Wanajamvi kama kichwa kinavyojieleza naomba msaada na maelezo ya kitaalamu ya namna ya kulima kitunguu kwa faida naomba kujuzwa juu ya
Mbegu bora ya kitunguu
Gharama za hekari moja kuanzia hatua ya mwanzo mpaka wakati wa kuvuna kwa hekari moja
Soko na bei ya gunia la kilo 100 pamoja na bei ya kg 1
Madawa na mbolea
Namambo mengine yote yanayohusiana na ulimaji wa kitunguu
Naombeni msaada wenu wa kifikra
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu wanajamvi
 
Habari waungwana. Naomba kufahamishwa, je vitunguu maji vinastawi maeneo ya Kimbiji-Kigamboni?
Ahsanteni
 
Malila unaweza kunipa mwanga kidogo kuhusu bei za hayo maeneo ya Ruaha na hayo mengine kama unafahamu. Nataka nikasurvey na angalau kabla sijaenda huko nijue bei ya kununua kwa eka au ya kukodi kwa eka.

Kilimo Kwanza!
Habari za humu wakuu,,mm ni mgeni haswa kitaka michakato ya kilimo hiki cha vitunguu ,,nlitaka kuanza Lima naweza pata muongozo kutoka kwenu wAdau,,nipo arusha ,nlitaka jua maeno sahihi ya kilimo hiki kwa arusha ,gharama na lini n miezi yake,,upatakanaji wa maeneo na being zake pia ,,,,msaada wakuu
 
Wadau nimejaribu kufuatilia taarifa mbalimbali za kilimo cha zao tajwa hapo juu. Kwa sasa nahitaji kupata maarifa kadha wa kadha kuhusu kilimo cha zao hili. Maswali yanayogonga kichwani mwangu ni;

1. Kwa uptodate data, wapi naweza kupata mbegu kwa uraahisi
2. Mbegu kiasi gani (kilo ngapi, au gunia ngapi zinatosha kwa ekari moja
3. Mbegu hizo zinapatikana kwa bei gani kwa sasa.

Nimejaribu kufuatilia mtandaoni, lakini posts zingine ni za miaka ya nyuma ambayo inaweza isiwe realistic kwa sasa hivi 2018 TZ ya Magufuli

Karibuni wazoefu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom