Kilimo cha Pilipili Hoho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo cha Pilipili Hoho

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Neanne, Oct 7, 2013.

 1. Neanne

  Neanne Member

  #1
  Oct 7, 2013
  Joined: Apr 23, 2013
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari wana waungwana? Naomba muongozo wa kilimo cha pilipili hoho kwa wenye uzoefu.

  Asanteni

  ===============================

   
 2. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2013
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,190
  Likes Received: 2,190
  Trophy Points: 280
  KILIMO BORA CHA PILIPILI HOHO

  Jina la kitalaamu la PILI PILI HOHO ni Capsicum annum. Asili ya zao hili ni bara la Amerika ya Kusini. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Iringa, Tanga (Lushoto), Mbeya, Ruvuma, Tabora na Arusha. Kilimo hiki kinaendeshwa na wakulima wadogo katika maeneo yenye ukubwa wa kati ya hekta 0.2-0.4 pia kuna maeneo ya wakulima wakubwa wenye hekta kati ya 2-20. Wakulima hao hujishughulisha na kilimo cha zao hilo kwa njia ya mkataba na kampuni hiyo.

  Hoho hutumika katika kutengeneza rangi za asili za vyakula ambazo kwa sasa hupendwa zaidi kuliko zile zinazotokana na kemikali na pia huongeza ladha na harufu katika vyakula. Hivyo hutumika katika viwanda vya kusindika vyakula, kwa mapishi ya nyumbani na hata katika viwanda vya vipodozi kama rangi ya mdomo, uso n.k. Ina virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kama madini ya chuma, vitamin A na C.

  [​IMG]


  2.0 TABIA YA MMEA
  Hoho ni zao la jamii ya pilipili isiyo kali, tunda lake ni nene kiasi la duara pia linaweza kuwa lililochongoka,.

  3.0 ENEO NA HALI YA HEWA INAYOFAA KWA KILIMO
  Hoho hustawi vema katika maeneo ya usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 2,000 yenye mvua ya wastani wa mm.600-1,250 na wastani wa joto la nyuzi za sentigredi 21 hadi 24. Udongo wa tifitifu wenye rutuba, usiotuamisha maji na wenye hali ya uchachu (pH) kati ya 5.0-6.5 hufaa zaidi. Umwagiliaji ni muhimu pale mvua inapokuwa chache.

  4.0 UZALISHAJI
  4.1 UTAYARISHAJI WA KITALU

  Chagua eneo katika ardhi isiyo na mtelemko mkali na yenye rutuba ya kutosha. Ardhi iwe imepumzishwa bila kuoteshwa mazao ya jamii ya pilipili, biringanya, nyanya, n.k. ili kuepukana na mashambulizi ya wadudu na magonjwa.
  Tayarisha kitalu kabla ya msimu wa mvua. Andaa vizuri matuta manne yenye urefu wa wastani wa mita 10 kila moja na upana wa mita moja (1) ili kustawisha miche inayotosha ekari moja.

  Acha njia ya nusu mita kati ya tuta na tuta. Mwagilia maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu na endelea kunyweshea kulingana na hali ya hewa na hali ya udongo. Sia mbegu kwenye, mstari, nafasi kati ya mstari na mstari ni sm 10 na kina cha sm1. Kiasi cha mbegu cha nusu kilo kinatosha eneo la hekta moja. Weka matandazo kwenye kitalu au tumia nailoni nyeusi ili kuhifadhi unyevunyevu na kuzuia uotaji wa magugu.

  4.2 UTAYARISHAJI WA SHAMBA

  Shamba lilimwe vizuri na kuweka matuta ili kuhifadhi unyevunyevu na kurahisisha umwagiliaji. Matuta yanaweza kuwa makubwa au madogo kulingana na matakwa ya mkulima. Matuta makubwa hupandwa mistari miwili na matuta madogo hupandwa mstari mmoja.

  [​IMG]


  4.3 UPATIKANAJI WA MBEGU

  Mbegu ambazo hutumika ni chotara ambazo huuzwa kwenye maduka ya pembejeo za kilimo nchi nzima. Haishauriwi kutumia mbegu kutoka zao la msimu uliopita kwani ubora wa paprika utaharibika na hivyo kuharibu soko unashauriwa kununua mbegu bora.

  4.4 UPANDAJI
  Mbegu huoteshwa na kukuzwa kitaluni kwa muda wa wiki 6-8 na miche hupandikizwa shambani ikiwa na urefu wa sm.6-10. Mwagilia maji kitaluni kabla ya kuhamisha miche. Panda shambani kwa nafasi ya sm.75-90 kati ya miche kwa sm.90-105 kati ya mistari, wastani wa miche 12,500 itapatikana kwa hekta. Weka samadi shambani tani 25-37 kwa hekta wiki 1-2 kabla ya kupandikiza miche, au kilo 560-670 za NPK (mbolea ya viwandani) kwa hekta kwa uwiano wa 4:7:7 katika udongo usio na rutuba ya kutosha.

  ITALIAN PAPRIKA
  [​IMG]


  5.0 KUHUDUMIA SHAMBA
  Palizi ifanyike mara magugu yanapotokea shambani. Umwagiliaji maji ufanyike kama ilivyo kwa mazao mengine kama nyanya. Tumia mbolea kiasi cha kilo 140 za SA au CAN kwa hekta hasa wakati mmea inapotoa matunda ili kupata matunda makubwa na kuvuna kwa muda mrefu (hadi miezi 10).

  6.0 MAGONJWA NA WADUDU


  Wadudu
  • Funza wa vitumba
  • Vidukari
  • Kidomozi (Leaf miner)

  Kudhibiti: Tumia dawa aina ya permethrin
  Magonjwa
  • Kuoza mizizi
  • Mnyauko wa majani
  • Batobato
  Kudhibiti: Choma nyasi kwenye kitalu kabla ya kusia mbegu.
  Badilisha mazao yasiyo ya jamii ya pilipili.

  7.0 UVUNAJI
  Matunda ya kwanza huwa tayari kuvunwa kuanzia miezi 2-3 baada ya kupandikizwa; matunda yaliyokomaa vizuri na kuwa na rangi nyekundu ndiyo huvunwa. Matunda 30-80 hupatikana kwa mmea mmoja.

  Ubora wa hoho huongezeka kutegemeana na kiwango cha rangi yake ikiwa ni nyekundu njano au kijani. Mazao kiasi cha tani 3.5 kwa hekta hupatikana. Baada ya kuvuna mwagilia maji, piga dawa (kama ni muhimu) na weka mbolea kuongeza uzalishaji unaofuata.

  8.0 USINDIKAJI

  Hoho huuzwa ikiwa bado fresh tofauti na jamii nyingine za pilipili ambazo zinaweza kukaushwa na kusindikwa kasha kuuzwa baadae.


  [​IMG]


  9.0 SOKO LA PAPRIKA
  Soko la hoho lipo nchi nzima kwenya masoko makubwa na hata magengeni, hoho hutumiwa zaidi kama kiungo cha kupikia mapishi mbali mbali au kutia kwenye kachumbari. Tatizo kubwa wanalokabiliana nalo wakulima ni kutokuwa na soko la uhakika ndani na nje ya nchi, mazao huweza kuoza shambani au njiani kutokana na tabu ya usafiri hasa vijijini ambapo mvua zikinyesha barabara hazipitiki kwa urahisi

  Kuna aina ya pilipili isiyo kali kama hoho lakini ni ndefu kama pilipili za kawaida ijulikanayo kama PAPRIKA ambayo ina soko kubwa nje ya nchi. Zao hili kwa sasa huzalishwa kwa msukumo wa kampuni ya kigeni ya Hispania inayoitwa Tanzania Spices Ltd iliyopo mkoani Iringa

  [​IMG]

  10.0 GHARAMA YA UZALISHAJI WA HEKTA MOJA:

  Mbegu Tshs. 24,000 /-
  Vibarua 200,000/-
  Mbolea(mboji/samadi) 300,000/-
  Madawa 100,000/-
  Jumla 624,000/-

  MAPATO:
  Kilo 3,500/- X 800/- 2,800,000/-
   
 3. GKM

  GKM JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2014
  Joined: Dec 5, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Wakuu nawasalimu sana, please naomba aliewahi kufanya hiki kilimo anisaidie nijue A-Z yake, mchakato mzima wa kukifanya, risk zake, mauzo/soko, mapato nk. Natanguliza shukrani za dhati.
   
 4. w

  wise-comedian JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2014
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,372
  Likes Received: 2,422
  Trophy Points: 280
  Eagerly waiting for the reply......utakaetoa somo usisahau kuweka gharama kwa ekari,aina ya udongo znapositawi vizur,mahitaj ya madawa,mambo muhimu ya kuzngatia tokea mche ukiwa kitaluni,mapato kwa ekari iliyotunzwa vizur na mwisho kabsa bei yake sokon kwa ujazo wa kiasi fulani.
   
 5. GKM

  GKM JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2014
  Joined: Dec 5, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Asante kwa kufafanua zaidi, naendelea kusubiri majibu.
   
 6. GKM

  GKM JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2014
  Joined: Dec 5, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mkuu nashukuru sana, nimekupata vilivyo
   
 7. baraka607

  baraka607 JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2014
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 852
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Safi sana. Kila la kheri.
   
 8. concrete15

  concrete15 JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2014
  Joined: Oct 16, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 33
  Thanks sana kaka hii kitu swafi sana maelezo nimeyakubali. Embu tupe mchanganuo wa kitunguu na dawa zake kuanzia kupanda mpaka kuvuna .Inaelekea uko vizuri sana kwenye agriculture wengine tumevamia fan mradi ni biashara
   
 9. w

  wise-comedian JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2014
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,372
  Likes Received: 2,422
  Trophy Points: 280
  ndugu baraka unaweza kushare nasi mahali unapolimia,soko lako unalipatia wap au wanunuzi wakubwa wako wap,kipindi cha mwaka ambapo bei inakuwa nzuri,uzoefu wako na mapato kwa ekari pamoja na ufungaji wa bidhaa kwenda sokoni
   
 10. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2015
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wanaukumbi

  Naomba mawazo yenu nipo najiandaa kulima PILIPILI HOHO maeneo ya kigamboni katika OPEN FIELD heka 1 natumia umwagiliaji wa drip

  Naomba msaada wa soko la pilipili hoho pamoja na mbegu ambayo inafaa kwa kilimo hiki
   
 11. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2015
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naomba msaada wanaJF
   
 12. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2015
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. m

  masanzu JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2016
  Joined: May 6, 2013
  Messages: 494
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  Mkuu hili zao mimi nalima tena sana tu kwnza kwa hiyo bajeti aliyoiweka ni ndogo sana mbegu tu kama unapanda mbegu chotara mf tycoon kwa hk 1 ni sh 250000 kukodisha shamba inategemea kiwango cha chini kbs ni 100000 kulimwa trekta tsh45000 kupiga halo tsh 40000 kulima matuta tsh 80000 mbolea ya kupandia kg100 =140000 vibarua wa kupanda tsh 50000 madawa ukungu+sumu=250000 mbolea kuumwa kg100 =tsh120000 mbolea kuzalishia kg100 =100000 ghalama za umwagiliaji namaanisha petrol tsh120000 palizi tsh100000 boy shamba tsh200000 ziada tsh 200000 soko inategemea na msimu kunakipindi gunia mmoja ni 80000-150000 kwa hk moja ukiitunza vizuri wastani wa maroba 20-30 kwa wiki pilipili hoho inavunwa kwa wastani wa miezi 3-6 inategemea na hali ya hewa
   
 14. MLIPAKODI

  MLIPAKODI JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2016
  Joined: Dec 11, 2012
  Messages: 240
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Good
   
 15. Atukilia

  Atukilia JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2016
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 643
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ahsante mkuu were unalima wapi? mimi nataka kuanza kufanya hiki kilimo dar
   
 16. LOGORIDDIM

  LOGORIDDIM JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2016
  Joined: Jan 25, 2013
  Messages: 2,429
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Asanteni kwa elimu
   
 17. dre4691

  dre4691 JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2016
  Joined: Feb 22, 2016
  Messages: 487
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 80
  Sio soko tu hoho hailimwi kwenye jua kali kuna kitu kinaitwa jua kali na hoho havipatani kabisa hakikisha shm haina mionzi ya jua manake kigambon kule si jua kama Dar , ushauri tu

  Sio soko tu hoho hailimwi kwenye jua kali kuna kitu kinaitwa jua kali na hoho havipatani kabisa hakikisha shm haina mionzi ya jua manake kigambon kule si jua kama Dar , ushauri tu
   
 18. Macky

  Macky Member

  #18
  Mar 19, 2016
  Joined: Mar 8, 2016
  Messages: 48
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 25
 19. heradius12

  heradius12 JF-Expert Member

  #19
  Apr 17, 2016
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 6,684
  Likes Received: 8,243
  Trophy Points: 280
  Hoho inahtaji jua. Cha muhimu ni maji maji maji....
   
 20. heradius12

  heradius12 JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2016
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 6,684
  Likes Received: 8,243
  Trophy Points: 280
  Ninaplani ua kupanda miche ya hoho 15000 hadi 20000. Mkuu naomba ushaur wako interms ya mbegu na masoko pia. Ninaandaa eneo lenye ukubwa wa 7000m2. Hili eneo halijawai limwa zaidi ya miaka 30. Nilijaribu kulima kama miche 300 aina ya calfonia wonder na ziliota vizur bila kutumia mbolea za dukani na hta hazikushambuliwa na magonjwa. Yani sikuweka chemical ya aina yoyote. Mavuno yalikuwa mengi sasa imenihamasisha kulima on a large scale.
   
Loading...