Kilimo cha Viazi Mviringo (Viazi Ulaya) na Masoko Yake

Young gamez

New Member
Nov 15, 2019
1
20
Jaman humu ndan hali yenu vipi wakuu. Nataka kujua hatua za ulimaji wa viazi mviringo, mambo ya kuzingatia na jinsi ya kuanza. Tusaidiane pia tujuzane, tiririka hapo chini.
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,772
2,000
Hatua ni nyingi ila inategemeana na mambo kadha wa kadha kama ifuatavyo:

1. Msimu unaolima, kuna viazi vya kiangazi na masika ie mwezi wa 11-12 na mwezi 3-7.Sasa unataka kulima vya mwezi wa ngapi.Tukuyu kuna maeneo wanalima hata mwaka mzima.

2. Andaa mbegu ilio bora, kuna ain a nyingi za mbe itayegemea na eneo ulipo.Arusha,Njombe, Mbeya au Iringa.Kwa kawaida heka moja haipungui mifuko 7-11

3. Andaa shamba vizuri, lisiwe na nyasi hata kidogo na lilimwe deep, kwa sababu viazi ni mizizi.

4. Andaa mbolea kulingana na eneo ulipo, uwekaji wa mbolea unatofautiana kulingana na ardhi, DAP, NPK NA CAN, kama kuna mbolea ya kuku nayo ni nzuri ila kuna utaalamu wake.Kama ardhi imechoka kila mfuko wa mbegu kiroba kimoja cha mbolea, kama haijachoka mifuko 4-5 mchanganyiko wa hapo juu.

5. Chimba mashimo sm30 kwa 75.

6. Weka kiazi kimoja kila shimo.

7. Weka mbolea iliochanganywa tafuta wazoefu wa kurusha mbolea au mwaka visoda 2 kila shimo mifuko ya mbolea isibaki hata kidogo,usipunje mbolea bora uzidishe

8. Fukia kwa kuweka vituta vidogo vidogo,usifukie sana vitaoza.

9. Andaa madawa ya muhimu ya kuchoma nyasi,ukungu,mbolea za majani na sumu ya wadudu.

10. Wiki ya 3-4 viazi vitanza kuota, hivyo vikiwa na majani kama matatu hivi piga dawa kuua nyasi na anza dawa ya ukungu na buster kwa msimu wa mvua.

11. Baada ya hapo utapiga dawa hizo 'as a routine' ratiba kwa kila siki 7-14 kulingana na msimu na hali ya hewa iliopo. Mvua nyingi dawa kwa wingi ukizembea unakula hasara hata wiki ya tano tu.

12. Piga palizi ya kwa kwanza kuanzia wiki ya sita na baade wiki 2 mbele pandishia matuta.

13. Subiri changamoto ya soko, unaweza kulima na usiuzee kabisa au ukauza kwa bei nusu iliozoeleka au unaweza piga hela ya hatari na kuuga umasikini.
 
Happy midaho

Member
May 26, 2020
7
45
Kwa uku Njombe shamba laki moja na nusu had lak mbil ukibatika hadi laki moja unapata ukulima kwa heka moja si chin ya laki 850000 had lak 9000000
 
The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
330
1,000
KILIMO CHA VIAZI MVIRINGO (SEHEMU YA 1)​

MAZINGIRA
Viazi mviringo (Solanum tuberosum) hupendelea maeneo yenye baridi kuanzia 7v°C hadi 26°C kwa siku 75 hadi 135 za ukuaji wake au zaidi, Hali ya joto hupunguza kiasi cha uzalishaji. Zao hili hupendelea udongo tifutifu usiotwamisha maji na wenye rutuba na wenye maozea "Matama huruku" (Organic matter) yenye pH ya 5.0 hadi 5.5.

AINA
Nchini Tanzania kuna mbegu za aina yingi za viazi mviringo ambazo hazalishwa na taasisi mbalimbali za utafiti wa kilimo (Agriculture Research Institute). Kwa upande wa Nyanda za juu kusini mwa Tanzania, Taasisi ya utafiti wa kilimo Uyole (ARI UYOLE) iliyopo mkoani Mbeya inazalisha mbegu za viazi mviringo zifuatazo;

1. Baraka
2. Kikondo
3. Tana
4. Arika

Mbegu zote za hapo juu hufanya vizuri endapo utatunza vizuri kwa kufwata taratibu za kilimo bora.

MAANDALIZI YA MBEGU

Kabla ya kupanda viazi mviringo lazima uwe na mbegu zilizotayari kupandwa. Mbegu zilizo tayari kupandwa huwa na machipukizi au maotea. Kama utapata mbegu zenye maotea unaweza ukazipanda. Pia mbegu hizo au kiazi kimoja cha mbegu kinaweza kutoa mbegu 2 au tatu inategemea ukubwa wa hicho kiazi.

Namna ya kuandaa mbegu kutoka kwenye kiazi kimoja (Viazi vikibwa);
 • Kata kiazi hicho katika vipande kadhaa vyenye maotea kila kimoja, maotea yanaweza yakawa zaid ya moja. Yani kila kipande ulichokata lazima kiwe na maotea (buds).

 • Baada ya kuandaa vipande hivyo vianike juani, au kama jua halipo kwa kipindi cha masika vitandaze mahali pakavu ili vikauke. Lengo la kuanika ni kusaidia zile sehemu zilizokatwa zikauke na zijirudi kama kiazi cha kawaida. Ina maana kwamba ukipanda hivyo hivyo mbegu zitaoza.
Namna ya kuandaa mbegu za viazi visivyo na maotea (Chitting);
 • Chagua viazi mviringo vyenye afya
 • Andaa chumba kisafi chenye giza yani kilichofungwa madirisha na milango ili kuzuia mwanga kupenyeza ndani.
 • Weka turubai au mkeka au masalfeti juu ya sakafu (lengo ni kuzuia unyevu wa sakavu kuozesha viazi)
 • Tandaza viazi kwenye chumba hicho kwa levo au ngazi moja.
 • Funga chumba hicho kwa wiki moja au mbili mpaka utakapoona machipukizi yametoka.
 • Ukiona machipukizi yameota basi viazi vipo tayari kupandwa. (Unaweza ukavikata katika vipande na kuviandaa kama nilivyoeleza hapo juu)
Kuandaa mbegu ni jambo la msingi sana ikiwa ni pamoja na kujua kiasi gani kinahitajika kwa eneo husika (seed rate)
Kwa viazi vikubwa vyenye uzito kuanzia gamu 50 na kuendelea kiasi cha mbegu ni magunia 24 kwa hekta moja.
Kwa viazi vidogo chini ya gramu 50, kiasi cha mbegu ni magunia 8 - 10 kwa hekta moja.

KUPANDA
Viazi mviringo hupandwa kwa nafasi ya sentimita 30 kutoka mche hadi mche na sentimita 40 - 75 kutoka mstari hadi mstari. Pia unaweza kutengeneza matuta kwa kufwata nafasi hizo.
Kama utapanda viazi pasipo kutumia matuta basi hakikisha umelima shamba lako kwa kina cha kutosha cha sentimita 30, na viazi vikishaota rundika udongo maeneo ya shina (earthing) hadi kufikia kina cha sentimita 25.

MATUMIZI YA MBOLEA
Tumia mbolea za asili na mbolea za viwandani. Unaweza ukapandia samadi pamoja na mbolea za viwandani kama DAP. Alafu baada ya mimea kutoa maua, weka mbolea ya CAN halafu endelea kupulizia mbolea za maji kama VIGMAX na nyinginezo. Mbolea ya maji unaweza ukaendelea kupiga kila baada ya wiki moja. Ukifanya hivyo utaona matokeo mazuri ya uzalishaji.

Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo
 
kt the irreplaceable

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
1,059
2,000
KILIMO CHA VIAZI MVIRINGO (SEHEMU YA 1)

Ahsante sana
 
Mkombalwiku Orijino

Senior Member
May 24, 2020
101
225
Je unahitaji kulima mahindi na hauna muda wa kusimamia? Au unataka upate mavuno mengi zaidi? Njoo ofisini kwetu.

Ofisi ya YAD yenye wataalamu wabobezi wa kilimo sasa inakuletea mpango wa kusimamia shughuli zote za shambani. Mkulima utatukabidhi shughuli zako pale shambani kwako sisi tutafanya kila kitu kwa utaalamu zaidi na kukukabidhi mazao yako yakiwa yamekomaa. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakuhakikishia kwa ekari moja kuvuna mahindi zaidi ya gunia 30. Usihangaike sasa, sisi tupo kwa ajili yako, Kwa Wale ambao hawana mashamba tutakuwezesha kupata mashamba ya kukodi kwa elfu 40 tu na mashamba ya kununua kwa elfu 60 tu hata ukihitaji ekari 100 za kununua utazipata kwa bei hiyo hiyo.

Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu.
Jengo la NSSF SONGEA
Ghorofa ya 3 chumba no. 317
Simu. 0621133117
 
fungi06

JF-Expert Member
Jul 1, 2020
431
500
Kama upo dodoma unataka gunia za viazi vya mbea (viazi obama vinene) nicheki
0755962963
Gunia moja 37000tsh
 
munroe

Member
Apr 3, 2019
8
45
Nipo mbeya - Rungwe kwamahitaji ya viazi mviringo nitafute tupo kwenye mavuno sasa karibu 0756416149
 
Risk takker

Member
Feb 28, 2015
18
45
Habari ndugu zangu ,Tunapatikana Mbeya Vijijini kwa mahitaji ya viazi mviringo aina ya Obama ,Wasiliana nasi ,Gunia kwa sasa bei ni sh 30,000 ,Unafika mpaka shambani unaangalia viazi ukilizika/ukivipenda tunafanya biashara ,Kwa wahitaji njoo DM tuongee nikupe na mawasiliano yangu.
 
Majan

JF-Expert Member
Jul 2, 2015
945
1,000
Habari ndugu zangu ,Tunapatikana Mbeya Vijijini kwa mahitaji ya viazi mviringo aina ya Obama ,Wasiliana nasi ,Gunia kwa sasa bei ni sh 30,000 ,Unafika mpaka shambani unaangalia viazi ukilizika/ukivipenda tunafanya biashara ,Kwa wahitaji njoo DM tuongee nikupe na mawasiliano yangu.
Kwasasa bei inaanza kuimarika,mlio na mali shambani sasahiv walau mtapiga hela
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom