Kilimo cha Parachichi - Fahamu Aina, Namna ya Kulima na Masoko

Nina kashamba kangu Gairo pale, sjui parachichi itakubali...
Wataalam msaada tafadhali
 
Watu wanauliza juu ya maeneo gani yanafaa parachichi.Maenei yote yenye baridi kuanzia Mbeya, Iringa, Njombe, Moshi Arusha na Kagera. Maeneo mengine ni Kigoma Manyovu, Rukwa, Songwe. Maeneo yote ya miinuko kuanzia mita 1000-2500. Hivyo milima Uluguru, Usambara, Meru, Rungwe nk parachichi itakubali ila zingatia soill ph. Parachichi haikubali kwenye mchanga.
 
Kama kuna mtu anategemea kupanda parachichi mwaka huu Wilaya ya Kilolo,
Basi tuwasiliane, tutakuletea seedlings mpaka shambani kwako, price yetu ni 2500/- kwa mchi,
Ni PM
Dar vipi parachichi hazioti au?
 
Parachichi inayofanya vyema ni Hass sokoni na inayofanya vyema zaidi ni inayokomaa mwezi November hadi March. Kipindi hiki wazalishaji wakubwa wanakuwa hawana mzigo. Mzalishaji anaechelewa ni Israel yeye anaishiwa mzigo mwezi January.

Hivy ukiwa ukanda wa Busokelo na lupembe maeneo ya Mfriga, Madeke, Mfriga, Iduli , ikondo una uhakika wa kukutana na soko la ukahakika.

Uzoefu unaonyesha parachichi mwaka wa tatu utakupatia matunda 40 had 60 ambapo utapata kilo 10 hadi 15.

Kingine cha kuzingatia mbegu bora ya parachichi inatakiwa itokane na kikonyo cha mti ambao ni kizazi kisichozidi cha nne, hapa utapata size na shape nzuri ya Hass. Kununua mche ambao kikonyo kimetoka kizazi cha mbali ni hasara kwako matunda yataanza kutoa yasio na shape halis ya hass.
 
Dar vipi parachichi hazioti au?
Zinaota ila haizai nimewahi uona mti kwa jirani.Parachichi haipendi joto kali na udongo wa kichanga.baadhi ya maeneo moro inaweza ota. Nimeeleza maeneo yanayofaa parachichi hapo juu. Kama unataka kupanda zipo kampuni zinasimamia mashamba mnaingia mkataba hata kama upo Dar.
 
Zinaota ila haizai nimewahi uona mti kwa jirani.Parachichi haipendi joto kali na udongo wa kichanga.baadhi ya maeneo moro inaweza ota.nimeeleza maeneo yanayofaa parachichi hapo juu.kama unataka kupanda zipo kampuni zinasimamia mashamba mnaingia mkataba hata kama upo dar.
Mkuu parachichi inaweza kubali hali ya hewa ya Kiteto?
 
Wakuu kilimo cha parachichi aina ya hass kwa sasa kinachukua umaarufu hasa kwa mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa, Arusha, Songea na kwingineko.

Mwenye kujua masoko yake hasa nje ya nchi na makampuni yanayonunua tujuzane please
Hii vita vya kiuchumi kati ya Marekani na China huenda ikaathiri soko la parachichi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom