Kilimo cha Parachichi - Fahamu Aina, Namna ya Kulima na Masoko

MLIPAKODI

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
234
88
2353768_Hass_Avocadoes.jpg

Wadau,

Nahitaji kulima maparachichi. Kwa mwenye ufahamu zaidi naomba kujua changamoto na nini nifanyeje ili nieweze kufanikiwa.



MASWALI YA WADAU WENGINE KUHUSU ZAO HILI
Kama kuna mtaalamu wa kilimo naomba msaada kwa maeneo ya huku Katavi - Inyonga. Nimepanda miche ya parachichi nataka kuwekeza. Je, kwa eneo letu huku ninaweza kupata matokeo chanya?
Wakuu kilimo cha parachichi aina ya hass kwa sasa kinachukua umaarufu hasa kwa mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa, Arusha, Songea na kwingineko.

Mwenye kujua masoko yake hasa nje ya nchi na makampuni yanayonunua tujuzane please.
Kilimo cha maparachichi ni moja ya miradi bora wilaya ya Rungwe na sehemu zingine, wadau naomba kujua umbali unaofaa kati ya mche na mche.

Sent using Jamii Forums mobile app

MICHANGO/ UZOEFU WA WADAU KUHUSU ZAO HILI
Agronomy ya Parachichi


Hali ya hewa

-Ni tunda linalopenda sana sehemu za baridi, maeneo kama ya Rungwe-Mbeya, Njombe, Makete, linastawi vizuri sana, na huwa na Fatty Contenty kubwa

Joto

Nyuzi 15-25 Sentigrade

Muinuko
Mita 1200-1800 kutoka usawa wa baridi

Udongo
-Uwe kichanga tifutifu (Sandy loam), usiotuamisha maji

Aina za Parachichi

1. Zipo aina za kiasili. Kila sehemu kuna iana za parachichi ambazo ni za asili ya eneo husika, parchichi hizi, huwa ndefu sana, na mavuno machache

2. Zipo aina za kisasa (Chotara)
Ziko aina nyingi sana za Parachichi chotara, na hizi hapa chini ni baadhi ya zile maarufu hapa tanzania

i. Hass
-Hii ni aina maarufu sana katika aina za parachichi

View attachment 332265

- Ni tunda linalokuwa na vipere vipere
-Limechongoka juu na chini
-Linahifadhika kwa urahisi

ii. Aina ya pili ni Fuerte

View attachment 332266

-Hili ni aina ya parachichi lenye ngozi laini saini, ngozi yake inateleza kama imepakwa mafuta
-liko na mafuta mengi ila linawahi kuoza
-Ni zuri kwa matumizi ya kawaida , si kwa kusafirisha umbali mrefu
-Aina hii ikilimwa sehemu za miinuko na baridi sana, inafaa sana kutoa mafuta mengi yanayoweza kutumika kutengeza lotion na baadhi ya vyakula vya mifugo

iii. Aina ya tatu maarufu hapa tanzania -inaitwa X-ikulu
-Ana hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma)
-Mti wa aina hii huwa na majani mapana kama mti wa embe
-Mti huu huchukua muda mrefu sana kustawi
-Tunda lake huwa ni kubwa, na lina gharama sana


Upandaji wa Parachichi

Nafasi kati ya shimo na shimo

-Umbali wa kutoka shimo hadi shimo ni MITA 7
-UMbali wa kutoka mstari hadi mstari ni MITA 7

Lakini kipimo hicho hapo juu kitategemea sana na aina ya udongo wa shamba lako , kwa udongo wenye Phosphorus kwa wingi (P), kipimo hicho hakifai, maana baada ya mika 3-5 miche ya mistari miwili inayofuatana itakuwa imekuatana katikati

-Hivyo nafasi yaweza kuwa

8M X 8M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 63 KWA EKA 1
AU 9M X 9M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 49 KWA EKA 1
AU 10M X 10M- KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 40 KWA EKA 1

Ukubwa wa shimo-Shimo laweza kuwa futi 2.5 x futi2.5 x futi 2.5 = (sm 75 x sm 75 x sm 75) (Kimo x upana x urefu)

-Au kipimo cha futi 3 x futi 3 x futi 3= sm 90 x sm 90 x sm 90

Mbolea

-Mbolea za kupandia zitakazohitajika , ni moja wapo kati ya hizi
-Samadi, Mboji, DAP, au TSP-Lakini ni muhimu kupandia mbolea asilia kama samadi ukachanganya kidogo na TSP au DAP

Kipimo cha mbolea,
-Kama ni mbolea za asili (Samadi au Mboji)-Kiasi cha kilo 16 hadi 20 kinapaswa kiwekwe katika shimo miezi 3 kabla ya kupanda mche

-Kama utapandia mbolea za viwandani (TSP, DAP, Minjingu, NPK etc)
kiasi cha gramu 100 hadi 200 kiwekwe kwa kila shimo, ichanganywe vizuri na udongo, kisha mmea uwekwe na kumwagiliwa

KUKOMAA NA KUTOA MAVUNO
-Parachichi hasa hizi za kisasa, hukomaa baada ya miezi 18 hadi 24

MAVUNO
-Kwa mara ya kwanza mti mmoja wa parachichi unaweza kukupa kati ya matunda 50 hadi 100 kwa mche mmoja.
-Mavuno hueongezeka kadri umri unavyoongezeka
-Mti wa parachichi ukifikia umri wa miaka 4 hadi 5, unakuwa full maturity, na hivyo mti mmoja unaweza kukupa hadi matunda 1200 kwa mwaka mzima '

FAIDA
kwa kipimo cha mita 10 x mita 10, katika eka mmoja utakuwa na mita 40
-Kila mti baada ya mika 5 unaweza kukupa wastani wa matunda 1000
-Hivyo kwa miti 40, utakuw na jumla ya matunda 40 x 1000= 40,000
-Kila tunda kwa bei ya shambani uuze tsh 250, na unamatunda 40,000
-Hivyo utapata jumla ya tsh 250 x matunda 40,000= 10,000,000tsh (MILIONI 10)

Magonjwa ya parachichi

Parcahichi kama mimea mingine inashambuliwa sana hasa upande wa majani pamoja na matunda.

1. Yapo magonjwa ya majani, yanayosababishwa na fangasi/Ukungu, Algae, pamoja na wadudu, pamoja na lishe duni.

View attachment 332289
Jani lililoshambuliwa na Alga

View attachment 332290
Mite-Utitiri mweupe Avocado lililoshambuliwa na Utitiri

2.Magonjwa ya matunda

View attachment 332291 View attachment 332291

View attachment 332292
-Tatizo la Scab, husababishwa na Ukungu/Fangasi hasa wakati wa baridi/unyevu mwingi

View attachment 332293
Thrips wa avocado Matunda yaliyoathiriwa na Thrips

DAWA
-Dawa za kutibu wadudu kama Karate, Matchi, Actellic 50 EC, za faa sana kumaliza wadudu katika mmea wa parachichi

-Dawa za Ukungu kama Ridomil Gold, Ebony 72 WP (Mancozeb na Metalaxyn), Ivory, na Nordox zaweza kutumika kumaliza matatizo ya ukungu

-Lishe ya mmea

Mbolea za kukuzia kama CAN, UREA NA SA (hasa kwenye maeneo yenye magadi kwa wingi, na chumvi nyingi) yaweza kutumika kubalane PH YA Udongo.

-Booster=Mbolea za majani, maua na matunda kama vile Polyfeed Starter, Polyfeed finisher, Wauxal macro mix, Potphos, au Multi K , Ni muhimu sana zikatumika wakati wa maua, na matunda ili kuzuia matunda ya parachichi kuabort (Fruit abortion) yakiwa machanga, pamoja na kuzuia matunda kudondoka yakiwa machanga.

Hitimisho
Parachichi-Kama matunda mengine, ukililima kitaalamu, na ukaweka juhudi na maarifa linakutoa katika umaskini
Hass na X-Kulu ndizo zinakubalika kwa ubora na wingi wa mazao

Parachichi hupendelea sehemu zenye barid na unyevunyevu. Bila shaka Iringa nzima ina hali hyo. Ila ni vizuri ukipima udongo wako ili kujihakikishia kiwango cha rutuba katika shamba lako.

Idadi ya miche ni kuanzia miche 60 mpaka 100 kwa ekari moja.

Kuhusu mbegu nzuri inategemea na target ya soko lako. Ila kwa ujumla parachichi za kisasa kama Hass na X-Kulu ndizo zinakubalika kwa ubora na uwingi wa mazao.
Hass ndo parachichi tamu zaidi lenye soko la nje

Panda mbegu moja inaitwa Hass. Kwanza ndo parachichi tamu zaidi likiiva na yanapelekwa hadi masoko ya nje, kama unafanyia Moshi nenda Usa River Arusha, kuna chama kinaitwa TAHA. Ukiweza waGoogle watakupatia mbegu idadi yeyote utakayo; hata miche na unapewa bure yakiiva wanakutafutia na soko wao wanakukata asilimia 10% ya malipo yako, hawana wizi wala konakona wateja wanao tayari.
Parachichi zinalipa sana ila kabla hujafanya chochote jifunze mengi ndio uamue kama uwekeze au la

Mbegu bora ni HASS ni nzuri kwa maana kiwango cha mafuta, palatability na shlev life yake ni kubwa sana
Kama unalima Moshi Hakikisha hali ya hewa ya mahalia haizidi 30 nyuzi joto hali ya udongo usiotuamisha maji.
Mbegu zinapatikana hapo SIHA kwenye shamba la Africado, bei maelewano.

Uzalishaji: Kulingana na utaalamu ekari moja ni miche kat ya 40 - 106. hii inategemea unataka kuleaji miti yako, kama utaicha iwe bush 40 ni sahihi. kama unauwezo wa kulea vizuri bila kuiacha iwe miti mikubwa 72 - 106. ukienda siha utaona mashamba ni aina mbalimbali za upandaji.

Kuhusu mavuno: Mti mmoja unaweza kutoa hadi 200kg (export quality fruit) kama umelenga masoko mengine unaweza kupata hadi 400kg kwa mti wenye miaka 6 na kuendelea. mavuno yanaanza mwaka wa nne.

Bei ya maparachichi kwa msimu huu imesimama 1450/kg kwa yale yanayosarishwa nje. Kumbuka kuna size 12,14,16, 18, 20, 24, 26 kwa lugha nyepesi hiyo idadi intakiwa ifike 4kg

Parachichi zinalipa sana ila kabla hujafanya chochote nenda kawatembelee Africado na wakulima, ama nenda Njombe kawatembelee wakulima na Mnununuzi Korongo 3 au nenda Rungwe uonane na wakulima kupitia umoja wao UWAMARU, ongea nao kisha wanuunuzi KUZA Africa, Rungwe Avocado, Korongo 3, Biofarm/Biofresh usikie na upate mengi ndio uamue kama uwekeze au la.
Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wanaita parachichi Green Gold (Dhahabu ya Kijani)

Kusini hili zao huitwa green gold, wengi wametoka.

So far kuna mpaka viwanda vya usindikaji MBozi na NJombe vimeanza kujengwa. Ukipanda hass which mature at the age of 2.5 to 3 years, mti mmoja hutoa matunda 300 kwa mwaka mpaka 500. UKiwa na miti 70 kwa eka manake una matunda 21,000 sawa na 7000kg. Assume kilo moja ni 1500tshs (bei ya leo Njombe iyo) kwa eka unapata 10.5mil ukiwa na eka kumi sawa na 105mil kwa mwaka ambayo kwa mwezi ni sawa na mapato ya 8.7mil (mshahara wa mkurugenzi huo tena gross nadhani ikija take home lazima alambe 5mil)

Just assume mwaka mbaya ukapata just nusu ya iyo 105mil maisha yanasonga huna haja ya kuajiliwa ni kutafuta mtaji panda parachichi.

Mambo iko uku wahi mashamba Moshi Mbeya na NJombe kuwa na better future yako na ya wanao
Wananunuzi wanakuja nyumbani kwako kununua hata kama una mti mmoja

Mbeya, Njombe wananunuzi wanakuja nyumbani kwako kununua hata kama una mti mmoja. Kampuni ya Rungwe wao ndio kidogo wanamasharti hasa ya usafi, mti usiwe karibu na jalala au choo. Hata hivyo soko la ndani ni kubwa sana maana hatuna mahekta ya parachichi panda tu parachichi isitoshe wakenya ndio huja nyanda za juu kununua hivyo Arusha ni karibu kabisa na wakenya unaweza tafuta connection.

Wakenya wenzetu wana export to UK. Jambo lingine ni kwamba Parachichi za Tanzania zinaenda msimu tofauti na ulaya hata tulime ardhi ya mikoa yote inayostawi parachichi hatutoshelezi soko la dunia. Mikoa inayastawi parachichi ni Mbeya, Njombe, Arusha Kilimanjaro, Kgera na Kigoma. Kila sehemu inayostawi kahawa na chai parachichi itakubali.
Parachichi inayofanya vyema ni Hass sokoni na inayofanya vyema zaidi ni inayokomaa mwezi November hadi March. Kipindi hiki wazalishaji wakubwa wanakuwa hawana mzigo. Mzalishaji anaechelewa ni Israel yeye anaishiwa mzigo mwezi January.

Hivy ukiwa ukanda wa Busokelo na lupembe maeneo ya Mfriga, Madeke, Mfriga, Iduli , ikondo una uhakika wa kukutana na soko la ukahakika.

Uzoefu unaonyesha parachichi mwaka wa tatu utakupatia matunda 40 had 60 ambapo utapata kilo 10 hadi 15.

Kingine cha kuzingatia mbegu bora ya parachichi inatakiwa itokane na kikonyo cha mti ambao ni kizazi kisichozidi cha nne, hapa utapata size na shape nzuri ya Hass. Kununua mche ambao kikonyo kimetoka kizazi cha mbali ni hasara kwako matunda yataanza kutoa yasio na shape halis ya hass.
China wanahitaji mamilioni ya tani za parachichi kwa mwaka

China wanahitaji mamilioni ya tani za parachichi kwa mwaka (umesikia avocado deal waliyosaini Kenya na China)
Hapa ndio utaona uzuri wa kilimo cha matunda ya muda mrefu. Mti wa parachichi unadumu na kuvuna miaka 40+ kwahiyo hata uchumi ukiyumba miaka 7 mfululizo utavuna nakuuza kwa bei nzuri miaka ijayo. Tofauti sana na mazao ya muda mfupi kama mahindi, maharage, spices like ginger etc.

Uchumi hata ukiyumba upande wa chakula hii ni basic human need, research nyingi zina-favor avocado kutokana na health benefits zake nakufanya iwe kilimo salama zaidi.

Watu kila kukicha wanazidi kutambua umuhimu wa matunda kwa afya zao.

Idadi ya watu inazidi kuongezeka na hivyo watumiaji wa agriproducts wanazidi kuongezeka.

Dalili njema ipo hata hapa Tanzania ambapo kila mkoa, wilaya mpaka kijijini bei ya parachichi vibandani/mezani kila mwaka ni 500 iwe masika, kiangazi tofauti na embe, chungwa, pear.

Iwapo utafuata masharti ya soko la nje na kufanya organic farming, utapeta hata uchumi uyumbe vipi.
 
MLIPAKODI

Mimi si mkulima ila nilipata sehemu hii:

NJIA BORA YA KUZALISHA MICHE YA MAPARACHICHI

Utangulizi
Maparachichi ni matunda ya bustanini na mashambani kwa wakulima wadogo.

Maparachichi yana matumizi mengi yenye faida kubwa kwa wakulima na wadau wengine.

Matunda ni chakula chenye viini lishe bora kama Vitamini (A,B2, C, D,E,K ) na madini ( P,K, Mn, S ) ambavyo vinalinda mwili, mafuta kwa wingi ( 5-30%) ambayo huleta joto mwilini, protini (1-5%) ambayo hujenga mwili na kiasi cha calories 250 ambayo huleta nguvu mwilini.

Tofauti na matunda mengine, maparachichi ni malighafi ya viwandani kutengenezea madawa ya ngozi pamoja na vipodozi mfano mafuta ya nywele na ngozi,shampoo, sabuni na kadhalika. Miti hutumika kama kuni, mbao nk.

Vilele majani yake na mbegu hutumika kama dawa. Mapararachichi ni zao la chakula na biashara na huuzwa na wakulima na wafanya biashara wadogo na wakubwa kwa ajili ya kipato.

Aina za maparachichi Kuna aina nyingi za maparachichi zisizopungua 30 nyingi nzikiwa za kienyeji.

Hizi zimekuwepo katika mifumo yetu ya uzalishaji hasa katika nyanda za juu kusini na kasikazini kwa muda marefu, lakini uzaaji wake ni mdogo kutokna na ubora hafifu, kuzeeka na kuchakaa kwa miti na utunzaji hafifu.

Aina bora za mapararchici ambazo zimefanyiwa utafiti na kukubalika kwa wakulima na walaji ni pamoja na; HASS, FUERTE, WEISAL, SIMMONDS, EX- TENGERU, IKULU, MWAIKOKESYA, NABALI.

Aina hizi hutofautiana kwenye urefu wa mti, uzaaji wa matunda, ukubwa wa matunda, ladha na muda wa kukomaa.

Aina hizi zinazaa matunda mengi na bora pia huchukua muda fupu kukomaa.Kiasi cha matunda kwa mti kwa msimu ni kati ya 300 hadi 800 kutegemeana na matunzo.

Njia bora ya kuzalisha miche ya maparachichi kwa njia ya vikonyo Njia ya miche bora ni kutumia vikonyo. Faida zinazotokana na njia hii ni:

• Miti kuchukua muda mfupi kukomaa na kuzaa matunda (miaka 3-3 ½)
• Miti huwa na umbo na urefu wa wastani
• Kuzalisha miche yenye tabia moja. Mti haubadili tabia
• Kuepuka magonjwa hasa virusi
• Miche mingi kuzalishwa kwa wakati mmoja
• Kumwezesha mkulima kufanya uchaguzi

Hatua za kufuata kabla ya kuzalisha miche kwa njia ya vikonyo:

1. Kuzalisha miche ya kubebeshea vikonyo kutokana na mbegu
2. Kubebesha vikonyo kwenye miche

Vifaa vinavyohitajika:
• Viriba –mifuko ya plastiki yenye kipenyo cha 5’’-6’’ na urefu wa 5’’-6’’
• Udongo safi usio na magonjwa hasa wa msituni, samadi, mchanga/pumba za mchele kwa uwiano wa 3:1:1
• Mbolea ya TSP
• Mbegu za maparachichi

Njia;
1. Andaa kitalu sehemu wazi na tengeneza kichanja ili kuzuia jua na mvua.
2. Changanya udongo na jaza kwenye viriba
3. Panda mbegu kwenye viriba
4. Panga viriba kwenye kitalu
5. Mwagilia maji
6. Baada ya wiki 2-3mbegu zitaanza kuota
7. Tunza miche hadi kufikia umri wa kubebeshwa miezi 3-4 au unene wa pensile.

Ukuaji wa miche hutegemea hali ya hewa. Sehemu za joto mbegu huchipua upesi na miche kukua haraka.

Kubebesha vikonyo
Vifaa:

• Visu maalumu kwa ajili ya kubebeshea
• Jiwe la kunolea
• Mikanda ya nailoni (tapes)
• Mifuko ya nailoni kufunikia kikonyo
• Vikonyo Uchaguzi wa tawi kwa ajili ya vikonyo:
• Ni muhimu kuchagua tawi zuri kwenye mti uliokomaa na kuzaa matunda ili kuharakisha kukomaa na kuzaa kwa mti uliobebeshwa .
• Chagua kikonyo chaenye macho au vijichoza (buds) vyenye afya nzuri.
• Usichague kikonyo chenye maua
• Kikonyo kikianza kuchipua hakifai kwa kubebesha kwa sababu ni kichanga
Mambo muhimu katika ubebeshaji
• Miche inayobebeshwa itoke kwenye jamii moja, kwa mfano mparachichi na mparachichi, limau na limau au limau na chungwa nk.
• Urefu wa kikonyo uwe sm 15-20 na chonga kikonyo bapa sm 2- 3
• Mche wa kubebeshea kikonyo ukatwe juu kwenye shina sm 20-25 kutoka usawa wa udongo na kata kipenyo cha sm 2-3. Urefu wa kipenyo ulingane na urefu wa bapa la kikonyo
• Sehemu ya mmea yenye mirija ya kupitisha chakula na maji zihakikishwe zinaungana.
• Pachika kikonyo kwenye kipenyo cha shina na hakikisha kikonyo kina simama wima kwenye shina
• Fungia vizuri kikonyo kwenye shina na mkanda (strip) wa nailoni nyeupe. Tendo hili lifanyike kwenye mazingira safi na haraka ili utomvu kwenye bapa na kipenyo usikauke
• Funika mche na mfuka wa nailoni nyeupe yaani tube au rambo inayopitisha mwanga mradi isiwe nyeusi
• Tunza miche na hakikisha kuna unyevu wa kutosha kwenye mche na kitaluni ili miche ipone
• Hakikisha maji hayagusi ungio ili kuepuka maambukizi ya magonjwa
• Baada ya wiki 2-3 vikonyo vilivyopona vitaanza kuchipua
• Ondoa machpukizi/maotea yote yanayojitokeza chini ya ungio yaani kwenye shina la kibebesheo
• Majani yakijitokeza kwenye kikonyo ondoa mfuko uliofunika kikonyo
• Tunza miche kitaluni kwa kumwagilia maji na kuondoa machipukizi/maotea
• Baada ya miezi 3-4 miche itakuwa na majani 6-8 dalili ya kutosha kupandikizwa shambani

Utayarishaji wa shamba
• Chagua eneo la wazi lenye rutuba
• Eneo liwe na mteremko wa wastani ili maji yasituwame
• Eneo liwe jirani na chanzo cha maji
• Tayarisha shamba mapema kabla ya msimu wa mvua

Uchimbaji wa mashimo
• Pima nafasi za kupanda ambazo ni: 6m x 5m, 6m x 6m au 6m x 8m. Kwa nafasi hizi unaweza kuyarisha mashimo kati 220-400 kwa hekta
• Chimba mashimo kwa nafasi zilizopendekezwa. Urefu wa shimo sm 75 upana, sm 75 na kina sm 75
• Tenganisha udongo wa chini na wa juu
• Changanya udongo wa juu na samadi iliyooza kabisa debe moja
• Rudisha udongo wa juu kwenye shimo
• Weka kijiti katikati ya shimo
• Rudishia udongo wa chini
• Acha shimo kwa muda wa wiki 2 hadi mwezi 1 kabla ya kupanda

Kupanda
• Panda miche wakati wa masika
• Chimba kashimo kadogo katikati ya shimo kubwa ( palipo wekwa kijiti) waweza kuchanganya mbolea ya TSP gm 50 na CAN gm 50
• Chagua miche yenye afya nzuri
• Ondoa kiribu (tumia kisu au wembe)
• Panda mche kwenye kishimo
• Sehemu iliyounganishwa isiguse udongo
• Shindilia vizuri na mwagilia maji ya kutosha

Utunzaji miche shamabani
• Fungua mikanda ya nailoni (tapes) iliyounganisha shina na kikonyo wiki 2-3 baada ya kupanda mche
• Shughuli nyingine muhimu ni palizi, kumwagilia maji, kuondoa machipukizi na kuzua magonjwa na wadudu

• Kupogole: ondoa matawi yanayogusa udongo
• Baada ya mwaka mmoja weka mbolea TSP gm 100 na CAN gm 100 kwa mche ili iweze kukua haraka na kuzaa matunda mapema
 
Last edited by a moderator:
Mwenye detail zaidi wataalam wa kilimo cha parachichi atusaidie wandugu.
 
Wadau,

Nahitaji kulima maparachichi. Kwa mwenye ufahamu zaidi naomba kujua changamoto na nini nifanyeje ili nieweze kufanikiwa.

Mkuu sijui nianzie wapi maana haujafunguka, umbali toka mti hadi mti mi mita 10 mstari hadi mstari mita 10. Mbegu unaweza otesha kwenye viriba, kitalu au shambani moja kwa moja.

Kuandaa kitaru
lima na lainisha kitalu,panda mbegu zako kwa umbali wa 30cm-40cm, hakikisha kitako(upande mnene) unaangalia china na kwembamba juu, fukia kwa udongo kidogo na tandaza nyasi mwagilia mpaka ziote.

Kuhamishia shambani
chimba masimo 30cm na ondoa udongo weka pembeni. chimba tena 30cm zaidi, chukua udongo wa kwanza changanya na mbolea kisha urudishe shimoni, udongo ulioutoa ndani yaan 30cm za ndani usambaze nje ya shimo weka alama ktk kila shimo miche ikiwa tayari panda.

Fanya hivyo mashimo yote, kama kuna zaidi sema.
 
Vizuri utumie miche iliyoungwa inazaa 2 to 3 years ila ya mbegu itakuchukua up to 7 years, kama unashamba Moshi jiunge na Africado wao wanakuuzia miche then ukizalisha wananunua kwako ndugu, watafute.
 
Badilika kaka huu ulimwengu mwingine unapitwa na mengi. Ukibadilika karibu kuna hamasa nyingi sana.
 
Nahitaji kupewa elimu hiyo wadau juu ya

- Mbegu bora ya kupanda.
- Ekari moja ni miti mingapi?
- Hatua za kuandaa shamba mpaka kupanda.
- NA ZAIDI,WILAYA YA KILOLO ENEO LA MAKAO MAKUU YA WILAYA KWA WANAOPAFAHAMU. JE, PATAFAA?

Nitashukuru sana ukija na full details.
 
Parachichi hupendelea sehemu zenye barid na unyevunyevu. Bila shaka Iringa nzima ina hali hyo. Ila ni vizur ukipima udongo wako ili kujihakikishia kiwango cha rutuba ktk shamba lako.

Idadi ya miche ni kuanzia miche 60 mpaka 100 kwa ekari moja.

Kuhusu mbegu nzuri inategemea na target ya soko lako. Ila kwa ujumla parachichi za kisasa kama Hass na X-Kulu ndizo zinakubalika kwa ubora na uwingi wa mazao.
 
Agronomy ya Parachichi

Hali ya hewa

-Ni tunda linalopenda sana sehemu za baridi, maeneo kama ya Rungwe-Mbeya, Njombe, Makete, linastawi vizuri sana, na huwa na Fatty Contenty kubwa

Joto
Nyuzi 15-25 Sentigrade

Muinuko
Mita 1200-1800 kutoka usawa wa baridi

Udongo
-Uwe kichanga tifutifu (Sandy loam), usiotuamisha maji

Aina za Parachichi
1. Zipo aina za kiasiliKila sehemu kuna iana za parachichi ambazo ni za asili ya eneo husika, parchichi hizi, huwa ndefu sana, na mavuno machache

2. Zipo aina za kisasa (Chotara)
Ziko aina nyingi sana za Parachichi chotara, na hizi hapa chini ni baadhi ya zile maarufu hapa tanzania

i. Hass
-Hii ni aina maarufu sana katika aina za parachichi

Hass.jpg

- Ni tunda linalokuwa na vipere vipere
-Limechongoka juu na chini
-Linahifadhika kwa urahisi

ii. Aina ya pili ni Fuerte

Fuerte.png

- Hili ni aina ya parachichi lenye ngozi laini saini, ngozi yake inateleza kama imepakwa mafuta
- liko na mafuta mengi ila linawahi kuoza
- Ni zuri kwa matumizi ya kawaida , si kwa kusafirisha umbali mrefu
- Aina hii ikilimwa sehemu za miinuko na baridi sana, inafaa sana kutoa mafuta mengi yanayoweza kutumika kutengeza lotion na baadhi ya vyakula vya mifugo

iii. Aina ya tatu maarufu hapa tanzania -inaitwa X-ikulu
-Ana hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma)
-Mti wa aina hii huwa na majani mapana kama mti wa embe
-Mti huu huchukua muda mrefu sana kustawi
-Tunda lake huwa ni kubwa, na lina gharama sana


Upandaji wa Parachichi

Nafasi kati ya shimo na shimo


- Umbali wa kutoka shimo hadi shimo ni MITA 7
- UMbali wa kutoka mstari hadi mstari ni MITA 7

Lakini kipimo hicho hapo juu kitategemea sana na aina ya udongo wa shamba lako , kwa udongo wenye Phosphorus kwa wingi (P), kipimo hicho hakifai, maana baada ya mika 3-5 miche ya mistari miwili inayofuatana itakuwa imekuatana katikati

- Hivyo nafasi yaweza kuwa

8M X 8M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 63 KWA EKA 1
AU 9M X 9M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 49 KWA EKA 1
AU 10M X 10M- KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 40 KWA EKA 1

Ukubwa wa shimo-Shimo laweza kuwa futi 2.5 x futi2.5 x futi 2.5 = (sm 75 x sm 75 x sm 75) (Kimo x upana x urefu)

-Au kipimo cha futi 3 x futi 3 x futi 3= sm 90 x sm 90 x sm 90

Mbolea

- Mbolea za kupandia zitakazohitajika , ni moja wapo kati ya hizi
- Samadi, Mboji, DAP, au TSP-Lakini ni muhimu kupandia mbolea asilia kama samadi ukachanganya kidogo na TSP au DAP

Kipimo cha mbolea,
- Kama ni mbolea za asili (Samadi au Mboji)-Kiasi cha kilo 16 hadi 20 kinapaswa kiwekwe katika shimo miezi 3 kabla ya kupanda mche

-Kama utapandia mbolea za viwandani (TSP, DAP, Minjingu, NPK etc)
kiasi cha gramu 100 hadi 200 kiwekwe kwa kila shimo, ichanganywe vizuri na udongo, kisha mmea uwekwe na kumwagiliwa

KUKOMAA NA KUTOA MAVUNO
-Parachichi hasa hizi za kisasa, hukomaa baada ya miezi 18 hadi 24

MAVUNO
- Kwa mara ya kwanza mti mmoja wa parachichi unaweza kukupa kati ya matunda 50 hadi 100 kwa mche mmoja.
- Mavuno hueongezeka kadri umri unavyoongezeka
- Mti wa parachichi ukifikia umri wa miaka 4 hadi 5, unakuwa full maturity, na hivyo mti mmoja unaweza kukupa hadi matunda 1200 kwa mwaka mzima '

FAIDA
kwa kipimo cha mita 10 x mita 10, katika eka mmoja utakuwa na mita 40
-Kila mti baada ya mika 5 unaweza kukupa wastani wa matunda 1000
-Hivyo kwa miti 40, utakuw na jumla ya matunda 40 x 1000= 40,000
-Kila tunda kwa bei ya shambani uuze tsh 250, na unamatunda 40,000
-Hivyo utapata jumla ya tsh 250 x matunda 40,000= 10,000,000tsh (MILIONI 10)

Magonjwa ya parachichi


Parcahichi kama mimea mingine inashambuliwa sana hasa upande wa majani pamoja na matunda.

1. Yapo magonjwa ya majani, yanayosababishwa na fangasi/Ukungu, Algae, pamoja na wadudu, pamoja na lishe duni.


Screenshot from 2016-03-24 14:02:22.png

Jani lililoshambuliwa na Alga

1.png

Mite-Utitiri mweupe Avocado lililoshambuliwa na Utitiri

2.Magonjwa ya matunda

2.png
2.png


3.jpg

-Tatizo la Scab, husababishwa na Ukungu/Fangasi hasa wakati wa baridi/unyevu mwingi

4.png

Thrips wa avocado Matunda yaliyoathiriwa na Thrips

DAWA
-Dawa za kutibu wadudu kama Karate, Matchi, Actellic 50 EC, za faa sana kumaliza wadudu katika mmea wa parachichi

-Dawa za Ukungu kama Ridomil Gold, Ebony 72 WP (Mancozeb na Metalaxyn), Ivory, na Nordox zaweza kutumika kumaliza matatizo ya ukungu

-Lishe ya mmea

Mbolea za kukuzia kama CAN, UREA NA SA (hasa kwenye maeneo yenye magadi kwa wingi, na chumvi nyingi) yaweza kutumika kubalane PH YA Udongo.

