Kilimo cha Starawbery na Cape gooseberry

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,902
Mbali na maswala ya Ufugaji kwa sasa pia tunajishughulisha na Kilimo cha matunda hasa Strawberry na Cape gooseberry.

Strawberry ni matunda yenye thamani sana na mara nyingi huliwa au kutumiwa na watu wa Daraja la kati.

Matumizi ya Haya matunda.

1. Juice-Haya ndo matumizi makubwa kwa Mahoteli na majumbani.

2. Ice cream- Pia hapa matumizi yake ni makubwa kwa mahoteli na Migahawa mikubwa.

3.Fresh-Kuliwa fresh hapa ni sawa na Juice.

4. Jam-Hapa inahitajika uwekezaji makubwa kidogo kuweza kuzalisha Jam.

5. Yogurt- Matumizi makubwa kabisa kuliko yote yako hapa. Na viwanda vinazo zalisha Yogurt kwa Tanzania vinalazimika kutumia Flavour kutoka nje ya nchi kutokana na supply kuwa ndogo hapa Tanzania.

6. Manukato- Pia matumizi yake ni makubwa sana.

7.Keki Decoration na kutengenezea mikate hapa matumizi yake sio makubwa sana.

Hivyo utaona kwamba matumizi yake yako nyanja nyingi sana.

Viwanda cya maziwa huwa vinaogopa kununua Matunda kwa sababu hawana uhakila na supply.

Hivyo viwanda karibia vyote vinatumia flavour kutoka nje.

Matumizi sasa yanabakia kwenye vitu kama Ice cream, Juice, keki na kadhalika.

Kwenye Jam nako tatizo linakuja kwenye Supply kiwa hafifu na kwa Tanzania hatuna kiwanda kinazalisha Jam ya Starwberry.

Hivyo ukitaka kuwekeza kwenye Kilimo kama hiki Target vitu kama Jam au Yogurt.

Soko lake kwa Tanzania.

Watu wengi sana wanajua au wanaisikia Starwberry ila hawajawahi kula haya matunda.

Hata humu mnao soma wengi hamjawahi kuyala haya Matunda ingawa mnayasikia tu.

KWA NINI?

Bei yake ndo inafanya watu wasiweze kuyala haya matunda kumbe sasa unaweza zalisha na kuuza kwa bei ambayo hata kada ya chini watamudu kununua na kula.

Pia Supply yake ni ndogo sana ndo maana watu wengi hawawezi yanunua au kuyapata.

Pia kasumba kwamba ni matunda ya watu wenye pesa kumbe sio.


Yanalimwa Kanda zote isipokuwa maeneo yenye joto kari kama Dar au Zanzibar Tanga baaadhi ya Wilaya yanalimwa.

MATUNZO.

Haya matunda uwe na maji sio maji ya Mungu bali maji ya uhakika.na kama huna maji basi usilime.

Yanapenda sana maji hivyo maji ni muhimu sana.

Udongo wa tifutifu na hata mfinyanzi yana stawi isipo kuwa kichanga.

Mbolea ya Samadi inafaa sana na hayapende mbolea za viwandani.

Dawa- Haya pigwi kabisa dawa.

MAVUNO

Baada ya miezi mitatu hadi minne tangu kupandwa ndo mavuno huanza.

MAISHA YAKE.

Miaka mitatu.

AINA
Kuna aina 60 za Starwberry.

Kwa Tanzania ni Chandrlie ndo inafanya vyema kabisa.


CAPE GOOSEBERRY

Haya ni aina ya pili ya matunda ambayo yana matumizi sawa kabisa na Starwberry na yanafanana kwa kila kitu isipo kuwa haya unaweza yalima hata kwenye Joto kari kama Dar na Zanzibar

MBUGU ZA STARAWBERRY.

Starawberry huoteshwa kwa kutunia mbegu na pia miche.

Ila utumiaji wa mbegu ni mgumu sana na zinachukua muda mrefu dana kugerminate na kuku na hivyo optiobal ya miche kuwa ndo bora zaidi.

Miche hupatikana kwa ku proone maotea. Strawberry hutoa maotea kama ili Migomba na hiyo ndo huwa inakuwa miche tena.

Huwa ukuaji wake unafanana na Mgomba hasa kwenye kutoa watoto pembeni ya mama

.
20180704_100855.jpg
FB_IMG_1530605490427.jpg
IMG_1530385129408.jpg
 
Mbona post yako imeishia hewani?
Mbegu zinapatikana wapi?
Umesema yanastawi sehemu zenye baridi Halafu mwisho unaweka picha ya zinazostawi Zanzibar Na Dar!
Hizo za kwenye baridi zikoje?
Picha ya zinazo stawi Zanzibar ni Ipi? Naomba utoe kabisa na maelezo kwamba ni Zanzibar
 
Mbona post yako imeishia hewani?
Mbegu zinapatikana wapi?
Umesema yanastawi sehemu zenye baridi Halafu mwisho unaweka picha ya zinazostawi Zanzibar Na Dar!
Hizo za kwenye baridi zikoje?
Kama hujaelewa kitu Uliza na sio kujubu kwa unavyo waza wewe.
 
mm mwenyewe sijawahi kuyakala kabisa naona ni mazuri sana
je sehemu za joto yaweza kulimwa haya matunda?
 
Hayo matunda nimekula sana Chunya-Mbeya ila sikuwa na interest kujua thamani yake sokoni!..
 
dah mkuu yaani mavuno yanaanza baada ya miaka mitatu maana umesema yanachukua miaka mitatu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom