Kilimo cha Parachichi - Fahamu Aina, Namna ya Kulima na Masoko

Nataka nijaribu hii project kwa bidii sana, naangalia ni jamii gani ya parachichi zinaweza kufika sokoni maana hizi oviusly ni mali kuoza.

Nataka nijue production yake ni ya kiasi gani au yield per cultivation over area kwenye jamii itayo tajwa kuwa the best.
Hii project nitaifanyia Kilimanjaro, binafsi nimeona ni kilimo kizuri japo siyo cha muda mfupi kama wengi wanavofikiria kupenda kulima muda mfupi.

Mimi napata changamoto ya kuzalisha Miche tu au kuwa na Miche ya kutosha inavyotakikana maana natarajia kupanda eneo kubwa kidogo ili mavuno yawe ya kutosha niuze kibiashara hata ifike mahali niwapelekee wajomba zangu wakenya japo wao hawana eneo la kulima kibiashara nawaona wakinunua sana na wamenipa hii idea, Sasa nipeni madini na pia nipeni solution mtakayopendekeza ya changamoto yangu ya Miche.

Anayeweza kunitatulia changamoto ya Miche tayari anapata fursa kwangu. Nasubiri ABCD kutoka kwenu.
 
Yale ya kijani yakiiva ndani yanakuwa njano, ukubwa wake unaweza kufika Papai na uzito wa 1/4 kilo yana bei nzuri.
Ni kweli lakini mazuri zaidi kibiashara tunaweza lenga Yale yanayo kaa bila kuiva Mara baada ya kutolewa shambani, pia kumbuka Bei kubwa saa nyingine uhitaji unaeza ukawa kawaida.
 
Mimi mwenyewe ninampango wa kupanda miche 200-400. Mwezi wa pili hapa naandaa kitalu. Hizi mbegu zinaenda kitaluni wiki ijayo, mwezi wa pili, shambani

IMG_20181202_073229.jpg
 
Panda mbegu moja inaitwa Hass. Kwanza ndo parachichi tamu zaidi likiiva na yanapelekwa hadi masoko ya nje, kama unafanyia Moshi nenda Usa River Arusha, kuna chama kinaitwa TAHA. Ukiweza waGoogle watakupatia mbegu idadi yeyote utakayo; hata miche na unapewa bure yakiiva wanakutafutia na soko wao wanakukata asilimia 10% ya malipo yako, hawana wizi wala konakona wateja wanao tayari.
 
Maparachichi aina ya HASS ndo mpango mzima.

Ni matamu kiasili, Na yanadumu Muda Mrefu Baada ya Kuvuna

All the Best Mkuu.
 
Safi sana mkuu, tunda hili ni zuri sana kwa afya.

Mie lazima nile japo moja kila siku asubuhi wakati wa chai pia nzuri kwenye smoothie au chakula chochote kuongezea radha na nutrients/virutubisho.

Ni vizuri wakulima mue mnawaelimisha wananchi faida ya kula matunda na mboga za majani kama njia ya kuongeza soko la bidhaa zenu.

Jamii yetu haina elimu ya kutosha kwenye umuhimu wa kula matunda na mboga za majani.
 
Safi sana mkuu, tunda hili ni zuri sana kwa afya.

Mie lazima nile japo moja kila siku asubuhi wakati wa chai pia nzuri kwenye smoothie au chakula chochote kuongezea radha na nutrients/virutubisho.

Ni vizuri wakulima mue mnawaelimisha wananchi faida ya kula matunda na mboga za majani kama njia ya kuongeza soko la bidhaa zenu.

Jamii yetu haina elimu ya kutosha kwenye umuhimu wa kula matunda na mboga za majani.
Safi mkuu kwa hamasa yako naimani wamekusikia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom