisi tumejiorganise tuko watu watatu.tunatarajia kulima kwenye bonge la ziwa Rukwa large scale.pia naushauri tunaweza unganisha nguvu tukawa tunaexport kwa pamoja nje wadau..

Hongereni wakuu ila mkumbuke UFUTA hauhitaji maji mengi mi nalima eka 10 Januari. Mwaka huu nilikuwa 88 nimepata utaalam wakutosha sana khs zao hili mi natumia Mbegu inaitwa LINDI 2002 Eka 1 gunia 8 hdai 12!

Tutakuwa tunapeana uzoefu kadri cku zinavyokwenda!
 
Wadau nataka kuanza kilimo kikubwa cha Ufuta, nafikiria kuanza mwakani na ekari kama 40 hivi maeneo ya Vigwaza.​

Naomba wadau mnipe ushauri juu ya faida, soko na changamoto za kilimo hiki sina uzoefu wa kutosha na pia ghrama zake za uzalishaji kwa eka.

Pia nafikiria baadaye miaka kadhaa ijayo nijishughulishe na kilimo cha vitunguu saumu, kama kuna mwenye utaalamu wa kulima hii kitu naomba msaada pia. Changamoto zake, soko na gharama zak a uzalishaji kwa eka.

Ahsanteni!!
 
Back
Top Bottom