kwema wakuu!

nimepitia uzi huu kabla sijajaribu kulima kitunguu saumu. nimekumbana na changamoto hii (tazama picha)....
Habari mkuu
Hilo tatizo linasababishwa na maji kuwa mengi kwenye mmea, hilo zao halitaki maji mengi kama unalima kwa kutegemea mvua lazima iwe hivo na kitunguu haitatengeneza punje, na kama unatumia njia ya umwagiliaji, mwagilia kila baada ya siku 7-9 utapata matokeo mazuri.

IMG_20201014_155717_605.jpeg
IMG_20201005_183607_8.jpeg
 
Aisee kwenye masoko bado tunateseka sana, Kuna mkenya anataka nimpe kwa 50k vile vi net vyao Vinne (4) huku nikuumizana kabisa, Sokoni Kilombero shishimbi inauzwa 80,000/=
 
naombeni muongozo, natamani kilimo hiki, ni mtaji wa sh ngap naweza kuanza nao? kwa hayo mashamba ya iringa? asante
 
Habari wanaJF naitwa Pierre ni mkulima wa kitunguu swaumu pia ni suplier kwa mikoa ya dar morogoro pia na zanzbar kama kuna mtu anauhitaji wa kitunguu swaumu na anauhakika na soko kwenye maeneo yake kwa kiasi chakuanzia gunia moja na kuendelea tuwasiliane kupitia namba 0785092386,0758176570,0620630514,kitunguu kinalipa ulioko mkoa wowote kinafikika ukishakua na uhakika wa soko ntafute tufanye biasharaView attachment 1251709View attachment 1251713View attachment 1251718
Unapatikana wapi mkuu?
 
Habari zenu magwiji wa kilimo!

Wakuu mwaka jana {2020} nililima ufuta ekari 12 Katika wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga, kwa bahati mbaya mvua zilizidi sana kuliko kawaida na kufanya ufuta kuwa mrefu sana, hivyo haukuweza kuzaa vizuri nikaambulia gunia moja moja kwa kila ekari sawa na gunia 13 za kilo miamoja kwa kila gunia moja.

Kwakua sina kawaida ya kukata tamaa licha ya kupata hasara, nimeamua kubadili zao na kulima vitunguu swaumu mkoa wa Iringa nimelima eneo lenye ukubwa wa ekari mbili na nusu, niliweza kukodi shamba, kuandaa shamba na kupanda kupitia kusoma nyuzi za wadau mbalimbali JamiiForums, nashukuru vitunguu vimeota vizuri sana na vina hali nzuri sana vina mwezi sasa tangu vimeota na vinakua kwa speed ya 4G.

Naishukuru JamiiForums na wadau wake kwa kuwa mwanga bora kwa jamii, ila kwa sasa nimeamua kumshirikisha Bwana shamba ili niweze kupata mavuno mazuri. Changamoto niliyo nayo ni kuhusu soko bado sijui.

Nitaleta mrejesho baada ya mavuno.
 
NAUZA BIASHARA YA CAR WASH:

LOCATION: KINONDONI BLOCK 41
NAMBA YA SIMU: 0717 26 33 77

MAELEZO:

MACHINE ZOTE, UJENZI, VYOMBO, SIMTANK, KODI n.k JUMLA: TZS 7,000,000
NIMEBAHATIKA KUPATA KAZI SERIKALINI NA KITUO CHANGU KIKO MKOANI, SO NIMEAMUA KUUZA HII BIASHARA.
 
Habari za mapambano ya maisha,

Naomba msaada mwenye mfanobwa proposal yoyote ya kilimo naomba anisaidie...naandaa mpango wa kilimo wa Vitunguu maji.

Naomba msaada wenu niwekee hapa Pdf au DOC
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom