MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

CHASHA FARMING,
Kwa kwelu hapa ndo huwa tunachemka....unakuta mtu kafungia gumia 600 ndani, anakuja kufungulia baada ya miezi sita, gunia kama kumi zimeliwa na panya, na baadi zimepoteza ubora
 
Wakuu mi huwa nalima mpunga kwa kutegemea mvua huku Mwanza, Mwaka huu msimu haujaenda vzuri, na hvyo hali ni mbaya....
katika pita pita zangu nikakutana na jamaa anafanya kilimo cha umwagiliaji mpunga huku huku Mwanza, anatoa maji ziwani mpak shambani, kiukweli amescore vzur, na mpak sa hv amelima shamba jingine tena, yan yeye ni non stop....

Kwa kweli alinifikrisha sana , lakn inavyoonekana jamaa ana mtaji mkubwa make system alivyoitengeneza inaonesha yupo vizur upande wa capital Istoshe anatumia electric machine kupump maji.....

Nimevutiwa sana na hiki kilimo sababu mpunga ni kilimo cha uhakika, changamoto kubwa huwa ni upatikanaji wa mvua.....

nami nataka nifanye hiki kilimo cha umwagiliaj japo mtaji wangu ni mdog kama 2mil hv...nimepata shamba ambalo ni umbali wa 100m toka ziwani....hvyo nina maswali kadhaa kwa wanajukwaa kwa wenye uzoefu wanisaidie kunijibu ili kama naanza nianze na kama siwezi bas nitafute namna nyingine....

1.Naulizia mashine ya bei nafuu inayoweza kusukuma maji M50-M100 horizontal, Mashine ambayo yaweza saidia kwa hekari angalau 2
2. Naulizia kias cha mafuta mashine hyo inaweza tumia kwa siku na nitahtajika kumwagilia kila baada ya siku ngap?
3.Naulizia pia mbegu nzuri , make na mpango wa kulima mwezi ujao wa sita, nimesita kdog kutumia mbegu za kienyeji hvyo nahtaj mbegu za kisasa ili nipate mavuno mazur.
Natanguliza shukrani wakuu
 
Mawazo mazuri sana, kwa umbali huo unahitaji pump ya kawaida (maarufu pump ya bustani).. kwangu mimi boss inch 3 ni nzuri na inadumu bei ni laki 3-4, koromeo mita 6 @10,000, pipe 1 la kitambaa inch 3 yenye mita 100/150 inauzwa 150,000, inch 2 ni 125,000

Utahitaji tank 1 au 2 za lita 3000 na roller pvc 1 mita 150 bei ni 60-70,000.
Nenda hapo mwanza mjini stand ya Sahara barabara ya rwagasore zungukia kila duka piga sound utapata vyote hivyo kwa bei hizo ni wewe tu na sound yako

Hiyo budget inatosha sana kuweka mfumo wa maji
 
Pia ni vyema ukapima na udongo ili kujua utatumia mbolea ipi na zao gani litakubali vzr zaidi
 
Mawazo mazuri sana, kwa umbali huo unahitaji pump ya kawaida (maarufu pump ya bustani).. kwangu mimi boss inch 3 ni nzuri na inadumu bei ni laki 3-4, koromeo mita 6 @10,000, pipe 1 la kitambaa inch 3 yenye mita 100/150 inauzwa 150,000, inch 2 ni 125,000
Utahitaji tank 1 au 2 za lita 3000 na roller pvc 1 mita 150 bei ni 60-70,000.
Nenda hapo mwanza mjini stand ya Sahara barabara ya rwagasore zungukia kila duka piga sound utapata vyote hivyo kwa bei hizo ni wewe tu na sound yako

Hiyo budget inatosha sana kuweka mfumo wa maji
Mkuu shukrani sana.....ngoja nifanye hvo,
 
Narubongo,
Tank la Maji pamoja na hizo rola hazihitajiki maana mpunga umwagiliaji wake ni kwa njia Flood irrigation (unamwagilia moja kwa moja kwenye majaruba) hivyo unatakiwa kununua generator na pipe ya kuvuta Maji moja kwa mja mpaka kwenye jaruba au unaweza tengeneza Farrow (mifereji ya kupelekamaji) au tafta mtaalam wa umwagiliaji atakujibu maswali yako yote
Watumieni wataalam wa kilimo
 
Tank la Maji pamoja na hizo rola hazihitajiki maana mpunga umwagiliaji wake ni kwa njia Flood irrigation (unamwagilia moja kwa moja kwenye majaruba ) hivyo unatakiwa kununua generator na pipe ya kuvuta Maji moja kwa mja mpaka kwenye jaruba au unaweza tengeneza Farrow (mifereji ya kupelekamaji) au tafta mtaalam wa umwagiliaji atakujibu maswali yako yote
Watumieni wataalam wa kilimo
Hizo njia zote zinawezekana, nimemwambia option ya kuwa na tank kwasababu kuna kipindi huwa tunatumia hayo maji kiwiziwizi na mbaya zaidi usumbufu upo sana iwapo utatumia hizo njia za mifereji. Ukitumia tank inapunguza gharama ya labor unajaza maji kwenye tank, pipe zinapeleka kwenye kila jaluba (kazi yako ni kufunga na kufungua koki)
 
M
Nipo moshi lower
Kukodi shamba mita mia laki tatu,
Kuhudumia shamba hadi mavuno wastani kama laki 7-8 hivi
Kwa mbegu za huku ni saro 5 na 64 huwa ni muda wa miezi mitatu hadi minne mpaka mavuno..
Kwa mita mia waweza pata gunia 17 hadi ishirini
Mkuu Kama umetumia laki 7 kwa heka halafu ukapata wastani wa gunia 17 je bei ya kuuza huwaga ni sh ngp kwa gunia ili upate faida
 
M
Mkuu Kama umetumia laki 7 kwa heka halafu ukapata wastani wa gunia 17 je bei ya kuuza huwaga ni sh ngp kwa gunia ili upate faida
Bei ikiwa juu sana huwa inafika hadi laki ishirini,ikishuka hata themanini unauza kulingana na uingiaji wa mipunga kutoka maeneo mengine..bei zinakua shindani
 
Mkuu vipi upatikanaji wa hayo mashamba ya kukodi? Na je eneo liko ndani ya irrigation scheme?
Nipo moshi lower
Kukodi shamba mita mia laki tatu,
Kuhudumia shamba hadi mavuno wastani kama laki 7-8 hivi
Kwa mbegu za huku ni saro 5 na 64 huwa ni muda wa miezi mitatu hadi minne mpaka mavuno..
Kwa mita mia waweza pata gunia 17 hadi ishirini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom