MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

Wakuu Mimi ni kijana mpambanaji na mwaka huu nilitaka kujikita katika kilimo Cha mpungaa kwa umwagiliaji na nimependekeza kulimia ruvu

Hivyo basi naombeni muongozo katika hio scheme ya ruvu kuhusu

1.Upatikanaji wa mashamba

2.Gharama zake kuanzia

3.Mbegu

4.mbolea

Pia kama kuna mtu mwenye ushauri au muongozo zaidi ya hayo nilotaja naomba anisaidie.
 
Kiongozi Ruvu hakuna shamba kwa msimu huu.
Kama una mpango wa kulima jaribu kulipia mwaka huu ulime mwaka ujao.
Kukodi Heka laki 3 mpk 4 inategemea na sehemu.
Bei ya kukodi heka inaunganisha gharama za kulimiwa na kupigiwa harrow (kuchabangiwa).
Yaani utalimiwa na kuchambangiwa shamba kwa bei hio hio moja. Huna haja ya kukodi Tractor tena.
Mbegu unaotesha pamoja na wenzako kwenye shamba la karibu yako litakalo chaguliwa kuotesha mbegu za msimu.
Mbolea ni maamuzi yako.
Kuna choice nyingi za Mbolea. Inategemea na mfuko wako.

Nenda ofisini omba kuonana na Manager wa Skimu utasaidiwa.


Swali la ziada nikute PM.

All the best
 
kahtaan,
Nashukuru boss kwa maelezo yako ila nikusumbue tena mashamba hamna kwa mwaka huu ni Kwamba nimechelewa yameisha au mwaka huu hawalimi scheme imefungwa
 
Katavi,maji ya moto kukodi lak2 kulima na kupanda kama lak6 jumla.gunia 25,35
Hii ndio matumizi sahihi ya jamii forum. Tumeshapata taarifa ya fursa ya kilimo cha mpunga karibia kila pembe ya Tanzania. Bado KATAVI ili kabla ya kuingia kwenye ujasiriamali huo kichwa kichwa uwe umetathmini pro and cons, usije ukaingia kichwa kichwa kama ufugaji wa kware na sungura. Hongera uliyeanzisha uzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahio tusuburisubiri kwanza?Maji yapungue sio
Maji mengi mkuu
IMG_20200322_110144.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimelima hekari tano za mpunga mkoani morogoro wilaya ya mqlinyi je naweza vunq junia ngap wakuu anisaidie kwa alie na uzoefu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Waulize wakulima wenzio uliopakana nao wao wanaliona vizur shamba lako na uzoefu waliokuwa nao ktk eneo hilo,lakini pia wanaweza jua au kukuuliza ju ya huduma ulizofanya kama ni kwa kufuata utaalamu au mkumbo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom