Kilimo cha Vanilla kingekuwa rahisi namna hii, hakuna mkulima angekuwa maskini

Lasway.Jr

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
229
500
Salama wanajamvi , sitaki kuandika mengi sana ila wakulima wa nchi hii wanapitia mengi sana magumu hasa kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi na utaalamu , basi ngoja niwaletee stori ambayo nimeitoa kwenye group Moja la WhatsApp kuhusu kilimo cha Vanilla je ni kweli? Kila mmoja adondoshe comment yake Ili tupate maarifa , naanza na hawa jamaa wa Vanilla international huwa nawasikia sana

C&P
VANILLA INTERNATIONAL LIMITED
napenda kukualika KWENYE kilimo Cha Hela nyingi Cha ZAO LA VANILLA. Wekeza pesa kwa ili tukusaidie kukujengea Banda kitalu yaani SHAMBA kitalu (GREENHOUSE) kwa ajili ya KUKUPANDIA marando ya VANILLA ambayo ndilo zao namba moja kwa kuzaa sana na kwa kuwa na BEI KUBWA KWA KILO MOJA. Wastani wa BEI YA VANILLA NI TZS 1,500,000/=

MATARAJIO YA MAVUNO YA VANILLA:
Mche mmoja wa VANILLA INAZAA matawi 10 kwa mwaka na kampuni ya VANILLA INTERNATIONAL LIMITED inanunua matawi(marando) kwa Tzs 20,000/= kwa kila random(#VANILLACUTTINGS).
Hii Ina maana kuwa mche mmoja wa VANILLA utakuzalishia Tzs 200,000/= kwa kila MWAKA KWA KUUZA MARANDO TU(#VANILLACUTTINGS). Kwa hiyo ukiwa na Miche 100 itakuzalishia Tzs Milioni 20 kwa KUUZA MARANDO YA VANILLA (#VANILLACUTTINGS).

VANILLA BEANS (MAHARAGE YA BANILLA):
Mche mmoja wa VANILLA UNAZAA kilo 15 kwa wastani na Bei ya Vanilla mbichi kwa kilo ni TZS 220,000/= na hivyo kukupatia mpaka Tzs 3,000,000/= kwa mche mmoja. Kwa KIFUPI ZAO LA VANILLA LINA PESA KULIKO MRADI WOWOTE WA KILIMO. I MEAN VANILLA HAIFANANI NA MAHINDI, KAHAWA, KUNDE, PARACHICHI,MITI, MAHARAGE, VIAZI, STRAWBERRY, NDIZI WALA MPUNGA KAMA ULE MRADI WA MASANJA MKANDAMIZAJI.

MAADA itaendelea hivi karibuni.
Ila waweza kupata baadhi ya GHARAMA ZA GREENHOUSES ZA VANILLA:
UKUBWA (SQM). ..... BEI(000,000/=)
40. 3
72. 4
120. 6.2
200. 8.7
300. 12
400. 18
600. . 22
800 . 25
ROBO HEKA . 33
NUSU HEKA . 56
HEKA. 87
HEKA 2. 140
HEKA 4. 200.

(Negotiable).
Nb: LAZIMA UWE NA MTAJI
 
Prodigal Son

JF-Expert Member
Dec 9, 2009
1,002
2,000
Mkuu,
Msije mkaingia kichwa kichwa,mambo sio marahisi hivyo, Mosi Taarifa VANILLA INTERNATIONAL LIMITED kwa kiasi kikubwa sio kweli, Marando ya vanilla bei yake sio 20,000= bei yake ina range kati ya 3000 mpaka 5000

Bei ya vanilla duniani mara nyingi inapanda na kushuka na hii inategemea hali ya soko la Madagascar ambao ni waalishaji wakubwa duniani...kwahiyo mwaka huu inawea ikawa kubwa mwaka ujao ikawa ndogo, tangu nianze kulima vanilla sijawahi na wala sijui kama ntakaa niue kilo moja beans kwaaidi ya TSH Milioni kama wanavyotangaa

Ushauri wangu...kilimo cha vanilla sio kibaya ila kabla ya kuingia tambua

1- Ni labor intensive , uchavushaji wa vanilla unatumia mikono

2-WeZi; kwa maeneo hususan ya kagera na baadhi ya maeneo ya kilimanjaro kipindi cha mavuno kunakuwa na wii mkubwa saana

3- Jua soko lko au soko la hao wanaukulimia, kwa kiasi kikubwa wakulima wengi wanaingia hasara kutokana na kutokujua soko lake, mtu anaenda kulima akishakaribia kuvuna ndio anarudi mezani kaunza kufirikia atamuuzia nani...hapa nashauri kabla hujaenda sokoni plz anza kutafuta soko kwanza ikiwezekana ingia namnunuzi mkataba

4...Jifunze utambue ABC za vanilla, hii itakusaidia kuepusha kudanganjwa

5- Nashaurii ukilima vanilla plz panda kwenye shamba lako mwenyewe, mche wa vanilla unaweza dumu mpaka miaka 40 ukiangaliwa na kuhudiumiwa vizuri

Hitimisho

Mimi nalima vanila kwa mkataba ( contract farming), mapato yake sio kama yanavyotangazwa na hawa wajasiriamali. ninaliama na kampuni ya .....Natural Extracts Industries Ltd...hawa ndio wanaonunua, na wananipa huduma za ugani

Muwe na kilimo chema
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,217
2,000
MOTIVESHENI SUPIKAZ 😅😅

Vanilla uchavushaji inampasa binadamu mkulima kukesha mashambani akihamisha pollens kwenye maua from male to female parts,

Pia huwezi kulima kwenye open space kazi na kuwe na kivuli n.k
Ni changamoto na huvunwa inapokuwa inakauka kuelekea kuharibika, ili iwe ya kiwango cha quality nzuri.

Wengi hapo kwenye uchavushaji ni tatizo pia hali ya hewa, usipochavusha hakuna mavuno ya vanilla.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
34,746
2,000
Nilimsikia baba levo akipiga porojo kuhusu hio vannila ila kwa spana nilizopigwa mashambani hamna jinsi utanishauri nilime!
Watu walime mie ntanunua tu kisha niuze katika soko langu nalojua mimi!
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,791
2,000
MOTIVESHENI SUPIKAZ

Vanilla uchavushaji inampasa binadamu mkulima kukesha mashambani akihamisha pollens kwenye maua from male to female parts,

Pia huwezi kulima kwenye open space kazi na kuwe na kivuli n.k
Ni changamoto na huvunwa inapokuwa inakauka kuelekea kuharibika, ili iwe ya kiwango cha quality nzuri.

Wengi hapo kwenye uchavushaji ni tatizo pia hali ya hewa, usipochavusha hakuna mavuno ya vanilla.

Everyday is Saturday...............................

Unaielewa vizuri sana hili zao
Bora umetoa darasa la pollination
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,217
2,000
Nilimsikia baba levo akipiga porojo kuhusu hio vannila ila kwa spana nilizopigwa mashambani hamna jinsi utanishauri nilime!
Watu walime mie ntanunua tu kisha niuze katika soko langu nalojua mimi!
Wezi hao, swagga nyingi, hawaongelei ugumu wa kuchavusha, iwe jua iwe mvua, hizo siku za kupata mimba maua usipochavusha basi, usubirie msimu ujao,
Na bei wanazokuja nazo ni uongo mtupu.
Wanaandika bei ya vanilla iliyokuwa graded highest quality huko ulaya na siyo shambani Matombo huko.

Hawana tofauti na Namaingo, Kijani kibichi n.k

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
34,746
2,000
Wezi hao, swagga nyingi, hawaongelei ugumu wa kuchavusha, iwe jua iwe mvua, hizo siku za kupata mimba maua usipochavusha basi, usubirie msimu ujao,
Na bei wanazokuja nazo ni uongo mtupu.
Wanaandika bei ya vanilla iliyokuwa graded highest quality huko ulaya na siyo shambani Matombo huko.

Hawana tofauti na Namaingo, Kijani kibichi n.k

Everyday is Saturday............................... :cool:
Wale wa kupenda hesabu za kwenye makaratasi wataingia 18% na watabutuliwa kama kawaida
 
Uncle Lou

JF-Expert Member
May 22, 2016
905
1,000
MOTIVESHENI SUPIKAZ

Vanilla uchavushaji inampasa binadamu mkulima kukesha mashambani akihamisha pollens kwenye maua from male to female parts,

Pia huwezi kulima kwenye open space kazi na kuwe na kivuli n.k
Ni changamoto na huvunwa inapokuwa inakauka kuelekea kuharibika, ili iwe ya kiwango cha quality nzuri.

Wengi hapo kwenye uchavushaji ni tatizo pia hali ya hewa, usipochavusha hakuna mavuno ya vanilla.

Everyday is Saturday...............................

Machame, Kilimanjaro zinalimwa kwenye open space.
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,217
2,000
Wale wa kupenda hesabu za kwenye makaratasi wataingia 18% na watabutuliwa kama kawaida
😅 Kilimo cha WhatsApp, ngoja wauziwe marando ya vanilla, wakifikiria hicho sawa na kilimo cha tembele Kibaha au manumbu Gairo.

Tusubirie mirejesho ya wakurupukaji!

Everyday is Saturday................................:cool:
 
Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,969
2,000
Huyu jamaa wa Vanila international ni tapeli though ni mzur katika marketing. Kabla ya hapo alikuwa na kampuni anaiita greenhouseinteenational.ltd.

Sasa hivi kaja na mbinu nyingine. Jamaa ni opportunist mzuri sana.
Screenshot_20210421-081428_Instagram.jpg
 
DASM

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
1,786
2,000
Salama wanajamvi , sitaki kuandika mengi sana ila wakulima wa nchi hii wanapitia mengi sana magumu hasa kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi na utaalamu , basi ngoja niwaletee stori ambayo nimeitoa kwenye group Moja la WhatsApp kuhusu kilimo cha Vanilla je ni kweli? Kila mmoja adondoshe comment yake Ili tupate maarifa , naanza na hawa jamaa wa Vanilla international huwa nawasikia sana

C&P
VANILLA INTERNATIONAL LIMITED
napenda kukualika KWENYE kilimo Cha Hela nyingi Cha ZAO LA VANILLA. Wekeza pesa kwa ili tukusaidie kukujengea Banda kitalu yaani SHAMBA kitalu (GREENHOUSE) kwa ajili ya KUKUPANDIA marando ya VANILLA ambayo ndilo zao namba moja kwa kuzaa sana na kwa kuwa na BEI KUBWA KWA KILO MOJA. Wastani wa BEI YA VANILLA NI TZS 1,500,000/=

MATARAJIO YA MAVUNO YA VANILLA:
Mche mmoja wa VANILLA INAZAA matawi 10 kwa mwaka na kampuni ya VANILLA INTERNATIONAL LIMITED inanunua matawi(marando) kwa Tzs 20,000/= kwa kila random(#VANILLACUTTINGS).
Hii Ina maana kuwa mche mmoja wa VANILLA utakuzalishia Tzs 200,000/= kwa kila MWAKA KWA KUUZA MARANDO TU(#VANILLACUTTINGS). Kwa hiyo ukiwa na Miche 100 itakuzalishia Tzs Milioni 20 kwa KUUZA MARANDO YA VANILLA (#VANILLACUTTINGS).

VANILLA BEANS (MAHARAGE YA BANILLA):
Mche mmoja wa VANILLA UNAZAA kilo 15 kwa wastani na Bei ya Vanilla mbichi kwa kilo ni TZS 220,000/= na hivyo kukupatia mpaka Tzs 3,000,000/= kwa mche mmoja. Kwa KIFUPI ZAO LA VANILLA LINA PESA KULIKO MRADI WOWOTE WA KILIMO. I MEAN VANILLA HAIFANANI NA MAHINDI, KAHAWA, KUNDE, PARACHICHI,MITI, MAHARAGE, VIAZI, STRAWBERRY, NDIZI WALA MPUNGA KAMA ULE MRADI WA MASANJA MKANDAMIZAJI.

MAADA itaendelea hivi karibuni.
Ila waweza kupata baadhi ya GHARAMA ZA GREENHOUSES ZA VANILLA:
UKUBWA (SQM). ..... BEI(000,000/=)
40. 3
72. 4
120. 6.2
200. 8.7
300. 12
400. 18
600. . 22
800 . 25
ROBO HEKA . 33
NUSU HEKA . 56
HEKA. 87
HEKA 2. 140
HEKA 4. 200.

(Negotiable).
Nb: LAZIMA UWE NA MTAJI
Mkoa gani vanilla inastawi
 
AbouZakariya

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
1,181
2,000
Pesa haziji kirahisj hivyo,yaani umeweka mbupu juu tu uletewe maarifa.
Kaka punguza hasira, kama una taarifa njoo nambie mahitaji yako nikimudu utanipatia elimu, kama sitoweza si basi kaka, hakuna sababu ya hasira na povu jiiiingi bila sababu, kwa umri wangu nafahamu hakuna elimu bure.
Punguza hasira.
 
Lasway.Jr

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
229
500
Mkuu,
Msije mkaingia kichwa kichwa,mambo sio marahisi hivyo, Mosi Taarifa VANILLA INTERNATIONAL LIMITED kwa kiasi kikubwa sio kweli, Marando ya vanilla bei yake sio 20,000= bei yake ina range kati ya 3000 mpaka 5000

Bei ya vanilla duniani mara nyingi inapanda na kushuka na hii inategemea hali ya soko la Madagascar ambao ni waalishaji wakubwa duniani...kwahiyo mwaka huu inawea ikawa kubwa mwaka ujao ikawa ndogo, tangu nianze kulima vanilla sijawahi na wala sijui kama ntakaa niue kilo moja beans kwaaidi ya TSH Milioni kama wanavyotangaa

Ushauri wangu...kilimo cha vanilla sio kibaya ila kabla ya kuingia tambua

1- Ni labor intensive , uchavushaji wa vanilla unatumia mikono

2-WeZi; kwa maeneo hususan ya kagera na baadhi ya maeneo ya kilimanjaro kipindi cha mavuno kunakuwa na wii mkubwa saana

3- Jua soko lko au soko la hao wanaukulimia, kwa kiasi kikubwa wakulima wengi wanaingia hasara kutokana na kutokujua soko lake, mtu anaenda kulima akishakaribia kuvuna ndio anarudi mezani kaunza kufirikia atamuuzia nani...hapa nashauri kabla hujaenda sokoni plz anza kutafuta soko kwanza ikiwezekana ingia namnunuzi mkataba

4...Jifunze utambue ABC za vanilla, hii itakusaidia kuepusha kudanganjwa

5- Nashaurii ukilima vanilla plz panda kwenye shamba lako mwenyewe, mche wa vanilla unaweza dumu mpaka miaka 40 ukiangaliwa na kuhudiumiwa vizuri

Hitimisho

Mimi nalima vanila kwa mkataba ( contract farming), mapato yake sio kama yanavyotangazwa na hawa wajasiriamali. ninaliama na kampuni ya .....Natural Extracts Industries Ltd...hawa ndio wanaonunua, na wananipa huduma za ugani

Muwe na kilimo chema
Umeeleza vyema sana mtaalamu , lengo langu lilikuwa watu kujua , hii naona ni aina mpya ya upigaji tuu hakuna msaada wowote kwa mkulima
 
Lasway.Jr

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
229
500
Huyu jamaa wa Vanila international ni tapeli though ni mzur katika marketing. Kabla ya hapo alikuwa na kampuni anaiita greenhouseinteenational.ltd.

Sasa hivi kaja na mbinu nyingine. Jamaa ni opportunist mzuri sana. View attachment 1758946
Hiyo green house international iliishia wapi mzee niliisikia sana pia , walikuwa wanasema Wana soko kubwa Comoro
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom