Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Jamani wadau wa jukwaa la biashara naomba mnisaidie kuhusu hii kitu. Ninafikiria kuhusu hii biashara ya ufuta, ila sijui chochote.

Kwa hiyo naombeni msaada wenu katika hili, mahali inapopatikana nzuri na bei nzuri, soko lilipo (mauzo pia ubora unaohitajika), jinsi nnavyoweza kupata profit vizuri, changamoto na kila kitu kuhusu hiyo bisahara, nawasilisha maswali yangu kwa ma great thinkers naombeni msaada wenu.
 
Nipo Mbeya kwa sasa, natamani sana hio biashara nimesiki debe inakua 15 hadi 25 elfu kutokana na soko, nilisikia MeTL hua ananunua sijajua kwa sh ngapi, huku unapatikana kwanzia mwisho wa mwezi huu wa nne.
 
Kilimo kwa ujumla yake kinalipa sana, hii ikiwa ni pamoja na ufuta. Ila the good thing about kilimo ni kwamba utakuwa mtaalamu zaidi jinsi unavyozidi kulima, na unavyozidi kulima ndivyo utakavyojifunza jinsi gani ya kubana matumizi na kumaximize profit. Ufuta unalimwa sehemu mbali mbali ndani ya Tanzania yetu na soko kubwa la ufuta lipo Dar kwa wadosi. Kwahiyo jinsi unavyolima mbali na Dar ndivyo bei ya ufuta inavyozidi kuwa chini.

Nadhani na Arusha kuna wanunuzi wa ufuta pia Ufuta unashambuliwa na magonjwa mbalimbali pamoja na wadudu, itategemea na sehemu husika ambako utafanya kilimo chako cha ufuta. Kama utalima maeneo ya Rufiji unaweza kupambana na ukungu, magugu yanayotunza wadudu, panzi, etc.

Ila ukilima Arusha unaweza ukakutana na magonjwa tofauti kabisa na utakayo kutana nayo Rufiji. Ndio maana nimesema utaendelea kupata uzoefu wa kilimo jinsi unavyozidi kulima. Kwa kuendelea kulima, utagundua wadudu wanaosumbua ufuta ni wadudu gani katika eneo husika na magonjwa yanayosumbua ufuta ni yapi. Pia utajua dawa gani ni bora zaidi katika kupambana na hayo magonjwa husika.Ila as a general rule ufuta haukui vizuri sehemu inayoweka (tuama) maji kwa muda mrefu.

Mbegu hufa au huzaa ufuta uliodumaa Soko la ufuta ni kubwa sana, ila ugumu wa ulimaji wake hufanya wakulima wengi wakimbie kilimo cha ufuta. Bei za ufuta hupanda takribani kila mwaka kutokana na uzalishaji kushindwa kukidhi mahitaji. Kama unaamua kuanza kufanya kilimo cha ufuta hakikisha unaajiri mkulima ambae ameshalima ufuta zaidi ya mara tatu katika shamba lake awe mshauri wako na msimamizi wa shamba.

Pia unaweza kuwatumia maafisa kilimo. Ila usianze in large scale, anza kidogo huku ukikua kwa vile utakuwa unajifunza. Kilimo kinalipa, ila kinahitaji courage na kutokukata tamaa Kabengwe.
 
Wadau naomba msaada kwa wale wenye idea juu ya wanunuaji wa jumla wa zao la ufuta kwa mikoa ya Dar es salaam, Tanga na Morogoro, ningeomba kusaidiwa kujua na bei ya ununuzi kwa kilo moja ya ufuta!
 
Wadau kilimo hiki nasikia kinalipa ile mbaya gunia moja la ufuta linaenda mpk lak 3 za kitanzania,je kuna yeyote mwenye info za siada kuhusiana na kilimo hiki?
 
Ya Ufuta si kwamba unalipa sana bali una bei kubwa sana, Make ukiona bei iko juu , tambua kwamba kuna ugumu katika hiyo kazi, so kilimo cha Ufuta mpka ufikishe Gunia moja umelima shamba la kutosha,

Ukiona kitu kinauzwa bei ya juu si kwamba kina lipa no ni bei iko juu kulingana na supply kuwa ndogo, Mfano Huku Arusha kuna KAMPUNI MOJA YA MAUA na kuna aina fulani ya maua huwa ukilima unawauzia Kilo Moja Tsh 300,000/ Ila mziki wa kupata hizo kilo si mchezo unaweza lima ukaishia kupata nusu kilo tu,
Kuna rafiki yangu mmoja yupo Dumila, Morogoro yeye huwa analima Ufuta na ktk heka moja anapata magunia manne tu!!, nilishangaa sana.
 
Wandugu ninataka kuanza kilimo cha ufuta mwaka huu kwa kuwa ndio naanza nimechukua heka 5 kwanza ndio juzi tu nimetoka kuandaa shamba. Tunasubilia mvua sasa.

Yoyote anayeweza kunipa uzoefu wa hichi kilimo basi tushauriane hapa..mpango wangu baadae ni kuingia kwenye usindikaji kwa sasa bado nasaka mtaji mzuri.
 
Ya Ufuta si kwamba unalipa sana bali una bei kubwa sana, Make ukiona bei iko juu , tambua kwamba kuna ugumu katika hiyo kazi, so kilimo cha Ufuta mpka ufikishe Gunia moja umelima shamba la kutosha.

Ukiona kitu kinauzwa bei ya juu si kwamba kina lipa no ni bei iko juu kulingana na supply kuwa ndogo, Mfano Huku Arusha kuna KAMPUNI MOJA YA MAUA na kuna aina fulani ya maua huwa ukilima unawauzia Kilo Moja Tsh 300,000/ Ila mziki wa kupata hizo kilo si mchezo unaweza lima ukaishia kupata nusu kilo tu.

Mkuu usiwatishe watu,hakuna ugumu wowote kwenye kilimo cha ufuta..ni kilimo rahisi sana ukifuata taratibu zake kama uchaguzi wa mbegu, kuhudumia shamba kwa wakati, kudhibiti wadudu na mvua kidogo kwani hauitaji mvua nyingi sana maua yanadondoka.
 
Kilimo kinaendelea vizuri wadau..sasa ivi tupo kwenye kipindi cha kupulizia dawa ya magugu,tumelazimika kurudia kupuliza shamba zima maana,mara ya kwanza tulipuliza round up ila ikashindwa kuua majani mapana,sasa tumechanganya na dawa nyingine na magugu yanakufa sasa.
Baada ya hapo muda sio mrefu tutaanza kupanda sasa hii "dhahabu ya kusini".

Habari mimi ni mgeni katika safu hii na ninashamba jipya liko Morogoro lakini kwa kuanza tu ningependa kujua aina ya dawa unazotumia kuuwa magugu na zinapatikana wapi? Ikiwezekana nipatie na bei.

Na pia ningependa sana kujua unalima wapi? na kama naweza pata shamba huko? Maana huko ndiko kwenyewe
 
Njoo wilaya za karibu huku kama Ruangwa, ufuta huku ndio kila kitu, Nachingwea sanasana labda karanga na njugu ndio zinakubali.
 
Back
Top Bottom