-Booster=Mbolea za majani, maua na matunda kama vile Polyfeed Starter, Polyfeed finisher, Wauxal macro mix, Potphos, au Multi K , Ni muhimu sana zikatumika wakati wa maua, na matunda ili kuzuia matunda ya parachichi kuabort (Fruit abortion) yakiwa machanga, pamoja na kuzuia matunda kudondoka yakiwa machanga.


Hitimisho
Parachichi-Kama matunda mengine, ukililima kitaalamu, na ukaweka juhudi na maarifa linakutoa katika umaskini
 
Nahitaji kupewa elimu hiyo wadau juu ya.
-Mbegu bora ya kupanda.
-Ekari moja ni miti mingapi?
-Hatua za kuandaa shamba mpaka kupanda.
-NA ZAIDI,WILAYA YA KILOLO ENEO LA MAKAO MAKUU YA WILAYA KWA WANAOPAFAHAMU,JE PATAFAA?

Nitashukuru sana ukija na full details.

Kama haupo mbali na Mbeya, tembelea Rungwe Avocado Company. Ni kampuni inayozalisha maparachichi na miche ya hass avocado kwa kufuata kanuni za kilimo endelevu na huuzwa masoko ya ulaya. kuna wakulima kama 4000 ambao huzalisha kwa mkataba na hii kampuni. miche huuzwa sh 3500/, ekari moja kwa 7mx7m ni miti 80.

Zaidi ya hizo mbolea, parachichi kustawi vizuri ukitumia mbolea ya yara mila wina gm 175 kwa mti mdogo na gm 350 kwa mti mkubwa. kabla ya maua kuanza, piga mbolea ya yala bortrac mil 60 kwa pampu ya lita 15 na matunda yanapoanza piga mbolea ya yara zintrac mil 60 kwa pampu ya lita 15. Kwa maelezo zaidi nicheki inbox
 
Vizur utumie miche iliyoungwa inazaa 2 to 3 years ila ya mbegu itakuchukua up to 7 years,kama unashamba Moshi jiunge na africado wao wanakuuzia miche then ukizalisha wananunua kwako ndugu,watafute
Jamani naomba sana msaada namna ya kuzungumza moja kwa moja na watu wa AFRICADO, nimewatafuta sana kwa njia ya mtandao bila mafanikio. tafadhari mwenye mawasiliano ya moja kwa moja anisaidie, nina shida nao sana. check me inbox please
 
Salaam,

Tanzania yetu bado ina fursa nyingi sana, moja ya fursa iliyokuwa imeachwa sana ni kilimo cha matunda jamii ya Parachichi, a.k.a avocado. Matunda haya huzaa vizuri nyanda za juu. Zipo jamii nyingi za avocado, lakini aina inayotesa sokoni ni Hass.

Kwa nini kilimo hiki ni fursa nzuri, kuna sababu nyingi, mojawapo ni kwamba, kwenye soko la dunia sisi tuna nafasi ya pekee. Yale mataifa makubwa kwa uzalishaji humaliza msimu wa kuvuna mwezi may, na sisi huku ndio msimu unaanza. Kwa hiyo avocado toka latin America, south America na Australia zinakuwa zimeshaisha kwenye soko la fresh fruits wakati sisi ndio tunaanza.

Sababu nyingine ni soko la ndani, soko la Parachichi linakuwa kwa kasi sana,naamini miaka michache ijayo parachichi itakuwa lulu zaidi.

Sababu nyingine ni matumizi ya viwandani, kama itatokea Rwanda kama sio Burundi wakaimarisha kiwanda chao, hali itakuwa tete sana, maana parachichi itakuwa adimu sana.

Parachichi ya kisasa huanza kutoa mazao baada ya miaka mitatu na ile ya asili huvuta mpaka miaka saba na ushee. Changamoto ya kilimo hiki ni ardhi, pamoja na ukubwa wa ardhi ya Tz, lakini ni sehemu ndogo sana inayofaa kwa kilimo hiki. Mbaya zaidi maeneo hayo wanakaa/wanaishi wajanja kiasi kwamba kupata eneo inakuwa kazi kubwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom