Kilimo cha mpunga Morogoro/Kimara-Mbeya

mby real

New Member
Nov 3, 2010
3
1
Wakuu Mimi ni kijana mpambanaji na mwaka huu nilitaka kujikita katika kilimo Cha mpungaa kwa umwagiliaji na nimependekeza kulimia Kapunga/morogoro

Hivyo basi naombeni muongozo katika hio

a. maeneo ambayo ni mazuri
b.Upatikanaji wa mashamba

c.Gharama zake kuanzia

d.Mbegu

e.mbolea

Pia kama kuna mtu mwenye ushauri au muongozo zaidi ya hayo nilotaja naomba anisaidie.
 
Rekebisha,ni Chimala na si Kimara
 
Nenda katavi unakodi eka moja kwa laki ni ardhi ambayo haijatumika sana kwa Kilimo..mbegu nazan upatikanaji sio shida
 
Wakuu Mimi ni kijana mpambanaji na mwaka huu nilitaka kujikita katika kilimo Cha mpungaa kwa umwagiliaji na nimependekeza kulimia Kapunga/morogoro

Hivyo basi naombeni muongozo katika hio

a. maeneo ambayo ni mazuri
b.Upatikanaji wa mashamba

c.Gharama zake kuanzia

d.Mbegu

e.mbolea

Pia kama kuna mtu mwenye ushauri au muongozo zaidi ya hayo nilotaja naomba anisaidie.
Nakushauri nenda kalime wilaya ya momba kilimo cha umwagiliaji ktk kijiji cha nkala
1.kukodi heka moja-200,000
2.kukatua-40000
3.kuvuruga-40000
4.kupanda-80000
5.palizi 30000(siyo lazima maana palizi siyo kubwa)
 
Wakuu Mimi ni kijana mpambanaji na mwaka huu nilitaka kujikita katika kilimo Cha mpungaa kwa umwagiliaji na nimependekeza kulimia Kapunga/morogoro

Hivyo basi naombeni muongozo katika hio

a. maeneo ambayo ni mazuri
b.Upatikanaji wa mashamba

c.Gharama zake kuanzia

d.Mbegu

e.mbolea

Pia kama kuna mtu mwenye ushauri au muongozo zaidi ya hayo nilotaja naomba anisaidie.
Habari ya mapambano kijana mwenzangu!
Kulingana na hoja yako, ninapenda kuchangia baadhi ya mambo niyajuayo juu ya kilimo hiki cha mpunga. Mimi ni mkulima wa zao hili ktk mkoa wa Songwe wilaya ya Momba bonde la Kamsamba.
SIFA ZA BONDE HILI
~Ardhi yenye rutuba
~Uhakika wa maji
~Mavuno mengi
~Mpunga unaotoa mchele mzuri na wenye soko kubwa, ni mchele namba 1 kwa soko la mikoa ya nyanda za juu kusini.
~Gharama za wastani ktk uendeshaji
~Matumizi ya mbolea si ya lazima
~Miundombinu ya barabara iko vizuri
~Rasilimali watu inapatikana
~Shamba la 200000 unaweza panda na kuvuna mara2 kwa msimu

GHARAMA/EKA1
✓Kukodi shamba 100000-200000
✓Kukatua/kulima(ng'ombe) 40000
✓Kusawazisha/kuvuruga 40000
✓Mbegu plastik mbili 20000 kwa tahadhari ila plastik moja inatosha
✓Kitalu cha mbegu 10000
✓Kung'oa mbegu 25000
✓Kupanda 70000-100000
✓Kung'olea/palizi 25000-40000
✓Kufyeka 50000
✓Kusomba 25000
✓Kupiga 50000
Hizi ndizo hatua muhimu za kuzingatiwa ktk kilimo cha mpunga.

RATIBA YA MSIMU
>Kusafisha shamba Disemba mwanzoni
>Kuandaa kitalu na kuotesha mbegu Disemba mwanzoni.
>Kulima Disemba mwishoni, januari au februari mwanzoni.
>Kuvuruga na kupanda wiki moja au zaidi baada ya kulima
>Palizi/kung'olea wiki 3 na kuendelea baada ya kupanda.
>Kuvuna mwezi April hadi Mei.

Kama kuna swali au mchango wowote wa ziada unakaribishwa.
 
Back
Top Bottom