MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

Niko njiani kutoka kuvuna Mofu, imenichukua wiki 3 kukata, kupiga, kupepeta na kusafirisha. Nililima eka 10 ila mavuno si mazuri, ni kwa sababu ya kulima kwa rimoti, hata hivyo siwezi kusema nimepata hasara.

Nimeamua msimu huu nitalima kisasa na nitahakikisha nakuwepo shamba kwenye kila hatua niwepo na nisimamie.

Nakushauri usiingie kichwa kichwa, anza hata na eka 10 uone changamoto na upate uzoefu kwanza, mambo si rahisi hivyo jipange na uwe tayari kuingia mfukoni ipasavyo ingawa si rahisi kukosa kabisa.
 
Wana JF nataka kujaribu Kilimo cha Mpunga cha umwagiliaji Dakawa Naomba kujua taarifa zaidi kuhusu kilimo hicho katika yafuatayo,

1.Matatizo yanayokumba kilimo hicho
2.Soko la mpunga kwa sasa likoje
3.Faida zake na ekari moja unaweza kuproduce gunia ngani.
wanajamii nahitaji msaada wenu ndio niko kwenye utafiti wa kujua zaidi ili nisiingie kichwa kichwa.
 
Zar,

Habari yako ndugu yangu.

Mimi sijalima huko lakini ninaye mtu wangu wa karibu ambaye alikuwa analima huko na bado anaendelea lakini anakatishwa tamaa sana na mambo yanayotokea pale. Kwanza wenyeji wenyewe ni choka mbaya hawana uwezo wa kulima pale kwakuwa kilimo cha Pale ni cha umwagiliaji na kinahitaji pesa ili kuweza kuchangia mafuta ndio Pump ifanye kazi ya ku push maji kutoka mtoni yaingia mashambani. Sasa wenyeji hawapendi sana kuona watu kutoka Dsm na sehemu nyingine wanalima pale. So kama unaenda ulifahamu hili swala lipo.Nadhani wenyeji wana wish ile sehemu ikae pori kama ilivyoachwa na wachina kuliko kuona wageni wanakuja kulima.

Huyu jamaa alipoanza kulima alipewa sehemu pori na uongozi (kamati ambayo imeteuliwa pale kusimamia) akalima visiki akaanza kulima mpunga kwenye hivyo vi Plot vyake. Lakini jambo la ajabu baadae wakamnyang'anya wakamgawia mtu mwengine. Kwa kisingizio eti amechukua sehemu kubwa so wakampunguzia na hakupewa compensation yeyote.

Sometimes maji nayo yanakuwa changamoto kwakuwa si wakati wote mpunga unahitaji maji. Ili uweze kuvuna mpunga inabidi shamba liwe kavu kabisa. Sasa hapo lazima wote muende sawa wakati wa kumwagia pampu ikiwashwa inabidi wote muwe kwenye stage ya kuhitaji maji shambani.

Kuna changamoto nyingi za ki menejimenti pale mahala , hilo lazima ulifahamu.
 
Nashukuru mdau kwa ushauri mzuri coz hilo pia ni jambo la msingi na pia ni tatizo kubwa kwa maendeleo ya nchi hii just imagine watu hawana uwezo wa kulima eneo hilo lakini pia hawataki wanaoweza kulima walime.Ila nashukuru kwa kunijulisha ilo mapema ili nisijeingia kichwa kichwa nikijua kila kitu kipo ok
 
Nashukuru mdau kwa ushauri mzuri coz hilo pia ni jambo la msingi na pia ni tatizo kubwa kwa maendeleo ya nchi hii just imagine watu hawana uwezo wa kulima eneo hilo lakini pia hawataki wanaoweza kulima walime.Ila nashukuru kwa kunijulisha ilo mapema ili nisijeingia kichwa kichwa nikijua kila kitu kipo ok

Zar,

Nisikukatishe tamaa bandugu. Nimewasiliana na huyu bwana hivi karibuni amenieleza kwamba kuna menejimenti mpya pale ambayo inafanya kazi kwa bidii na mambo yana improve. Sema bado wananchi wa pale wana machungu sana na wale wanaowaita wageni ambao wanalima pale, wao wanajifanya na wao wana haki ya kulima pale lakini wakipewa eneo linawashinda bado wanakodisha kwa mtu wa mjini.

All the best bro...
 
kuhusu mashamba sijajua coz mostly wanaongelea mashamba ya kukodi labda tuulize wadau wengine wanasemaje
 
Re: Naenda Ifakara Kulima Mpunga.

Ni wazo zuri sana, kwani kilimo ukiingia vizuri na kulima kisasa, kitakutoa tu. Hasa kilimo cha umwagiliaji, hivyo nakushauri angana mahindi lia na option ya kule Madibira, Mbeya. Huko kuna kilimo cha mpunga cha umwagiliaji na miundo mbinu ipo tayari. Unaweza kukodi ekari kadri unavyoweza na labour ya kukodi ipo nje nje.
Hebu jaribu hiyo option pia.
 
Re: Naenda Ifakara Kulima Mpunga.

Ni wazo zuri sana, kwani kilimo ukiingia vizuri na kulima kisasa, kitakutoa tu. Hasa kilimo cha umwagiliaji, hivyo nakushauri angana mahindi lia na option ya kule Madibira, Mbeya. Huko kuna kilimo cha mpunga cha umwagiliaji na miundo mbinu ipo tayari. Unaweza kukodi ekari kadri unavyoweza na labour ya kukodi ipo nje nje.
Hebu jaribu hiyo option pia.

Thanks mzee kwa ushauri wako km una information zozote zap huko hebu nipatie nitashukuru maana sina information zozote za huko heka wanakodisha sh ngapi
 
Je,unasumbuliwa na ndege waharibifu kwenye shamba lako la mpunga?.Usipate tabu,fanya kama ifuatavyo;jitahidi kuwakamata japo ndege kumi waharibifu~>Wakate miguu yao kisha ikaange mpaka ibaki majivu~>Yale majivu changanya na maji kisha nenda kayapake hayo majivu kona zote za shamba lako.

Baada ya kufanya hivyo kuwa huru kufanya shughuli zako kwani ndege waharibifu wote watafanya shamba lako kama sehemu ya kupumzikia tu,njaa ikiwauma watakwenda mashamba ya jirani zako.SOURCE:Mzee mmoja mkulima wa mpunga kijiji cha Mvumi,wilayani Kilosa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom