Kilimo cha Parachichi - Fahamu Aina, Namna ya Kulima na Masoko

80% ya parachichi zinatoka Kilimanjaro hata Arusha wanatoa Moshi - Dar msimu wake hutokea Kilimanjaro, msimu ukiisha yanaenda fatwa Burundi na mnufaikaji mkubwa sio mkulima ni mtu wa kati na hata ukipanda miti 20 leo hadi ije kuzaa na hata ikizaa siokuja kukupa pensheni mzee.

Gunia la parachichi za Rombo baada ya kufika Dar ni 60,000 hadi 75,000 inategemea na msimu. Sasa kula hesabu gharama ya kutoa shamba hadi Dar na anaeleta Dar ananunua sokoni kwa anaetoa shamba. Kuna za Machame sasa ambazo ndio zinafanana na za Mbeya izo kuiva ni siku 1 tu ukijitekenya zinaivia njiani zinaharibika, ndio maana kuzitoa Mbeya ni jau sana na sio nzuri kama za Rombo na gunia lake ni 45000-50000 zikifika Dar. Sasa jiulize unazopanda ni zipi, Je, zitakupa pensheni?

tembajr,
Ndugu ina inaitwa HASS inaweza kukaa hata mwezi ukichuma ikiwa imekomaa bila kuoza ni kama zile embe za bolibo. na hizi nying husafirishwa nje na hapa jamaa anazungumzia kampuni ya kuuza nje.

Iko kampuni moja inaitwa AFRICADO iko kilimanjaro wanasafirisha sana parachichi kwenda Uyala.

LUMUMBA
 
HABARI,
@tembajr,

Ndugu ina inaitwa HASS inaweza kukaa hata mwezi ukichuma ikiwa imekomaa bila kuoza ni kama zile embe za bolibo. na hizi nying husafirishwa nje na hapa jamaa anazungumzia kampuni ya kuuza nje.

Iko kampuni moja inaitwa AFRICADO iko kilimanjaro wanasafirisha sana parachichi kwenda Ulaya.

LUMUMBA
Katika uelewa wa parachichi sijawahi jua hili mkuu asante kwa kunijuza. Hizi hass huwa ukizivundika kuziivisha kilazima zinaaribika? Mana nimewahi kukutana na parachichi zinazogoma kuiva tunaziweka hata siku 7 bado mbichi hii kwetu ilikuwaga ni pasua kichwa
 
Katika uelewa wa parachichi sijawahi jua hili mkuu asante kwa kunijuza. Hizi hass huwa ukizivundika kuziivisha kilazima zinaaribika? Mana nimewahi kukutana na parachichi zinazogoma kuiva tunaziweka hata siku 7 bado mbichi hii kwetu ilikuwaga ni pasua kichwa
HABARI. Asante Pia,

Aina hii sa HASS asili yake ni america kusini hasa Nchi ya MEXICO ambayo ndio nchi inayolima na kuuza Parachichi kwa wingi duniani soko kubwa likiwa marekani.Wakulima wa marekani walitoa mbegu kule miaka ya 1800 mishoni ndio wakaanza kulima waligungua ni mbegu nzuri isiyo haribika kwa haraka rahisi kuihifadhi na kushafirisha na kitu kinachosaodia hapa ni ganda lake kuwa ni gumu sasa kama ukichuma ikiwa imekomaa inaweza kuiva ndani ila ikachelewa kuoza kwasabau ya ganda lake.

Sasa hiyo aina ya huko kwenu inawezekana ikawa ni mbegu nyingine ambayo haijatambuliwa kimataifa ikawa ni fursa pia.

LUMUMBA
 
HABARI. Asante Pia,

Aina hii sa HASS asili yake ni america kusini hasa Nchi ya MEXICO ambayo ndio nchi inayolima na kuuza Parachichi kwa wingi duniani soko kubwa likiwa marekani.Wakulima wa marekani walitoa mbegu kule miaka ya 1800 mishoni ndio wakaanza kulima waligungua ni mbegu nzuri isiyo haribika kwa haraka rahisi kuihifadhi na kushafirisha na kitu kinachosaodia hapa ni ganda lake kuwa ni gumu sasa kama ukichuma ikiwa imekomaa inaweza kuiva ndani ila ikachelewa kuoza kwasabau ya ganda lake.

Sasa hiyo aina ya huko kwenu inawezekana ikawa ni mbegu nyingine ambayo haijatambuliwa kimataifa ikawa ni fursa pia.

LUMUMBA
Uko vizuri mkuu. Nikijipanga nitakutafuta tuyajenge katika hili.
 
Katavi sio maeneo salama kwa parachichi mkuu kwa namna nilivo izunguka japo inaweza kustawi lakini haitaweza kukidhi viwango stahiki vinavyotakiwa katika soko la kimataifa na hata la ndani. Katavi ardhi yake ni kichanga na hali ya hewa ni joto zaidi kama sikosei wakati huo parachichi inataka sehemu ya tifutifu zaidi na mfinyanzi napo panafaa, hali nzuri ya hewa na maji ya kutosha.

