Kilimo cha nyanya msimu wa 2021/2022

CoderM

Senior Member
Jun 15, 2015
102
272
Narudia tena kilimo cha nyanya msimu mwingine wa masika baada ya kumalizana na kiangazi.

Msimu uliopita nilipanda miche 1000 tu kama sehemu ya kujifunza kwa vitendo.

Matokeo yalikua sio mazuri sana kutokana na makosa ya kitaalamu lakini nimejifunza mengi sana kwenye kilimo cha nyanya.

Msimu huu nitalima kwenye green house na kwenye open field.

Greenhouse nitatumia mbegu ya Anna F1 miche 700

Open field nitatumia mbegu ya Faida F1(msimu uliopita ilifanya vizuri pamoja na kukosa matunzo muhimu nimeamua kuirudia tena) hii nitapanda miche 2500.

Kwa green house nitaweka mbegu kwenye kitalu kuanzia tar 1 Nov

Kwa open field nitaweka mbegu tar 10 Nov

Napokea maoni na ushauri, na nitakua natoa mrejesho huku kinachoendelea mpaka mavuno.

Location Songea
 
Bosi naomba kujua songea sehem gani?
 
Kilimo cha nyanya kinahesabiwa wakati kwa wiki

Wiki hii ilianza rasmi wiki ya kwanza(nilimechelewa kuanza kutokana na changamoto za kupata udongo mzuri wa kupandia mbegu kwenye tray).

Shughuli zilizofanyika ni;

1. kuwatika mbegu kwenye tray.
2. Kusafisha kitalu nyumba(green house) na kueambaza mbolea ya samadi kwenye matuta.
3. Kusafisha mfumo wa maji(drip) kwenye greenhouse
4. Kusafisha eneo la nje kwa ajili ya nyanya zitakazopandwa nje.
5. Kuandaa vitu muhimu vitakavyohitajika kwa wiki nne za mwanzo (yaani siku 21 za mbegu kwenye kitalu) na siku saba baada ya kupandikiza.

Vitu vinavyohitajika ni
1. Dawa ya ukungu
2. Mbolea ya majani(booster)
3. Mbolea ya kupandia(nitatumia Yara otesha)
4. Dawa ya wadudu kwa ajili ya nyanya nitakazopanda nje ya green house.
 
Green house inavyoonekana nje, ndani na open field.
IMG_20211105_065222_503.jpg
IMG_20211105_174739.jpg
IMG_20211107_181042_202.jpg
 
Hata mbegu ya Hasira na Imara pia Tanya Mwanga zinafanya vizuri sana !! Changamoto ya Nyanya kila step yake ya ukuaji ina changamoto !! Zinahitaji uangalizi wa karibu sana !! Tofauti na mazao kama Pilipili hoho
 
Ni kweli kabisa.

Ila kila mbegu ina maeneo yanafanya vizuri. Ukiona eneo ulilokuwepo mbegu haijakupa changamoto ya magonjwa na wadudu ni bora ukakomaa nayo kuliko kujaribu nyingine
 
Nyanya ya biashara hailimwi green house braza labda itakuwa ya mboga tu, kama unahitaji nyanya kibiashara lima shambani kabisa angalau uanzie ekari moja na kuendelea.
Nini (Zao) kinalimwa green house kibiashara?
 
Back
Top Bottom