Allen key
Member
- Jan 2, 2019
- 56
- 34
Umenena vizuri sana mkuu na kutoa honyo juu ya kukurupukaMkuu,
Msije mkaingia kichwa kichwa,mambo sio marahisi hivyo, Mosi Taarifa VANILLA INTERNATIONAL LIMITED kwa kiasi kikubwa sio kweli, Marando ya vanilla bei yake sio 20,000= bei yake ina range kati ya 3000 mpaka 5000
Bei ya vanilla duniani mara nyingi inapanda na kushuka na hii inategemea hali ya soko la Madagascar ambao ni waalishaji wakubwa duniani...kwahiyo mwaka huu inawea ikawa kubwa mwaka ujao ikawa ndogo, tangu nianze kulima vanilla sijawahi na wala sijui kama ntakaa niue kilo moja beans kwaaidi ya TSH Milioni kama wanavyotangaa
Ushauri wangu...kilimo cha vanilla sio kibaya ila kabla ya kuingia tambua
1- Ni labor intensive , uchavushaji wa vanilla unatumia mikono
2-WeZi; kwa maeneo hususan ya kagera na baadhi ya maeneo ya kilimanjaro kipindi cha mavuno kunakuwa na wii mkubwa saana
3- Jua soko lko au soko la hao wanaukulimia, kwa kiasi kikubwa wakulima wengi wanaingia hasara kutokana na kutokujua soko lake, mtu anaenda kulima akishakaribia kuvuna ndio anarudi mezani kaunza kufirikia atamuuzia nani...hapa nashauri kabla hujaenda sokoni plz anza kutafuta soko kwanza ikiwezekana ingia namnunuzi mkataba
4...Jifunze utambue ABC za vanilla, hii itakusaidia kuepusha kudanganjwa
5- Nashaurii ukilima vanilla plz panda kwenye shamba lako mwenyewe, mche wa vanilla unaweza dumu mpaka miaka 40 ukiangaliwa na kuhudiumiwa vizuri
Hitimisho
Mimi nalima vanila kwa mkataba ( contract farming), mapato yake sio kama yanavyotangazwa na hawa wajasiriamali. ninaliama na kampuni ya .....Natural Extracts Industries Ltd...hawa ndio wanaonunua, na wananipa huduma za ugani
Muwe na kilimo chema