Kilimo cha Parachichi - Fahamu Aina, Namna ya Kulima na Masoko

KILIMO BORA CHA PARACHICHI
Tunda hili lina faida nyingi sana, mbali ya kutumika kama zao la kiuchumi lakini pia hutumika kuimarisha afya ya mwili

1. Faida za Parachichi upande wa Lishe

-Tunda lina vitamini zifuatazo

1. Lina Vitamini A-husaidia sana kuimarisha Macho kuona vizuri

2. Lina Vitamini B (B1-B12)- Husaidia sana mfumo wa misuli ya mwili kuwa sawasa na kuuepusha mwili na matatizo ya nerve

3. Lina Vitamini C-Husaidia sana upande wa kuimarisha ngozi, kwa sababu liko na mafuta, lina zaidi ya mara 4 ya virutubisho vya vitamini C vinavyopatikana katika machungwa

4. Lina vitamini D-ambapo husaidia sana kuimarisha mifupa ya mwili

5. Lina vitamini E-hii husaidia sana kuimarisha seli za uzazi, linasaidia sana kuongeza nguvu na utengenezwaji wa seli za uzazi

6. Lina vitamini K-Husaidia sana kuganda kwa damu, na kuongeza uzalishaji wa chembe hai nyekundu za damu

Madini- (Mineral Elements)
Ni tunda lenye

1. Madini ya Chuma kwa wingi (Fe)-Haya huaidia sana utengenezwaji wa damu, na kuongeza uwezekano wa damu kuwa na oxygeni ya kutosha na kusafirishwa kwa urahisi

2. Madini ya Calcium-Lina madini ya calcium, yanayosaidia kama ufanyaji wa kazi wa seli hai za mwili

3. Lina virutubisho vingine vidogo vidogo vingi, vinavyotakiwa katika ufanyaji kazi mzuri wa selli hai za mwili

2. Agronomy ya ParachichiHali ya hewa

-Ni tunda linalopenda sana sehemu za baridi, maeneo kama ya Rungwe-Mbeya, Njombe, Makete, linastawi vizuri sana, na huwa na Fatty Contenty kubwa

Joto
Nyuzi 15-25 Sentigrade

Muinuko
Mita 1200-1800 kutoka usawa wa baridi

Udongo
-Uwe kichanga tifutifu (Sandy loam), usiotuamisha maji

Aina za Parachichi
1. Zipo aina za kiasiliKila sehemu kuna iana za parachichi ambazo ni za asili ya eneo husika, parchichi hizi, huwa ndefu sana, na mavuno machache

2. Zipo aina za kisasa (Chotara)
Ziko aina nyingi sana za Parachichi chotara, na hizi hapa chini ni baadhi ya zile maarufu hapa tanzania

i. Hass
-Hii ni aina maarufu sana katika aina za parachichi
-Ni tunda linalokuwa na vipere vipere
-Limechongoka juu na chini
-Linahifadhika kwa urahisi

ii. Aina ya pili ni Fuerte
-Hili ni aina ya parachichi lenye ngozi laini saini, ngozi yake inateleza kama imepakwa mafuta
-liko na mafuta mengi ila linawahi kuoza
-Ni zuri kwa matumizi ya kawaida , si kwa kusafirisha umbali mrefu

-Aina hii ikilimwa sehemu za miinuko na baridi sana, inafaa sana kutoa mafuta mengi yanayoweza kutumika kutengeza lotion na baadhi ya vyakula vya mifugo

iii. Aina ya tatu maarufu hapa tanzania -inaitwa X-ikulu
-Ana hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma)
-Mti wa aina hii huwa na majani mapana kama mti wa embe
-Mti huu huchukua muda mrefu sana kustawi
-Tunda lake huwa ni kubwa, na lina gharama sana

Upandaji wa Parachichi

Nafasi kati ya shimo na shimo

-Umbali wa kutoka shimo hadi shimo ni MITA 7
-UMbali wa kutoka mstari hadi mstari ni MITA 7

Lakini kipimo hicho hapo juu kitategemea sana na aina ya udongo wa shamba lako , kwa udongo wenye Phosphorus kwa wingi (P), kipimo hicho hakifai, maana baada ya mika 3-5 miche ya mistari miwili inayofuatana itakuwa imekuatana katikati

-Hivyo nafasi yaweza kuwa

8M X 8M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 63 KWA EKA 1
AU 9M X 9M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 49 KWA EKA 1
AU 10M X 10M- KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 40 KWA EKA 1

Ukubwa wa shimo-Shimo laweza kuwa futi 2.5 x futi2.5 x futi 2.5 = (sm 75 x sm 75 x sm 75) (Kimo x upana x urefu)

-Au kipimo cha futi 3 x futi 3 x futi 3= sm 90 x sm 90 x sm 90

Mbolea
-Mbolea za kupandia zitakazohitajika , ni moja wapo kati ya hizi
-Samadi, Mboji, DAP, au TSP-Lakini ni muhimu kupandia mbolea asilia kama samadi ukachanganya kidogo na TSP au DAP

Kipimo cha mbolea,
-Kama ni mbolea za asili (Samadi au Mboji)-Kiasi cha kilo 16 hadi 20 kinapaswa kiwekwe katika shimo miezi 3 kabla ya kupanda mche

-Kama utapandia mbolea za viwandani (TSP, DAP, Minjingu, NPK etc)
kiasi cha gramu 100 hadi 200 kiwekwe kwa kila shimo, ichanganywe vizuri na udongo, kisha mmea uwekwe na kumwagiliwa

KUKOMAA NA KUTOA MAVUNO
-Parachichi hasa hizi za kisasa, hukomaa baada ya miezi 18 hadi 24

MAVUNO
-Kwa mara ya kwanza mti mmoja wa parachichi unaweza kukupa kati ya matunda 50 hadi 100 kwa mche mmoja.
-Mavuno hueongezeka kadri umri unavyoongezeka
-Mti wa parachichi ukifikia umri wa miaka 4 hadi 5, unakuwa full maturity, na hivyo mti mmoja unaweza kukupa hadi matunda 1200 kwa mwaka mzima '

FAIDA
kwa kipimo cha mita 10 x mita 10, katika eka mmoja utakuwa na mita 40
-Kila mti baada ya mika 5 unaweza kukupa wastani wa matunda 1000
-Hivyo kwa miti 40, utakuw na jumla ya matunda 40 x 1000= 40,000
-Kila tunda kwa bei ya shambani uuze tsh 250, na unamatunda 40,000
-Hivyo utapata jumla ya tsh 250 x matunda 40,000= 10,000,000tsh (MILIONI 10)

Magonjwa ya parachichi
Parcahichi kama mimea mingine inashambuliwa sana hasa upande wa majani pamoja na matunda1. Yapo magonjwa ya majani, yanayosababishwa na fangasi/Ukungu, Algae, pamoja na wadudu, pamoja na lishe duniJani lililoshambuliwa na Alga

Mite-Utitiri mweupe Avocado lililoshambuliwa na Utitiri

2. Magonjwa ya matunda
Yasababishwayo na fangasi/Ukungu, Wadudu,na Lishe dunipia-Tatizo la Athracnose husababishwa na Ukungu/Fangasi

-Tatizo la Scab, husababishwa na Ukungu/Fangasi hasa wakati wa baridi/unyevu mwingi

Thrips wa avocado Matunda yaliyoathiriwa na Thrips

DAWA

-Dawa za kutibu wadudu kama Karate, Matchi, Actellic 50 EC, za faa sana kumaliza wadudu katika mmea wa parachichi

-Dawa za Ukungu kama Ridomil Gold, Ebony 72 WP (Mancozeb na Metalaxyn), Ivory, na Nordox zaweza kutumika kumaliza matatizo ya ukungu

-Lishe ya mmea

Mbolea za kukuzia kama CAN, UREA NA SA (hasa kwenye maeneo yenye magadi kwa wingi, na chumvi nyingi) yaweza kutumika kubalane PH YA Udongo.

-Booster=Mbolea za majani, maua na matunda kama vile Polyfeed Starter, Polyfeed finisher, Wauxal macro mix, Potphos, au Multi K , Ni muhimu sana zikatumika wakati wa maua, na matunda ili kuzuia matunda ya parachichi kuabort (Fruit abortion) yakiwa machanga, pamoja na kuzuia matunda kudondoka yakiwa machanga.

Hitimisho

Parachichi-Kama matunda mengine, ukililima kitaalamu, na ukaweka juhudi na maarifa linakutoa katika umaskini
........................................................................

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IMG_2391.JPG

Huo maparachichi niliupanda miaka minne iliyopita sio wa kisasa, nilinunua parachichi sokoni nikavutiwa nalo maana lilikua tamu sana nikaamua nipande mbegu yake.

Ni mzao wa kwanza lakini una matunda zaidi ya 300 japokua sijayahesabu, sijatumia mbolea yoyote ya dukani wala dawa. Ila hapo ulipo ndio kuna eneo la kutupia taka za nyumbani na maji ya jikoni.

Nimehawishika sana kupanda mingine japokua eneo langu ni dogo ila naweza nikapata hela ya mboga.

IMG_3046.JPG
 
Ahsante sana kaka, hivi kwa makadirio acre moja inaweza gharimu shs ngapi kwa mtiririko kama huo hapo ulivyoelezea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naishi singida nahitaji kulima parachichi naomba wazoefu wa maeneo na watalamu mnishauri nimkoa gani nasehemu gani nzuri kwa kilimo hicho kati ya Mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe ikizingatia maeneo ambayo parachichi zitakubali,upatikanaji wa mashamba,miundombinu na soko .natanguliza shukuran kwa wote mtakaonishauri nakunipa ushilikiano.
 
Naishi singida nahitaji kulima parachichi naomba wazoefu wa maeneo na watalamu mnishauri nimkoa gani nasehemu gani nzuri kwa kilimo hicho kati ya Mikoa ya iringa,mbeya na njombe ikizingatia maeneo ambayo parachichi zitakubali,upatikanaji wa mashamba,miundombinu na soko .natanguliza shukuran kwa wote mtakaonishauri nakunipa ushilikiano.
Ngoja wajuvi waje,kwa taarifa ndogo Njombe ndio
 
Naishi singida nahitaji kulima parachichi naomba wazoefu wa maeneo na watalamu mnishauri nimkoa gani nasehemu gani nzuri kwa kilimo hicho kati ya Mikoa ya iringa,mbeya na njombe ikizingatia maeneo ambayo parachichi zitakubali,upatikanaji wa mashamba,miundombinu na soko .natanguliza shukuran kwa wote mtakaonishauri nakunipa ushilikiano.
Njombe naona zinastawi sana.
Kule bwana nimeona watu wametoboa kisa hayo matunda, juzi nimeona mzee kabisa anasukuma ndinga wenyeji wanasema kapata mpunga kwenye parachchi.
Isitoshe kuna wanafanyabiashar wanakuja kutoka kenya, A.kusini na matrei yao kwa kilo moja 1500.
Good enough kuna kiwanda kinajengwa cha kuchakata hayo matunda Njombe.
Kwa maana ya soko na udongo yanastawi sana Njombe.
 
Nimesoma mahali heading wakulima wa Australia wanalia baada ya bei ya parachichi kushuka mno kama sio sana..nakuarifu tu ndg mkulima..sina nia mbaya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom