MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

kwa kawaida hekta moja ni kuanzia gunia 8/13 inategemea na matunzo ya shamba kwenye mchele pia inategemea na aina ya mpunga maana kuna ambao kukatika ni nature na mashine pia ila hiyo hesabu yako unazungumzia kuanzia hekta 15
 
Mkuu utakua unazungumzia kilimo cha kienyeji bila lakini kama mkuu hapo juu akipata hekari nne/hekta mbili zilizopo kwenye irrigation scheme na akaziendeleza kisasa unaweza vuna gunia mpaka 120.
Kwa sababu hekari moja inaweza kukupa gunia 30 kwa wastani na hekta yaweza kukupa gunia 50 mpaka 70 hivyo ukawa umefikia malengo ya mavuno unayohitaji..
 
Nahitaj ushaur wenu.. .
Ni shamba la ekari ngap naweza kutoa gunia 100 la mpunga au gunia 90 za mchele??

Kuhusu gunia 90 za mchele hapa tuongelee gunia za kilo mia mia hivyo jumla yake itakua kilo 9000. Gunia la mpunga la kilo tisini hutoa wastani wa kilo 55 mpaka 60 za mchele hivyo kupata tani 9 utahitaj gunia 150 mpaka 170 za mpunga kutegemea na mashine utakayo tumia kukobolea iwe ya ku grade au ya kawaida (maarufu kama vibelenge), hivyo kwa gunia 150 mpaka 170 utahitaji hekari 6 au hekta tatu kufikia target unayotaka.
 
Mkuu utakua unazungumzia kilimo cha kienyeji bila lakini kama mkuu hapo juu akipata hekari nne/hekta mbili zilizopo kwenye irrigation scheme na akaziendeleza kisasa unaweza vuna gunia mpaka 120.
Kwa sababu hekari moja inaweza kukupa gunia 30 kwa wastani na hekta yaweza kukupa gunia 50 mpaka 70 hivyo ukawa umefikia malengo ya mavuno unayohitaji..
Ni wapi naweza pata shamba la kumwagilia
 
Yaani humu kuna watu wanatka kujifanya wanajua kila kitu kwa sasa system ya SRI ukifuata vizur yaaan mbona utacheka mwenyewe fuata ushauri wa kchibo
 
Ni wapi naweza pata shamba la kumwagilia

Mkuu mi nafahamu sehemu mbili ambazo ni mwanzugi-igunga (tabora) na kapunga-mbarali (mbeya). Ifakara pia huwa nackia wanalima sana mpunga ila cjawahi fikai nadhani wanajukwaa wengine wanaweza kukusaidia na kututajia maeneo mengine pia.
 
kwa hapa Tanzania kulima shmba zaid hekta 5 na kuweza kuapply arrigation ni ngum wengi tunalima kilimo cha kutegemea mvua
 
Nahitaj ushaur wenu.. .
Ni shamba la ekari ngap naweza kutoa gunia 100 la mpunga au gunia 90 za mchele??
Ukilima vizuri eneo la ekari tano na kufuata mbinu zote unapata zaidi ya gunia hizo. Tafuta eneo lenye maji ya uhakika Kama kwenye irrigation schemes.
 
Mimi nililima shamba la mpunga Nyatwali Irrigation Scheme(Bunda) nilipata gunia 43 kwa ekari moja baada ya kufuata maelekezo ya kitalaam.
Maelezo yako yamenivutia. Je unaweza kunimegea kidogo hayo maelekezo ya kitaalam? Mimi nina eneo la (70 X 70) X 10 kando ya mto usiokauka mwaka mzima.
 
kwa anayependa kumiliki eneo lake kwa kilimo cha mpunga kwa bei isiyozidi laki moja
1464412611389.jpg
1464412611389.jpg
 
hamna asiyependa ila ni muhimu kufahamu eneo lenyewe liko wapi, ni accessible na pia kama linazalisha vyema
 
Mashamba yanapatikana kijiji cha iyendwe,kasinde na vijiji vingine ambavyo sivifahamu vizuri,umwagiliaji bado haujafika huko ila kuna Mito ya kutosha ambayo mvua ikinyesha hata Mara mbili inatililisha maji kwa msimu mzima pia mpango wa kupeleka miundombinu ya umwagiliaji ipo ktk mpango wa serikali kwani ni eneo kubwa zaidi ya hekta 60000 pia upande wa kipato kwa shamba ambalo ndiyo Mara ya kwanza kulimwa kipato si kizuri ina range kwenye gunia 10-20 za debe 7 ila kama shamba si jipya kipato ni gunia 20-30 kwa kilimo cha kawaida si kitaalamu
 
Barabara kipindi cha masika si nzuri sana inabidi uzunguke ila kuanzia mwezi wa 6 barabara zinapitika vizuri,umbali kutoka barabara ya lami iendayo sumbawanga hadi shambani ni km 10 hadi km 22
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom