Kilimo cha Vanilla nchini Tanzania

Mkuu bei yake ni laki 3 na nusu na ni zao ghali sana hili
Kwa UK kg moja ni £445 (1,3m hivi
Mhhh, mwaka huu, Morogoro(Matombo), Vanilla imekuwa haieleweki bei. Wakulima wa Vanilla Matombo walichukuliwa vanilla zao na kuambiwa kutokana na Corona, bei haieleweki kwenye soko la dunia. Baada ya mwezi wakaletewa elf 5,000 kwa kilo, alafu wakaongezewa elf 9,000/=. Kwahiyo mwaka huu vanilla Morogoro imeuzwa kwa elfu 14,000/= kwa kg 1. Ni zao gumu kwenye uchavushaji ua lake, ulimwa zaidi kwenye migomba inayopenyeza jua kwa kiasi kidogo. Ebu nipeni soko Lake zinapouzwa.
 
Mhhh, mwaka huu, Morogoro(Matombo), Vanilla imekuwa haieleweki bei. Wakulima wa Vanilla Matombo walichukuliwa vanilla zao na kuambiwa kutokana na Corona, bei haieleweki kwenye soko la dunia. Baada ya mwezi wakaletewa elf 5,000 kwa kilo, alafu wakaongezewa elf 9,000/=. Kwahiyo mwaka huu vanilla Morogoro imeuzwa kwa elfu 14,000/= kwa kg 1. Ni zao gumu kwenye uchavushaji ua lake, ulimwa zaidi kwenye migomba inayopenyeza jua kwa kiasi kidogo. Ebu nipeni soko Lake zinapouzwa.

Asante Mkuu kunifungua kwa kweli hiyo bei ya TZ nilikuwa najua hivyo
Kwa kweli wakulima wa huku ni bora wa Madagascar
Sina usemi zaidi
 
Duh,asante sana mkuu,hii info ni muhimu sana

Hiyo ndio bei nilikuwa naijua kwani kuna wakati kabla ya mambo ya corona ( kama mdau hapo juu alieweka bei ya sasa)
Niliongea na jamaa Kagera akaniambia anauza kwa laki 3.5/kg ila kama imeshuka hivyo ni hatari
 
Hiyo ndio bei nilikuwa naijua kwani kuna wakati kabla ya mambo ya corona ( kama mdau hapo juu alieweka bei ya sasa)
Niliongea na jamaa Kagera akaniambia anauza kwa laki 3.5/kg ila kama imeshuka hivyo ni hatari
Hiyo yng ilikuwa ni kitambo sana,sasa hv itakuwa sahihi hyo yako au hyo nyingine,hili zao ni balaa sana,sio kwa bei hizo
 
Ni kweli Vanilla ni zao ambalo bei yake inabadilika mara kwa mara hata kwenye soko la Dunia na huko Madagascar pia. Hii inajulikana kote.
Sasa hivi kweli Covid-19 imeathili bei yake Kama alivyo mazao mengine na bidhaa zingine.
Hii siyo sababu ya kukuzuia wewe mkulima kuendelea na mpango wa kulima hili zao. Kesho Unaweza kuamuka na bei ikawa juu sana. Sasa hivi chanjo ya Corona imeanza kutumika. Mambo yanaweza kubadilika.
 
Mkoa wa kagera hasa wilaya ya Missenyi, kulima vanilla ni kuweka maisha yako rehani.. wahuni wanaiba hata kabla haijakomaaa wanauza Uganda kilo 200k na kuendelea.

Kuna mzee nimeona kazungushia shamba la vanilla electric fence na na camera na mataa kama yote.

Kuna mashamba mengine walinzi wamechinjwa ili vanilla ichukuliwe.

Ukifanikiwakulima vanilla na ikakomaa bila shida au wizi, fungu lake ni nono sana.
Hizi sio mindset za kushea na watafutaji mkuu. Kila kitu kinatakiwa kitafutiwe solution yake.

Nilitegemea utawapa angalizo luqa kuna changamoto ta wizi wakiingia kwenye hiki kilimo wajipange kukabiliana na changamoto hii.

Lakini pia wizi wa vanilla umepungua sana miaka hii miwili, msimu uliopita na msimu huu kwa sababu bei ya vanilla imeshuka na hivyo kumekuwa na ushindani sana katika soko la dunia, ili uwese kuuza lazima upeleke mzigo ambao ni high quality ukipeleka mbaya hazinunuliwi badala yake wanachukua za Madagascar. Hivyo matajiri wengi waliokuwa wananunua vanilla changa za wizi ambazo hazijakomaa wameacha kabisa huo mchezo.

Sisi tunaolima ndo tunaosema hivyo, sasa nyie mnaosikia kwa wenzenu mnatuaminishaje??
 
Kuanzia kiroka kwenda juu kote sababu ni mwinuko 800m+ na udongo wa asili ya kivolkano au tindikali.
Mwisho hali ya hewa ya mlimani (Micro climate) hivyo kinole,mkuyuni mpaka matombo sifa zimekidhi na ubaya wa hayo maeneo hakuna zao linakataa.


Ni hivi sehemu inayostawi chai/kahawa bhas migomba au parachichi na macadamia lazima viote na hivyo vitu huambatana na zao la viungo na asilia ya hayo maeneo ni ya mwinuko au nyanda za juu kiikolojia hivyo uhusiano wa baridi,udongo na mvua upo pale pale
Uluguru+usambara na maeneo mengine ya mwinukoni.
Morogoro, Matombo eneo la juu la milima ya Uluguru zinakubari sana, zinatoa masuke makubwa sana kwenye migomba ya ndizi. Tatizo madalali wanalalia sana.
 
HABARI wakuu

SHAMBA+ ni mtandao unaotumia App, Whatsapp channel na SMS utakaokutanisha wadau wote wa kilimo ie Wakulima, Bwana shamba, wauzaji pembejeo na mbegu na madawa, na masoko ya bidhaa za kilimo. Kazi/dhumuni la huu mtandao ni : (i) Ushauri wa kilimo kutoka kwa agronomist - NI BURE kama unatumia WHATSAPP au APP, kama ni SMS utalipia (ii) Maswali na majibu kati ya mkulima, Agronomist, wauzaji pembejeo - NI BURE kama unatumia WHATSAPP au APP, kama ni SMS utalipia (iii) Agronomist kuweza kuona maduka ya pembejeo/mbegu, wakulima mbalimbali na Agronomists wenzao wa mikoa mbalimbali na kuweza kuwasiliana na kujitangaza - NI BURE ila ni kwa kutumia APP NA WHATSAPP tu (iv) Kuona masoko na kuwasiliana na wanunuzi wa mazao - NI BURE ila ni kwa kutumia APP NA WHATSAPP tu
 
habari wakuu....?
nimerahisisha kwa sasa unaweza kuingia kwenye hizo link ukajibu maswali ya survey kirahisi...

hii ni maalum kwaajili ya wakulima

 
Wakuu hivi hichi kilimo cha vanilla kina ukweli au ndio kilimo cha hesabu za karatasi aka pdf!?
Screenshot_20210307-102141_Instagram.jpg
 
Hela ipo tatizo bei haipo stable inaweza kufika laki 8 kwa kilo mwaka huu na mwaka unaofuata ikawa laki 1 kulingana na mahitaji ya soko la dunia. Vitawi vinauzwa elfu 2.. hiyo vanilla ya greenhouse waachie wenyewe nahisi wanataka kupiga hela za kutengeneza greenhouse (puuza hilo tangazo)
Kuipata kilo moja ya dry vanilla si lelemama kwakifupi ni kilimo kigumu
 
nakumbuka kwa mara ta kwanza nikiwahi kuiona matommbo huko morogoro juunkule miliman.aisee kuna had karafuu na warab wapo.kilo yake sio mchezo mana nimmpaka vile vijan vikauke
 
Back
Top Bottom