Kwa Sumbawanga ukipata eneo itakuwa vizuri zaidi au Nkasi.

Ukifanya na taratibu za kujiunga na ushirika wa UWAMARU itakuwa jambo la kheri zaidi sababu hata pindi wakati wa mavuno ukianza itakuwa rahisi kuunganishwa na wanunuzi. Jambo la msingi kuhamasisha na wengine wengi zaidi ili hata mnunuzi anapo toka Mbeya kuja Rukwa asije kwaajili ya 1tone.

Wanunuzi wapo wengi tu ila niutayari wako kuchangamkia fursa na tunavoendelea mbele zaidi wanazidiongezeka sababu ya ujio wa ndege ya mizigo kuanza kutua Songwe International Airport ndani ya mwaka huu kulingana na maelezo ya Waziri Mwenye dhamana.
Geita mji je parachichi zinaweza kukubali?
 
Karibuni jamani kuwekeza kwenye parachichi; cha muhimu usikurupuke. Ni vyema ukapata ushauri wa wataalamu kabla ya kupanda ili usije kujuta baadae ni zao la muda mrefu (perrenial crop) na lina mbinu zake za utunzaji (Good agriculture practices- GAP)
 
Wakuu kilimo cha parachichi aina ya hass kwa sasa kinachukua umaarufu hasa kwa mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa, Arusha, Songea na kwingineko.

Mwenye kujua masoko yake hasa nje ya nchi na makampuni yanayonunua tujuzane please
Songea sehemu gani?
 
aksante mdau naendelea kufuatilia kwa ukaribu inaonekana kilimo hiki kina tija faida yake kama unavyosema ni zaidi ya pension
Ya kisasa ni miaka 3 mpaka 4 unaanza kuvuna...nina experince kutoka Iringa na Njome
 
Kusini hili zao huitwa green gold, wengi wametoka.

So far kuna mpaka viwanda vya usindikaji MBozi na NJombe vimeanza kujengwa. Ukipanda hass which mature at the age of 2.5 to 3 years, mti mmoja hutoa matunda 300 kwa mwaka mpaka 500. UKiwa na miti 70 kwa eka manake una matunda 21,000 sawa na 7000kg. Assume kilo moja ni 1500tshs (bei ya leo Njombe iyo) kwa eka unapata 10.5mil ukiwa na eka kumi sawa na 105mil kwa mwaka ambayo kwa mwezi ni sawa na mapato ya 8.7mil (mshahara wa mkurugenzi huo tena gross nadhani ikija take home lazima alambe 5mil)

Just assume mwaka mbaya ukapata just nusu ya iyo 105mil maisha yanasonga huna haja ya kuajiliwa ni kutafuta mtaji panda parachichi.

Mambo iko uku wahi mashamba Moshi Mbeya na Njombe kuwa na better future yako na ya wanao.
Mkuu aina gani sasa ya parachichi tusije kurupuka na mbegu ambazo hazistahili kuingia sokoni?
 
Karibuni jamani kuwekeza kwenye parachichi cha muhimu usikurupuke ni vyema ukapata ushauri wa wataalamu kabla ya kupanda ili usije kujuta baadae ni zao la muda mrefu ( perrenial crop) na lina mbinu zake za utunzaji ( Good agriculture practices- GAP)
Naomba huo mwongozo ili kufikia kupata zao bora. Maana nataka kuwekeza ktk parachichi
 
Geita ni vyema ukapanda parachichi inaitwa x-ikuli au nabal inavumilia kidogo joto lakn pia unaweza ukajaribu hass maana kuna watu wamepanda hass mwanza.
Wataalamu vp kwa maeneo ya mwanza -usagara kwenda mpaka misungwi naweza panda parachichi na zikasitawi vizuri kwa udongo wa maeneo pia hali ya hewa?
 
Safi sana mkuu, tunda hili ni zuri sana kwa afya.

Mie lazima nile japo moja kila siku asubuhi wakati wa chai pia nzuri kwenye smoothie au chakula chochote kuongezea radha na nutrients/virutubisho.

Ni vizuri wakulima mue mnawaelimisha wananchi faida ya kula matunda na mboga za majani kama njia ya kuongeza soko la bidhaa zenu.

Jamii yetu haina elimu ya kutosha kwenye umuhimu wa kula matunda na mboga za majani.
Personally ahipitis iku bila kugonga parachichi
 
Mbeya kuna mzungu ni mnunuzi, yupo jiran na Rungwe sec

Kama ni Mbeya wala usihofu we lima tu, huyu mzungu kalima eneo kubwa kweli
Anaitwa Mr Robert na last month kazindua kiwanda cha kuchakata parachichi anapack safari Ulaya.
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom