Kilimo cha Vanilla nchini Tanzania

Naomba elimu kidogo hilo zao ni kwa ajili ya nini chakula matibabu ni nini mbona bei juuu mno?
 
Mi nataka kujua masoko yake,huku kwetu Kweuma Wilaya ya Mvomero tunailima sana ila wanunuzi wanatuambia eti kg ni elf70 wakati tetesi ni laki2.5.

Hawatupigi kweli???
 
Mi nataka kujua masoko yake,huku kwetu Kweuma Wilaya ya Mvomero tunailima sana ila wanunuzi wanatuambia eti kg ni elf70 wakati tetesi ni laki2.5.

Hawatupigi kweli???

mimi nanunua nipigie simu 0652472486


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Baada ya kusoma bandiko hili nilihamua kuingia shamba na kujaribisha miche 200 ya Vanilla. Matokeo mpaka sasa si mabaya. Wataalamu wananiambia mwakani nitakuwa na maua mengi zaidi

1606170039385.jpeg
 
Kilimo Bora Kinahitaji Nguvu Zote.

MSAGA SUMU uhusiano wa ukubwa wa shamba na kiasi cha vanilla utakacho pata upo vipi mkuu?(Optimum)

Maana uangalizi ni mkubwa sana unahitajika.
 
Katika mkoa wa Kagera zinalimwa sana hivi sasa ila pollination inawapa shida sana

Mkoa wa kagera hasa wilaya ya Missenyi, kulima vanilla ni kuweka maisha yako rehani.. wahuni wanaiba hata kabla haijakomaaa wanauza Uganda kilo 200k na kuendelea.

Kuna mzee nimeona kazungushia shamba la vanilla electric fence na na camera na mataa kama yote.

Kuna mashamba mengine walinzi wamechinjwa ili vanilla ichukuliwe.

Ukifanikiwakulima vanilla na ikakomaa bila shida au wizi, fungu lake ni nono sana.
 
Back
Top Bottom